"NDOTO ZANGU NI KUOLEWA NA MSANII AY"....SALAMA JABIR
Mtangazaji mahili wa show za TV/Radio aliyeisimamisha wima show mpya na kali inayorushwa kupitia channel 5 ‘Mkasi’
namzungumzia Salama Jabir ametupia ‘neno’ kupitia kipindi hicho kuwa huenda siku
moja akaolewa na AY!
Kama uliiangalia show ya Mkasi jumatatu ama marudio yake leo
(jumamosi) ambapo crew nzima ya kipindi cha mkasi chini ya C.E.O na Producer wa
show Ambwene Yesaya ‘AY’ walikuwa wakieleza changamoto na mambo mbalimbali
waliyokutana nayo wakati wanaanza kufanya kipindi hicho, mwishoni Salama ambae
alikuwa akimuelezea AY kuwa ni msanii ambae anajivunia kufanya nae kazi
kutokana na jinsi alivyomchapakazi na mtu wa kuaminika alimaliza kwa kusema “huenda
ipo siku moja tutaona..!”.
Wote tunajua Salama alivyo mtu wa utani sana, kitu kinachoongeza
burudani ya ziada katika show zake, alitamka hivyo na kumgeukia AY akimuuliza,
na AY mwenyewe akajikuta anacheka na kukubali.
Pengine ulikuwa ni utani tu, lakini hakuna aijuae kesho ukizingatia wote wako single!
Comments
Post a Comment