KASI YA MAAMBUKIZI YA VVU/UKIMWI YAPUNGUA HALMASHAURI YA MOSHI
- Get link
- X
- Other Apps
Kasi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi imepungua katika Halmashauri ya Moshi baada ya kuanzisha kampeni za kuhamasisha jamii kupima afya zao kwa hiari kwa kutumia vikundi mbalimbali vya sanaa za maonyesho .
Mratibu wa UKIMWI wa Halmashauri ya Moshi Benedicto Rwamuruku amesema ,kampeni hiyo wamaeanzisha baada ya kuona mafanikio ya elimu iliyotolewa awali kwa njia ya sinema imewafikia jamii na maambukizi yamepungua.
Aidha ameongeza kuwa maambukizi hayo yamepugua kutoka wastani wa asilimia 1,6 hadi kufikia asilimia 1.3 miaka mitaano iliyopita na lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi hayaogzeki kwani Tanzania bila ukimwi inawezekana.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment