HUWEZI AMINI,HUU NDIO UTAJIRI WA MAJUMBA YA KIFAHARI YA MCHEZAJI MRISHO NGASA ,JIONEE MWENYEWE HAPA


SASA ni miaka nane tangu aanze kucheza soka ya ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Kagera Sugar ya Bukoba, lakini kwa namna alivyopanga vyema karata zake, Mrisho Khalfan Ngasasa anafurahiamaisha ya mpira. 
Huwezi kumuita tajiri, lakini huwezi kuacha kumpa heshima miongoni mwa wachezaji wakizazi chake, kwamba amewaacha mbali. Amecheza klabu nne katika Ligi Kuu tu, baada ya Kagera Sugar ni Yanga SC mwaka 2007 hadi 2010, Azam 2010 hadi 2012,Simba SC 2013 na sasa amerejea Jangwani.





Hakuna maslahi makubwa aliyopata Bukoba, zaidi alikuwa anatafuta njia ya kutokea katika soka ya Tanzania na tangu Yanga SC hadi sasa unaweza kusema Mrisho ametumia kipindi hicho kuchanga vyema karata zake. 
Anamiliki nyumba tano, tatu zipo Mwanza na mbili Dar es Salaam- na ana gari nane, wakati huo huo akaunti yake wakati wote ikiwa ‘imefulia sana’ ina Sh. Milioni 20. Akiwa bado anategemea soka kama ajira yake, Ngassa amekwishaanza kujipanga kwa maisha ya baada ya soka na katika mahojiano na BIN ZUBEIRY

wiki hii anasema anafanya biashara ya usafirishaji na kilimo.




Ngassa akiwa na bibi na babu




Ngassa katika kaburi la shangazi yake



Ngassa na watoto wake


“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara, mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya shughuli za nyumbani wakati wote na mbili nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”.

Ngassa anasema baada ya kustaafu soka atajitanuazaidi kibiashara, kwani ndoto zake ni kutoka kuwamwanasoka nyota hadi mfanyabishara mkubwa.

“Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa sitegemei kurudi shule kusomea chochote, nitafanya biashara. Nimekwishaanza kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”.“Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za kuigana igana sijui kufungua saluni au madukaya nguo. 
Mimi nitafanya biashara kubwa na siku moja nitatatambulika kama mwanasoka wa zamani na mfanyabiashara mkubwa, tayari nina mashamba kama matatu, haponazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni biashara kubwa,”anasema Ngassa.






Nyumba nyingine ya Mwanza







Moja ya gari za kutembelea za Ngassa ikiwa katika nyumba ya Dar es Salaam, Yombo.







Nyumba ya Bwiru ni marumaru tupu







Ngassa akiwa na watoto


Pamoja na kufanikiwa uwanjani na katika maisha katika upande wa kuwekeza, Ngassa hakuwa mvivu pia katika ujenzi wa familia, hadi sasa akiwa na umri wa miaka 25, ana watoto wawili,ambao ni Farida (5) na Farkhiya (3). Ngassa anawajali sana watoto wake na wote anaishi nao mwenyewe, ingawa ametengana na mama yao, kwa sasa akihakikisha wanapata malezi bora,ili wakue vizuri. 
Baada ya kumaliza kuitumikia timu ya soka yataifa ya Tanzania, Stars katika mechi za kuwania kucheza Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), Ngassa ameenda likizo Mwanza tangu Jumatatu naanatarajiwa kuripoti kazini, Yanga SC Jumapili. 
Ngassa alijaribu sana kuibeba Stars akitoa krosi ya bao lililofungwana Amri Kiemba na kukaribia kufunga mara mbili, lakini Tanzania ikalala 3-1 mbele ya Uganda mjini Kampala na kutolewa CHAN. 
Amekubali matokeo na kwenda kusalimu wazazi, ndugu, jamaa na marafiki baada ya mwaka mzima wa kuwa kazini Dar es Salaam. Akiwa huko, Ngassa alitembelea bibi na babu zake, ndugu, jamaa na marafiki hadi vijijini na pia kuzuru kaburi la shangazi yake aliyefariki mwezi mmoja uliopita yeye akiwa ametingwa na majukumu ya kitaifa.





Gari la Ngassa la Mwanza





Gari lingine la Ngassa



Ngassa aliwatemebelea watoto na kuwazawadia mipira ili wacheze soka, akiwahamasisha kujibidiisha na wao watakuwa kama yeye siku moja, kwani hata yeye aliaanzia kama wao.
Mjini Mwanza, Ngassa ni kama mfalme, anapendwa mnokutokana na mfumo wake wa maisha, siku zote ni kijana mwenye nidhamu, adabu na utii- na asiyesahau asili yake. Likizo yake hii ya sasa amekwenda hadi msikitini kufuturu na waumini wenzake wa dini ya Kiislamu na kufanya ibada yasadaka. Anatakiwa dua njema tu na watoto hadi wazee, wake kwa waume na hakuna ajabu akiendelea kuwa mwanaoskanyota Tanzania.
CHANZO : BIN ZUBERY
         
               USISAHAU KU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK NA TUPE MAONI YAKO

Comments

Popular posts from this blog