MSANII WA KIKE BONGO MOVIE AMWANDIKIA BARUA RAIS KIKWETE!!


Yobnesh Yusuph(Batuli) ambaye ni actress maarufu Swahiliwood amemuomba Rais Jakaya Kikwete alivunje Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) na kuliunda upya. Leo kupitia akaunti yake ya twitter muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto na kupendwa na mashabiki wengi wa filamu ali-tweet moja kwa moja akimtaja JK kwa kuandika "ujumbe wa sikukuu ya Eid kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana, vunja baraza la BASATA uliunde upya".
Ingawa Batuli hakutaja moja kwa moja kwanini baraza hilo linalosimamia sanaa ikiwemo tasnia ya filamu nchini livunjwe lakini kwa muda mrefu wasanii wakiwemo wa filamu na muziki wamekuwa wakililalamikia baraza hilo kuwa linafanya mambo kienyeji na baadhi ya wasanii kudai kukumbana na urasimu wanapotaka kufanya kazi zao za sanaa.
Wengine wanadai hata hatua iliyopigwa sasa katika sanaa nchini ni juhudi za wasanii wenyewe pasipo sapoti ya kutosha kutoka BASATA. Baadhi ya wasanii wa filamu wamekuwa pia wakitaka TAFF ndiyo ipewe mamlaka kamili ya kusimamia shughuli zote za tasnia ya filamu nchini kutokana na BASATAkuwepo muda mrefu lakini Sanaa ya Tanzania bado haijapewa hadhi ya sekta rasmi na kuwa na sera ya kueleweka katika kumkomboa msanii na kuzidi kupiga hatua.
Hivi karibuni pia mwanamuziki Diamond Platinumz alikaririwa akisema BASATA ndiyo wa kulaumiwa kwa kutokuwa na tuzo nyingine za muziki mpaka sasa kwa kuwa chombo hicho kimekuwa kikiweka kauzibe kwa watu wanaotaka kuazisha tuzo mbalimbali za sanaa ikiwemo hata katika tasnia ya filamu.

Comments

Popular posts from this blog