HOSPITAL YASHTUMIWA KUSABABISHA KIFO CHA MSANII WA BONGO MOVIEZ JOHN S. MAGANGA

Msanii wa bongo moviez john s masanga amefariki dunia jana saa 4 usiku katika hospital ya mwananyamala kwa kile kilichosemakana kwamba alikuwa ameanguka ghafla katika semina aliyokuwepo kwa ajili ya mambo ya filamu.

Akiwa na kina natasha,mama yake monalisa na shija katika hali isiyokuwa ya kawaida ameanguka gafla,na kukimbizwa katika hospital ya mwananyamala hapo ndipo alipopimwa na kuambiwa kuwa alikua na vidonda vya tumbo  na kufanyiwa oparation, baada ya madaktar hao kuona kuwa hali yake imezidi kuwa mbaya wakamwamishia hospital ya muhimbili na huko ndipo alipoendelea kupata matibabu zaid, lakin hali yake ilizid kuwa mbaya na kugundulika kuwa alikuwa na ugonjwa mwengine tofauti na aliokutwa nao hospital ya mwananyamala.

 

Muhimbili waligundua kuwa alikuwa na ugonjwa wa kujaa maji katika mapafu. ambapo muda wa kutibia ugonjwa huo ulikuwa umeshakwisha mpaka kupelekea kifo chake. marehemu john s maganga ameacha pengo kubwakatika tasnia ya filamu tanzania,marehemu alishaigiza filamu nyingi kama;-mrembo kikojozi,chanzo ni mama, my dreams,cake ya birthday,bar maid,pretty gal. na nyingine

Comments

Popular posts from this blog