HII NDIO HISTORIA FUPI YA MAISHA YA ANTI EZEKIEL ALIKO ANZIA MPAKA SASA.ISOME HAPA
- Get link
- X
- Other Apps
JINA
la Aunt Ezekiel siyo geni kwa wadau mbalimbali wa burudani hapa
nchini, ni staa ambaye hivi sasa ana jina kubwa kupitia sanaa yake ya
uigizaji wa filamu aliyoianza miaka sita iliyopita.
Japokuwa kwa sasa ni staa, amepitia mambo mengi magumu katika safari yake ya maisha mpaka kufikia hapo alipo hivi sasa.
Aunt
alizaliwa mwaka 1988 mkoani Dar es Salaam, baba yake akijulikana kama
Ezekiel Grayson’ Jujuman’ ambaye alikuwa ni mchezaji hodari sana wa timu
ya Simba. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Bunge mwaka 1993
hadi 1998. Alienda kumalizia darasa la saba katika Shule ya Msingi
Chanzige iliyopo Kisarawe, mkoani Pwani.
Vipi maisha yalikuwaje baada ya kumaliza shule?
“Kwa
kweli maisha yalikuwa ni magumu mno kwa maana nilipomaliza shule tu,
alijitokeza mwanaume na kutaka kunioa kitu ambacho mimi sikukipenda
kabisa lakini baba yangu alitaka hivyo kwa vile uwezo wa kunisomesha
hakuwa nao tena na maisha yalikuwa ni magumu sana.
“Baada
ya kuona mambo ya mimi kuolewa yanapamba moto huku yule mwanaume
akizidi kuihudumia familia yangu, nikaona nikichelewa nitabebwa
mzobemzobe, hivyo niliamua kutoroka alfajiri na mpaka natoroka, sikuwa
najua naelekea wapi.
“Baada
ya kutoroka, asubuhi ile nilienda mpaka Ukonga, sehemu moja inaitwa
Mazizini, nikagonga nyumba moja ya mtu na kumwambia natafuta kazi za
ndani, bila kuchelewa yule dada aliniambia hata yeye anatafuta msichana,
hivyo nilianza kufanya kazi nikawa namlea mtoto na kufanya kazi zote za
ndani huku nyumbani kwetu wakinitafuta bila mafanikio.
“Baada
ya kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu, niliamua kumpigia simu baba
yangu ambapo aliposikia sauti yangu alifurahi sana na kuniambia kuwa
nirudi nyumbani wala hawataweza kuniozesha tena, hivyo niliamua kumuaga
tajiri wangu na kumwambia narudi nyumbani kwetu.
“Niliporudi
nyumbani bado nilimkuta yule mchumba lakini nilimwambia kama anataka
kunioa anisubiri nisome, hivyo nilienda Iringa katika Shule ya Sekondari
Kawawa na kuanza kidato cha kwanza mpaka cha pili, nikarudi Dar na
kumalizia katika Shule ya Sekondari Makongo mwaka 2004.
“Baada
ya kumaliza sekondari, nilijiunga na mambo ya computer pale Amana,
lakini baadaye niliamua kushiriki mambo ya urembo ambapo niliibuka kuwa
Miss Mwanza 2006 na kuingia katika shindano la kumsaka mrembo wa
Tanzania lakini sikufanya vizuri na hapo ndipo nilipoingia kwenye
uigizaji wa filamu ambapo filamu yangu ya kwanza kabisa ilikuwa ni Miss
Bongo, iliyokuwa ya William Mtitu.
“Ilipofika
mwaka 2007 nilifunga ndoa ya bomani na mfanyabiashara maarufu Jack
Pemba. Yule mchumba aliyekuwa akinisubiri mwanzo alikuwa ameshakata
tamaa na kuendelea na maisha yake, hivyo nilianza kuishi na Jack kama
mke na mume huku akinisaidia katika mambo yangu ya sanaa.
“Baadaye
alinizuia kwani alikuwa hapendi nitoke nyumbani na baada ya muda
nilipata ujauzito wake kitu ambacho kilimfurahisha sana na kunizawadia
vito vya dhahabu vyenye uzito wa kilo moja, lakini kwa bahati mbaya
ilipofika miezi saba nilijifungua mtoto akafariki.
“Ndoa
ilikuwa ni nzuri, nilikuwa napata kila kitu ambacho nataka na
kutembelea gari za kifahari lakini kitu ambacho nilikishindwa ndani ya
ndoa hiyo ni kipigo kikali nilichokuwa nakipata, kwani nakumbuka kuna
siku alinipiga kiasi ambacho mashuka meupe yalikuwa kama yamepakwa rangi
nyekundu, hivyo bibi yangu alikuja kunichukua na kuondoka moja kwa
moja.
“Baada
ya kuondoka kwa Jack, nilianza kupigana katika maisha na niliingia
kwenye uhusiano na mtu mwingine na nikaanza kuingia kwenye kucheza
filamu ambapo huko jina langu lilizidi kukua siku hadi siku, hivyo
nikawa naweza kuyaendesha maisha yangu ya kila siku, mpaka nilipokutana
na mume wangu wa sasa, Sunday Demonte ambaye alinioa mwishoni mwa mwaka
jana.
“Unajua
kazi yangu kubwa mimi ni uigizaji ambapo huku Tanzania ndiyo kila
kitu, sasa nikisema nikae Dubai muda wote ni lazima kipaji changu
kitapotea, hivyo nafanya kazi zangu kwa kutengeneza filamu kama tatu,
kisha narudi Dubai kidogo kukaa na mume wangu.
“Siku
zote naumia sana kuwapoteza wazazi wangu wawili, yaani baba na mama,
nilitamani sana mpaka leo wawepo na waione kazi yangu na nilifurahi sana
siku ambayo nilifunga ndoa yangu ya pili na Sunday Demonte,” anaeleza
Aunt.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment