Posts

ZIFAHAMU FAIDA KUMI ZA MMEA WA ALOE VERA KWA BINADAMU...

Image
                                                                  mmea wa aloe vera ni mmoja ya mimea ambayo imejizoelea umaarufu miaka hii ya karibuni  baada ya kuonyesha kutibu na kuzuia aina mbalimbali za magonjwa, lakini pia kurefusha maisha na kupunguza makali ya magonjwa yasiyopona kama kisukari, presha, magonjwa ya moyo, pumu, kifafa, ukimwi na mengine mengi, lakini mmea huu ulikua ukitumika tangu miaka ya zamani sana na watu waliishi miaka mingi wakiwa na nguvu na akili kupitia mmea huu. kwa faida za mmea huu ni bora kumiliki hata bidhaa moja tu ambayo utakua unaitumia siku zote za maisha yako ili kupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa hatarishi..kwa sasa kampuni ya forever living product ndio inaongoza kwa mauzo hayo duniani, ikiwa imetapakaa zaidi ya nchi 150.hapa tanzania ikiwa  imeuaza zaidi ya bilioni ishirini kwa mwaka jana tu  na kulipa kodi serikali zaidi ya bilioni tano za kitanzania, hii inaonyesha watanzania wameamka na wanatumia sana bidhaa

Mwanamuziki Lady Jaydee Azungumzia Msanii wa Kiume Anaemfikiria Sasa Kushirikiana Naye

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Ndi ndi ndi' amefunguka na kuweka wazi wazi msanii wa kiume ambaye kwa sasa anamfikiria katika kufanya nae kazi. Kupitia Accout yake ya twitter ambapo alitoa nafasi ya maswali kutoka kwa mashabiki zake Lady Jaydee aliulizwa swali kama ataweza kufanya remix ya wimbo wake mpya na kama atafanya hivyo anadhani ni msanii gani wa kiume ambaye ataweza kufanya nae kazi hiyo. Ndipo hapo aliposema kwa sasa anamfikiri sana Mr Blue. "Kiukweli mtu niliemfikiria hapo ni Mr Blue, naona ndio ata fit vizuri zaidi, Msanii wa Tanzania alieko akilini kwangu hivi sasa ni Mr Blue" alisisitiza Lady Jaydee Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi sababu za ukimya wake kwenye muziki kabla ya kuja na wimbo huo mpya na kusema kuwa huo ndio utaratibu wake toka amenza muziki na toka anatoka na Album ya kwanza mwaka 2001 yeye si mtu ambaye anatoka ngoma mara kwa mara bali huwa

Shamsa: Nusura niharibike ubongo kwa kipigo

Image
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford. Stori: Imelda Mtema Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa amekutana na kipigo cha mara kwa mara kipindi anaishi na baba mtoto wake Dickson Matok ‘Dick’ kiasi ambacho alikuwa akikaribia kupata athari kwenye ubongo. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa amenusurika kumpoteza mtoto wake akiwa tumboni kutokana na mitama aliyokuwa akipigwa na mpenzi wake huyo lakini kwa sababu alikuwa anampenda alikuwa habanduki. “Jamani napinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake wenzangu kwani ilibaki kidogo niharibike ubongo kwa kipigo cha mwanaume huku nikiamini napendwa kumbe ni ujinga mtupu,” alisema Shamsa

Fina Mango na Masoud Kipanya waongezeka katika timu ya Power Breakfast ya Clouds Fm

Image
Siku kadhaa zilizopita katika mitandao ya kijamii zilisambaa habari za kuwa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm, Gerrard Hando na Paul James (PJ) wameondoka katika redio hiyo. Katika kipindi hicho cha Power Breakfast leo Ijumaa, Aprili 1 zimesikika sauti mpya katika kipindi hicho ambapo ni Fina Mango na Masoud Kipanya ambao wamesikika katika kipengele cha kuperuzi na kudadisi ambacho kinahusika na kupitia magazeti ya siku husika. Baada ya kuongezeka kwa watangazaji hao, inaonyesha dhahiri kuwa Gerrard Hando na PJ watakuwa wameondoka katika kituo hicho baada ya kudumu kwa kipindi kirefu ambapo mikataba yao ilimalizika jana Machi, 31.

