MAZISHI YA ALIYEKUWA KAIMU KAMANDA WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA KATAVI , KATIKA KATA YA MZUMBE, WILAYA AYA MVOMERO
- Get link
- X
- Other Apps
Baadhi
ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliwa wamebeba jeneza lenye
mwili wa aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Katavi, Mrakibu
msaidizi, Mohamed Madulika, mara
baada ya kifikishwa nyumbani kwake , Kijiji cha Mikongeni, Kata ya
Mzumbe, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro kwa ajili ya utaratibu wa
mazishi , Madulika alifariki dunia kwa ajali ya gari Augoti 5, mwaka huu
,Wilayani Sumbawanga wakati akielekea mkoani Katavi akitokea Jijini Dar
es Salaam na mazishi yake yamefanyika Augost 8, mwaka huu kijijini
hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Faustine Shilongile akiweka udongo kaburini.
Mazishi yakiendelea.
Luteni Kanali , Lidwino Simion Mgumba, Naibu Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Augt 8, mwaka huu akiweka udogo ndani ya kaburi anamozikwa Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Katavi, Mrakibu msaidizi, Mohamed Madulika , eneo ka Kijiji cha Mikongeni , Kata ya Mzumbe , wilayani Mvomero , mkoa wa Morogoro , baada ya kufariki dunia kwa ajali ya gari Augoti 5, mwaka huu ,Wilayani Sumbawanga akielekea mkoani mwake alipokuwa akitokea Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Majeshi mengine , wakitoa saluti ya heshima ya mwisho mara baada ya kukamilika kwa mazishi ya Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa mkoa wa Katavi, Mrakibu msaidizi, Mohamed Madulika, katika makaburi ya Kijiji
cha Mikongeni, Kata ya Mzumbe, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro ,
Madulika alifariki dunia kwa ajali ya gari Augoti 5, mwaka huu ,Wilayani
Sumbawanga wakati akielekea mkoani Katavi akitokea Jijini Dar es Salaam
na kuzikwa Augost 8, mwaka huu Kijiji hapo.
Sehemu ya Waombolezaji wa Msiba huo.Picha na John Nditi.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment