NATAFUTA MWENZA WA MAISHA (MUME)






Habari zenu wanajamii.

Jamani maisha ni safari ndefu na inahitaji uvumilivu na ujasiri. Nimetumia ujasiri wangu kwa kujitokeza katika jukwaa hili ili kuweza kupata mwenza ambae atakuwa mume kama Muumba akibariki. Kwa aliye na nia ya dhati haswa naomba tuwasiliane kwa private message.
Sifa zangu
Umri: Miaka 30
Umbo:Ni wa kawaida sana, na kwa wale wanopenda makalio makubwa, mimi sina jamani, ni bora kuwa mkweli!
Urefu: Centimeter158
Rangi: Maji ya maharage
Elimu: Degree mbili
Kazi: Muajiriwa wa serikali
Dini:Islam
Sifa za Mtarajiwa
Umbo: asiwe na kitambi kwa kweli
Urefu: itakuwa vyema kama akinizidi maana isije leta zahma
Rangi: yeyote
Elimu: Degree
Kazi: Ni muhim maana maisha ni magumu sana
Dini: Islam, ila uwe hujaoa!
Najua kunawatakoleta mzaha, ni kawaida sana kwenye jamii. Nipo tayari kwa maswali mtakayoyauliza. Karibuni!
Weka Sifa zako..Acha number ya Simu ama E-mail

Comments

Popular posts from this blog