MBINU ZA KUPANGA JINSIA YA MTOTO WA KUZAA ( MVULANA AU MSICHANA ) KABLA MKEO HAJASHIKA MIMBA


Mpendwa  msomaji  wa  JUKWAA  LA  WAKUBWA, Maada  yetu  ya  leo  ni  mbinu za kupanga  jinsia  ya  mtoto  wa  kuzaa  kabla  mkeo  hajashika  mimba....

Siku  hizi  ulimwengu  umeendelea  sana, matatizo  mengi  yanatibika  kwa  msaada  wa  wataalamu...Hakuna   tena  haja  ya  kupigana  na  kupeana  talaka  kisa  jinsia  ya  mtoto...


Somo  letu  ni  lefu  sana, hivyo  tunaomba  uwe  mvumilivu.Kutokana  na  utefu  wa  somo  hili, tutaandika  sehemu  fupi  katika  mtandao  huu  na  sehemu  nyingie  itawekwa  katika  JUKWAA  LA  WAKUBWA  ambako  kutakuwa  na  majadiliano  ya  wazi  miongoni  mwa  wasomaji  wetu....

Aidha, somo  la  leo  litajikita  zaidi  katika  mbinu  za  kuzaa  mtoto  wa  kike.

Ni vipi jinsia ya mtoto huainishwa?
Kinyume na wengi wanavyofikiria kwamba mwanamke au mwili wa mwanamke ndio wenye jukumu la kuainisha jinsia ya mtoto kwa kuwa yeye ndiye anayebeba mimba, uhakika wa mambo ni kuwa mwanamume ndie mwenye uwezo wa kuainisha jinsia.



 Kila yai la mwanamke lina chromozu mbili za X. Iwapo manii ya mwanamume au spemu (ambayo in chromozomu X na Y) itakuwa na X na kurutubisha yai la mwanamke lenye X tupu, basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanamke.

Vilevile iwapo spemu ya mwanaume itakuwa na Y na kurutubisha yai la mwanamke lenye X, basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanamume. 

Hivyo kwa kufahamu suala hilo, ni matumaini yetu kuwa vile visa vya kinamama kuachwa eti kwa kuwa hawakuzaa watoto wa kiume au wa kike vitapungua katika jamii zetu. Mke wako asipozaa mtoto wa jinsia uitakayo, usifikiri kuwa yeye ndio mwenye makosa.

Wakati mwanamume anapomwaga shahawa, spemu kati ya milioni 200 hadi 400 humwagwa katika uke wa mwanamke. Baadhi ya spemu hizo huwa zina chromozomu X na baadhi zina chromozomu Y. 

Hata hivyo, ni spemu moja tu ambayo hutakiwa kwa ajili ya kurutubisha yai la mwanamke na kuunda mimba.  


Nadharia mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kuchagua ni jinsia gani unaitaka awe nayo mwanao, zinategemea suala la kuandaa mazingira katika uke na mwili wa mwanamume na mwanamke, yatakayosaidia spemu ya baba yenye chromozomu inayotakiwa irutubishe yai la mama, na hivyo kutungwa mimba ya jinsia inayotakiwa.


Njia ya Dr. Shettles ya kuzaa mtoto wa kike
Njia hii imekuwa ikitumiwa na watu wengi kwa miaka mingi sana na imewasaidia kuweza kuzaa mtoto wa kike. 



Wengi wanasema kuwa uwezekano wa kufanikiwa njia hii ni asilimia 90. Njia ya Dr. Shettles inategemea msingi kwamba, chromozomu Y (yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kiume) ni ndogo na yenye kwenda kwa kasi zaidi ikilinganishwa na chromozomu X (yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kike) ambayo ni kubwa na huenda polepole. 

Pia kwa kutegemea kuwa chromozomu X inaishi muda mrefu zaidi kuliko ile ya Y. Hivyo Dr. Shettles anashauri kuwa iwapo unataka kuzaa mtoto wa kike uhakikishe kuwa:
  

Comments

Popular posts from this blog