ULIMWENGU MZIMA WALAANI MAUAJI YA RAIA NCHINI MISRI



Baada ya polisi wa Misri kutumia nguvu kuvunja mikusanyiko ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa Muhammad Musri na kuua mamia ya watu na kujeruhi maelfu ya wengine mjini Cairo, walimwengu wameonesha wasiwasi mkubwa na kulaani mauaji hayo. 

Umoja wa Mataifa umelaani vikali ukandamizaji huo wa polisi wa Misri dhidi ya waandamaji wanaotaka kurejeshwa madarakani Rais Muhammad Mursi, suala ambalo limesababisha maelfu ya watu kuuawa.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia imelaani vikali mauaji na ukandamizaji wa jeshi la Misri dhidi ya wananchi wa nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa ikisema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa karibu matuko ya Misri na inabainisha wasiwasi wake mkubwa kutokana na yanayojiri nchini humo.

" Iran imetahadharisha kwamba machafuko ya sasa nchini Misri yanaweza kuitumbukliza nchi hiyo katika vita vya ndani.

Wakati huo huo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani kuuawa wafuasi wa rais aliyepinduliwa Muhammad Mursi mjini Cairo na kutaka maafisa wa Misri waache kuua raia na kulenga maadamano ya amani. 

Ukandamizaji na mauaji dhidi ya raia yanayojiri nchini Misri yameendelea pia kulaaniwa na taasisi mbalimbali na nchi tofauti duniani kama vile Ufaransa, Uturuki, Tunisia, Russia, Qatar na kadhalika.

Comments

Popular posts from this blog