IRINE CHEPTAI WA KENYA AANGUKA NA KUZIMIA BAADA YA KUMALIZA MBIO ZA MITA 3,000
- Get link
- X
- Other Apps
Daktari wa kwanza kabisa kumkimbilia Irine Cheptai akihaha kuuzindua moyo wake baada ya kuzimia, alipokuwa akimaliza mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini London jana.
Jopo la Madaktari wakihangaika kumpatia huduma ya kwanza Irine Cheptai, alianguka na kuzimia wakati akimaliza mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki.
Cheptai (wa pili kulia) akikimbia mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini London.
LONDON, England
Cheptai, binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11, katika muda bora zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa kumalizia
MKIMBIAJI wa mbio ndefu wa kimataifa wa Kenya, Irine Chebet Cheptai jana alikimbizwa hospitali kwa matibabu baada ya kupatwa na mshituko wa moyo kwenye Uwanja wa Olimpiki baada ya kumaliza mbio za mita 3,000.
Cheptai, binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11, katika muda bora zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa kumalizia.
Madaktari waliokuwa uwanjani hapo wakaharakisha kumtundikia mtungi wa Oksijeni, ambapo kwa mujibu wa taarifa kuhusiana na tukio hilo zilipasha kuwa alikuja kurejewa na fahamu akiwa hospitalini.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment