DUDU BAYA ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUCHOMA MOTO NYUMBA YA MSANII MWENZAKE


MSANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ ameswekwa rumande kwa kudaiwa kuchoma nyumba ya baba wa msanii mwenzake ‘Geez Mabovu’, Mashaka Mrisho.

Tukio hilo lilitokea Agosti 1, mwaka huu ambapo mwenye nyumba sambamba na polisi walimkamata Dudu Baya na mkewe Mariam kwa madai ya kuchoma moto nyumba kwa makusudi na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
 

“Mkewe alitupia mkaa wa moto katika sofa, likashika moto kabla majirani hawajanisaidia kuuzima. Baada ya kuwauliza kulikoni wakanitishia maisha ndipo nikawapeleka polisi na kupewa RB namba OB/RB/13485/2013 na kuja kumkamata,” alisema Mashaka.
 

Dudu Baya alipotafutwa na mwandishi wetu, alikiri kukamatwa na kuwekwa sero kwa saa sita kabla ya kuwekewa dhamana na shemeji yake aliyemtaja kwa jina la Vero.


“Vyumba vyake na vyangu haviingiliani kabisa, tumetenganishwa na ukuta hivyo shutuma zake hazina ukweli dhidi yetu ila naamini uchunguzi wa polisi ndiyo utatoa majibu,” alisema Dudu baya.
 ........................................ TUPE MAONI YAKO .....................................

Comments

Popular posts from this blog