MAKONDA AWAGEUKIA BODABODA WA DSM.AWAAHIDI PIKPIK KWA SH.3,500 KWA SIKU,KUINGIA POSTA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama Bodaboda mkoani humo na kuwapa ahadi nono za kuwainua kimaisha kupitia biashara hiyo. Pamoja na mambo mengine, Makonda ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya shilingi 25,000 kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia wazimiliki wao. Mwendesha bodaboda akiwa amepakia abiria watatu kwenye chombo hicho cha usafiri, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, kama walivyokutwa eneo la Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam juzi. Picha na Joseph Zablon (Maktaba) Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuwatengenezea mpango mzuri wa utakaowawezesha bodaboda hao kuingia katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa. Ahadi ya Makonda kuwaruhusu Bodaboda kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana. Juzi, Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia

SAKATA LA WASTARA MAPYA YAIBUKA,MBUNGE ASEMA AMELOGWA NA WASTARA,AJIBU MAPIGO,AELEZA MAZITO

Image
  Makubwa! Aliyekuwa mume wa nyota wa Filamu za Bongo, Wastara Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Zanzibar, Sadifa Juma ameibua jambo zito miongoni mwa jamii akidai kuwa, mtalaka wake, Wastara Juma amekuwa akimroga, twende na Risasi Jumamosi. Madai hayo aliyatoa Alhamisi iliyopita baada ya gazeti hili kumuuliza habari zilizoenea kwamba, amemuangukia Wastara akitaka warudiane kwani yaliyopita si ndwele. Sadifa alisema kuwa, aligundua hilo la kurogwa baada ya Wastara kuondoka nyumbani kwake na kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa, amepewa talaka mbili. Akizungumza kwa dakika 25, Sadifa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Ukimwangalia Wastara harakaharaka unaweza kusema ni mwema sana lakini hana wema wowote. Hivi Wastara ni wa kuniroga mimi kweli?” ILIKUWA HIVI Risasi Jumamosi: (baada ya kujitambulisha na salamu) “mheshimiwa tunataka kujua nini kinaendelea kati yako na mkeo Wastara?” Mume: “Kuhusu nini?” Risasi Jumamosi: “Kuna madai kwamba, umea

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA GEREZA LA BANGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATUMISHI WA WIZARA MKOANI KIGOMA

Image
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akiongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo(kushoto) na Mkuu wa Gereza la Bangwe,SSP Raphael Mwanyingile(kulia), alipofika kutembelea gereza hilo katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma tarehe 31/3/2016. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisaini kitabu cha wageni katika Gereza la Bangwe mkoani Kigoma, ambapo baadae alisikiliza risala iliyohusu  mambo mbalimbali,  iliyoandaliwa na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo na kuahidi kushughulika changamoto zao. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo, akisoma taarifa ya hali ya magereza mkoani Kigoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Mmoja wa Askari Magereza mkoa wa Kigoma, akizungumza wakati wa kipindi cha maswali kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch

Tuhuma za Rushwa: Mbunge Ndassa Naye Afikishwa Kortini

Image
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa. MBUNGE wa Sumve, Richard Ndassa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar, leo akituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi  milioni 30  akiwa kwenye Kamati za Bunge. Ndasaa  anakuwa  mbunge  wa  nne  wa  CCM kupandishwa  mahakamani  kwa  tuhuma  za  rushwa  baada  jana wabunge Mh.Kangi Lugola wa jimbo la Mwibala, Mh.Sadiq Murad wa jimbo la Mvomero na Mh.Victor Mwambalaswa wa jimbo la Lupa kupandishwa  mahakamani kwa tuhuma za kuomba rushwa ya milioni 30 toka kwa mkurugenzi wa Wilaya ya Gairo  ili taarifa yake ipitishwe bila kujadiliwa.

SERIKALI KUPITIA UPYA MIKATABA YA TRL

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza mmoja wa abiria anayetumia usafiri wa reli ya kati mkoani Kigoma. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Saveli Maketta. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mkoani Kigoma. Muonekano wa mabehewa ya treni yakiwa mwisho wa reli ya kati, mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kapteni wa Meli ya MV Liemba ya namna inavyoendeshwa, mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akipata ufafanuzi wa namna ya injini za Meli ya MV Liemba zinavyofanya kazi wakati alipotembelea Meli hiyo mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye kizibao cha njano), akimsikiliza Kapt

Wifi wa Zari adaiwa kutimuliwa kwa Diamond

Image
Wifi nambari moja wa Zarinah Hassan ‘Zari’, Esma Platnumz. Stori:  Musa Mateja,  Ijumaa Hivi karibuni yalitua madai kwenye meza ya gazeti hili yakieleza kuwa, eti yule wifi nambari moja wa Zarinah Hassan ‘Zari’ anayefahamika kwa jina la Esma Platnumz (pichani) ametimuliwa pale nyumbani kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Madale jijini Dar na sasa anaishi Tandale. Chanzo chetu ambacho kiliomba jina lake lisiandikwe gazetini kilidai kuwa, baada ya Zari kutua Bongo kabla ya kwenda Ulaya, Esma alitakiwa kufungasha kila kilicho chake na kwenda kuishi kwenye ile nyumba ya familia iliyokuwa ikikarabatiwa pale Tandale. Diamond akiwa na waubani wake, Zari. “Nyie mbona mnapitwa na ubuyu? Esma katimuliwa pale kwa Diamond, sasa hivi anaishi kule Tandale kisa ni zile figisufigisu zilizokuwa zikitokea kati yake na Zari. “Diamond ameona ili mzazi mwenzake awe na amani, anayeweza kuondolewa kwenye ule mjengo aondolewe ili amani itawale na kusiwepo manenomaneno,” kilidai chanzo

Rais Zuma apewa siku 105 kurejesha fedha za umma alizotumia kukarabati makazi yake

Image
Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika ya Kusini imemuamuru Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ndani ya siku105 awe amerejesha serikalini dola milioni 16 fedha za walipakodi ambazo alizitumia kukarabati makazi yake binafsi. Mahakama hiyo imesema Rais Zuma mwenye umri wa miaka 73 alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kumtaka alipe fedha hizo zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi. Jopo la Majaji 11 wa Mahakama hiyo ya Kikatiba ya nchini Afrika ya Kusini limesema Rais Zuma alikiuka Katiba ya nchi hiyo kwa kutumia fedha hizo katika ukarabati wa nyumba yake hiyo ambayo ipo eneo la nkandla -kwazulu-natal na kuhitimisha miaka 6 ya sakata hilo. Chama cha siasa cha Democratic Alliance cha nchini humo  kimeanzisha kampeni ya kumuondoa Rais zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka Katiba. Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimisha Rais Zuma kuzingatia mat

MCHUNGAJI APOTEZA WATOTO WANNE KATIKA AJALI YEYE NA MKEWE WASALIMIKA

Image
Kama kuna jambo limefichwa usoni pa wanadamu ni Kifo, tungelijua sijui tungekuwa na aina gani ya Maisha... Labda tusingesoma, labda tusingejenga nyumba, labda tusingeoa na kuolewa, labda tusingezaa watoto na yamkini tusingenunua magari wala kusafiri kwa kutumia magari hayo...inabaki kuwa fumbo! Jana imekuwa siku ngumu na mbaya ambayo itabaki kuwa kovu kwa maisha yote kwa mchungaji Pastory Michael Kajembe ambaye ni mchungaji wa TAG-Ebenezer (Dodoma) Mwanataaluma mahiri wa Theolojia, na Mwalimu wa Chuo cha Biblia Dodoma (Central Bible College, zamani AGBC) na familia yake,Kanisa la TAG kwa ujumla, ndugu jamaa na marafiki... Baada ya kupata Ajali ya Gari akiwa na familia yake, jana alfajiri katikati ya Mtera na Mpunguzi, Mkoani Dodoma na Kupoteza Watoto wake Wanne kwa pamoja Junior, Isaac, Gabriel na Glady katika ajali hiyo. Mchungaji Pastory Kajembe na Mama, Bwana amewaponya,bado wanahitaji maombi maana nao wamepatwa na Majeraha na wanaendelea na matibabu. B

Breaking News!! LEMBELI APIGWA CHINI KESI YA UBUNGE KAHAMA

Image
Habari tulizozipata hivi punde kutoka Kahama mkoani Shinyanga ni kwamba aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kahama James Lembeli(Chadema) ameshindwa katika kesi ya Ubunge jimbo la Kahama iliyokuwa inaendelea mahakamani. Lembeli alikuwa amefungua kesi kupinga ushindi wa Jumanne Kishimba ambaye sasa ni mbunge wa jimbo la Kahama kwa tiketi ya CCM. ...Taarifa kamili tutawaletea hivi punde...

WATANZANIA KUNUFAIKA NA BIMA YA ELIMU KUTOKA SANLAM LIFE INSURANCE TANZANIA

Image
Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo.Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe na kulia ni Mchambuzi wa Mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando.  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Elimu ya 'Sanlam Education Care,Kulia ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (wapili kushoto), akimkabidhi Hati ya Bima ya Elimu wa 'Sanlam Education Care', Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando na kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood. Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa bima za maisha TanzaniaSanlam Life Insurance, leo, imezindua bima ya elimu ya kipekee inayolenga

ZARI THE BIG BOSS NA DIAMOND PLATINUMS KIMENUKA ULAYA,MAZITO YAIBUKA.

Image
Hakuna furaha isiyo na karaha! Ndiyo kauli inayoweza kutumika kwenye habari ya ziara ya Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Familia ya Wasafi Classic Baby (WCB) huko barani Ulaya ambapo staa huyo na mama mtoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wanadaiwa kukinukisha, kisa kikidaiwa ni wivu wa mapenzi, Amani limenyetishwa. NI MUDA MFUPI BAADA YA KUTUA SWEDEN Habari kutoka kwa chanzo chetu makini ambacho ni mmoja wa watu waliopo kwenye msafara wa ziara hiyo iliyopewa jina la From Tandale to the World, zilidai kuwa, mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari na Diamond walitibuana muda mfupi baada ya kutua katika Jiji la Stockholm nchini Sweden kwa ajili ya shoo. Kilidai kwamba, Diamond alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na warembo wakimtaka kimapenzi huku Zari akishuhudia. CHANZO CHATIRIRIKA “Huku kuna ishu ambayo ni nyeti sana maana kilichomkuta Diamond kwa Zari walipofika hotelini kama isingekuwa sisi kuokoa jahazi basi hata shoo zingeharibika ma

BREAKING NEWZ:Takukuru Imewapandisha Kortini Wabunge Hawa Leo kwa Rushwa.

Image
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa Lupa Mh. Victor Mwambalaswa . Wakijadiliana jambo Dar es Salaam Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), leo imewaburuza kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar, wabunge wa 3 wa Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotuhumiwa kwa rushwa. Wabunge hao ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa Mh.Victor Mwambalaswa. Taarifa zaidi za tukio hilo zitawajia kadri tutakavyozipata.

Waziri wa Rwanda Afia Gerezani Burundi

Image
Bujumbura, Burundi WAZIRI wa zamani wa Rwanda, Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi. Rwanda imesema marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria. Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji ameandika na kusema kifo cha Jacques ni “mauaji”. Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua. Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.

Ruge akanusha Gerald Hando na PJ kuacha kazi!

Image
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba. MKURUGENZI wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba,  leo kupitia kipindi cha Power Breakfast‬ amekanusha uvumi wa watangazaji wa kituo hicho, Gerald Hando, Abel Onesmo na PJ,  kuacha kazi. “Kwa nafasi yangu kama mkurugenzi,  taarifa nilizonazo ni kwamba tuna mikataba na wafanyakazi hao ambayo inaisha leo tarehe 31.  Sehemu kubwa ya wafanyakazi  wetu mikataba yao inaisha mwezi huu, hivyo  katika hali ya kawaida huwa tunatoa nafasi ya kumwambia anayetaka kuendelea na mkataba aandike barua au aseme,” alisisitiza Mutahaba

MWANZA NA ARUSHA YAONGOZA WATUMISHI HEWA.

Image
  Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi majina hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik  akikabidhi majina hewa kwa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene  baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa , jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam. Wakuu wa Mik