ZIWA NYASA LOTE NI MALAWI, TANZANIA HAINA HATA PUNJE YA ENEO".... MGOMBE URAIS NCHINI MALAWI AFUNGUKA
- Get link
- X
- Other Apps
Mgombea
Urais wa Democratic Progressive Party (DPP) nchini Malawi, Peter
Mutharika, amesema hakuna sababu za kufanya majadiliano kuhusu Ziwa
Malawi ambalo Tanzania wanaliita Ziwa Nyasa.
Mutharika, ambaye ni mwanasheria, aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi Mkoa wa Kati.
Akikaririwa na gazeti la Nyasa Times, Mutharika alisema Tanzania haina cha kuambulia kwa Ziwa Malawi.
Kiongozi
huyo ambaye hakuwapo katika mkutano wa Rais Joyce Banda na wapinzani
kuzungumzia mustakabali wa ziwa, aliwahakikishia Wamalawi kuwa wasiwe na
wasiwasi wa mvutano huo.
Mutharika ziwa lote ni mali ya Malawi na akisisitiza kuwa, Tanzania haina hata punje ya eneo.“Hakuhitajiki
majadiliano, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi, litakuwa la Malawi,”
alisema Mutharika ambaye alichukua masomo ya Sheria Tanzania.
“Tanzania
inatumia nafasi ya udhaifu wa uongozi wetu, lakini ukweli, hawana hata
tone la eneo... Tutakapoitwa kwenye uchaguzi ujao mwakani, tutamaliza
haya yote.
"Nitaleta
meli nyingi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, kutengeneza ajira za
kutosha kwa vijana,” alisema Mutharika huku akishangiliwa na wafuasi
wake.
Tanzania
inataka kugawana ziwa, lakini Malawi imegomea mpango huo na suala hilo
liko katika majadiliano ambayo Banda alisema kama mwafaka haukupatikana
ifikapo Septemba 30, Malawi itapeleka suala hilo Mahakama ya Kimataifa
(ICJ).
Subscribe for updates:
Email:
Submit
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment