RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AFANYA MABADILIKO MAKATIBU WAKUU
- Get link
- X
- Other Apps
NA MAGRETH KINABO NA ELEUTERI MANGI – MAELEZO
RAIS
Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za
utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu
wakuu katika wizara mbalimbali, ambapo wapo waliohamishwa,
wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.
Kauli
hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Rais
amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za
Serikali katika ngazi hizo za juu,”alisema Balozi Sefue.
Mabadiliko
yaliyofanywa kwa upande wa makatibu wa wakuu ni kama ifuatavyo; Dk.
Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Joyce Mapunjo
Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki(awali alikuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Masoko, Jumanne Sagini
amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa(TAMISEMI) awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi wa Waziri Mkuu –
TAMISEMI.
Wengine
ni Dk. Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,awali
alikuwa Naibu Katibu Wizara ya Fedha, Dk. Patrick Makungu amekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali
alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Alphayo Kitanda amekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali
alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.
Dk.
Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,awali alikuwa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Dk.Uledi
Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, awali
alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Profesa Sifuni
Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
Wanaofuata
ni Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri, Anna Maembe amekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, awali alikuwa
Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo, Sihaba Nkinga amekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu
Katibu Mkuu Wizara hiyo na Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo.
Balozi
Sefue aliongeza kwamba Katibu Mkuu aliyepewa uhamisho
ni Peniel Lyimo ambaye anahamia Ofisi ya Rais –
Ikulu kwenye ‘Presidential‘s Delivery Bureau’ kama Naibu Mtendaji Mkuu
mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo
mwanzoni alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.
Makatibu
wakuu watakaopangiwa kazi nyingine ni Sethi Kamuhanda aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Kijakazi
Mtengwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na
Watoto na Injia Omari Chambo aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Uchukuzi.
Kwa
upande wa Makatibu wanaostaafu ni Patrick Rutabanzibwa ambaye alikuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amestaafu kwa
hiari.
Aidha Balozi Sefue alisema Rais Kikwete pia amefanya uteuzi wa naibu makatibu wakuu wapya na kuwapa uhamisho baadhi yao.
Alisema
naibu makatibu wakuu wapya walioteuliwa ni Angelina Madete Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Regina
Kikuli Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Zuberi Sumataba Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI- anayeshughulikia suala la
elimu katika ngazi za Serikali za Mitaa , Edwin Kiliba Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.
Wengine
Deodatus Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI
ambaye atashughulikia saula la afya upande wa Serikali za Mitaa, Dk.
Yamungu Kayandabila amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula
na Ushirika, Profesa Adolf Mkenda Naibu Katibu Mkuu ya Fedha
anayeshughulikia sera, Dorothy Mwanyika Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni.
Rose
Shelukindo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Dk. Selassie Mayunga Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ,Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Monica Mwamunyange Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Uchukuzi, Consolata Mgimba Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi.
Naibu
makatibu wakuu wengine ni Profesa Elisante ole Gabriel Laizer amekuwa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na
Armantius Msole Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
Balozi
Sefue aliwataja naibu makatibu wakuu waliopewa uhamisho kuwa ni John
Mngondo ambaye amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia ametoka Wizara ya Uchukuzi katika nafasi hiyo, Selestine
Gesimba amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii anatoka Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya
Nishati na Madini kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais.
Wanaofuatia
ni Maria Bilia amehamia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Nuru Milao anahamia Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Maliasili na
Utalii.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment