Posts

Showing posts from August 26, 2013

WEMA SEPETU ADAIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

Image
Skendo ya mastaa mbalimbali Bongo kutajwa katika biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya ambapo tayari majina ya wasanii wawili wakubwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ yametajwa huku kinachowaponza kikijulikana. Habari zinadai kuwa mastaa hao wameanza kujutia tambo zao za kutangaza utajiri walionao hivyo kuibua maswali kuwa huenda wana uhusiano na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ikiaminika ndiyo njia ya haraka ya utajiri. WEMA Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema kutangaza kununua nyumba, magari ya kifahari na kutapanya fedha ndiko kulikomponza na sasa anatajwa na wengi vinywani mwao juu ya kuhusika katika biashara hiyo haramu. Kuna madai kuwa bosi huyo wa Endless Fame Productions amehojiwa juu ya suala hilo lakini meneja wake, Martin Kadinda alikanusha uvumi huo. DIAMOND Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni u

Ofisa usalama Kigoma alindwa..

Image
JESHI la Polisi na Idara ya Madini, mkoani Kigoma, limemnasua kiaina ofisa usalama wa uwanja wa ndege, Cleophace Lukindo, aliyedakwa na maofisa wenzake akivusha madini ya dhahabu bila kuwa na vibali. P.T Tukio hilo lilitokea Agosti 22 uwanjani hapo wakati Lukindo akitaka kupita bila kukaguliwa tayari kwa ajili ya kusafirisha madini hayo kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania kuelekea jijini Dar es Salaam ndipo wenzake wakamtilia mashaka na kumkamata. Madini hayo yalikuwa na uzito wa kilogramu tisa huku thamani yake ikielezwa kuwa takriban sh milioni 400. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, tukio hilo limekuwa likifichwa na uongozi wa uwanja pamoja na jeshi la polisi mkoani humo kwa kile kinachodaiwa kuwa ofisa huyo amekuwa akitoa vitisho kwa wafanyakazi wenzake. Katika hatua ya kushangaza gazeti hili jana lilidokezwa kuwa madini hayo yamekabidhiwa na idara ya madini kwa raia mmoja wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) baad

Ofisi ya Pinda yatumika kutapeli

Image
MTANDAO wa watu wasiofahamika umetumia Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuandaa semina hewa kwa madiwani na wataalamu mbalimbali kutoka katika halmashauri za wilaya 16 nchini. Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Bagamoyo juzi, baadhi ya madiwani na wataalamu waliotapeliwa walisema kuwa walipokea barua za mwaliko zikionyesha jina la ofisi hiyo zikiwataka wahudhurie semina ya siku nne kuhusu miradi ya maji katika miji midogo kuanzia Agosti 20-23, mwaka huu. Barua hiyo yenye Kumb. Na PMO/RG/LG/TR/344 ya Agosti 12, mwaka huu, inaonyesha kusainiwa kwa niaba ya Katibu Mkuu Tamisemi na J. Sagini ikieleza kuwa ofisi hiyo kwa kushirikiana na nchi za Falme za Kiarabu iliandaa semina hiyo kwa ajili ya kutatua tatizo la maji. Barua hiyo ilitumwa kwa wakurugenzi watendaji wa halmashauri za Biharamulo, Bunda, Bukombe, Maswa, Nkasi, Iramba, Karatu, Mufindi, Masasi, Muleba, Kibondo,

‘Nyufa’ zajitokeza Bunge la Afrika Mashariki;

Image
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), wameingia katika mpasuko, kutokana na baadhi ya wabunge hao kupinga kutumia ukumbi wa kisasa wa Bunge hilo uliopo Arusha kwa vikao vyote, na badala yake baadhi wanataka kuendelea na utaratibu wa kufanya vikao vya Bunge katika kila nchi wanachama. Habari za uhakika toka ndani ya Wabunge wa Afrika ya Mashariki, walioanza kikao cha Bunge la jumuiya hiyo juzi jijini hapa, zimebainisha kuwa, licha ya Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo, kufikia uamuzi ya vikao vyote sasa kufanyika Arusha, lakini bado kuna wabunge wanapinga. Kikao cha kamati ya uongozi kilichoongozwa na mwenyekiti wake ni Spika wa Bunge hilo, Dk Magreth Zziwa, kiliamua baada ya kukamilika jengo la Bunge, likiwa na ofisi kwa kila mbunge sasa vikao vyote vifanyike Arusha ili pia kupunguza gharama. Awali Bunge hilo, katika vikao vyake vya Arusha, vilikuwa vikifanyika katika Jengo la Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC) kwa kukodi. Katika hatua

SIMBA WAFANIKIWA KUPATA ITC ZA TAMBWE, KAZE

Image
MWENYEKITI wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, leo mchana amefanikisha upatikanaji wa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC), kwa wachezaji wawili wa klabu hiyo kutoka nchini Burundi -Amissi Tambwe na Gilbert Kaze. Wachezaji hao wawili ambao pia ni tegemeo la timu ya soka ya taifa ya Burundi (Intamba Murugamba), hawakucheza katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania iliyochezwa jana kutokana na kutokamlika kwa uhamisho huo, jambo lililoleta usumbufu mkubwa kwa benchi la ufundi, wachezaji wenyewe, uongozi na wapenzi na washabiki wa klabu. Rage aliondoka jijini Dar es Salaam jana usiku na imechukua chini ya saa 24 kuweka kufanikisha suala hilo. Katika taarifa yake kwa wana Simba, Mbunge huyo wa Tabora Mjini alisema amelazimika kuingilia kati suala hilo kwa sababu lilihusu baadhi ya taratibu muhimu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na ukweli kwamba viongozi wa Vitalo, klabu waliyotoka wachezaji hao hawakuwa mjni na hivyo kuchelewa kwao kungeigharimu Simba. &

MOURINHO: MAN UNITED INABIDI WAIGE MFANO WA SERIE A KWA KUTUZUIA ROONEY

Image
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameiambia klabu ya Manchester United ikubali kumuuza Wayne Rooney kwa klabu yake ya Chelsea. (HM) Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mourinho alitoa mfano namna timu pinzani za Italia zinavyofanya biashara ya kuuziana wachezaji na akaishangaa Man United kukataa kumuuza Rooney kwa wapinzani wao na kuita ni mambo ya kizamani: "Hayo ni mambo ya kizamani ya kukataa kuuza mchezaji wako kwa timu ambayo mnacheza nayo ligi moja - hilo halisadii soko na pia wachezaji husika. "Unaona nchini Italia, inavyotoke kila msimu bila matatizo yoyote. Mchezaji anaweza kutaka kuhama kutoka Milan kwenda Inter, kutoka inter kwenda Milan, kutoka Roma kwenda Juventus, kutoka Juventus kwenda Inter, na wanafanya hivi siku zote. "Umeona Inzaghi, alicheza Juventus, Milan, Inter. Nadhani ni [Francesco] Totti pekee ambaye amekaa kwenye klabuy moja maisha yake yote. [Andrea] Pirlo – amecheza Inter, Milan, Juventus

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA VIONGOZI SASA KUPEKULIWA KAMA ABIRIA WENGINE UWANJA WA NDEGE...

Image
KULIA: Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam. KUSHOTO: Dk Harrison Mwakyembe. Kuanzia sasa viongozi wote serikalini watakaopita kwenye viwanja vya ndege nchini, watakuwa wakikaguliwa kama abiria wengine, isipokuwa Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge. Waziri  wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema ipo tabia ya  viongozi  wenye madaraka, kukiuka utaratibu na kupita   katika  viwanja vya ndege  bila kukaguliwa. Alisema kutokana na hali hiyo, amewaambia watumishi  wanaofanya kazi katika viwanja hivyo, hususan Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) viongozi wasiokaguliwa ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge. Alitoa msimamo huo wiki iliyopita  kupitia kipindi cha Jenerali on Monday, kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten. Alisema viongozi wengine wote, wakiwamo mabalozi na mawaziri lazima wakaguliwe

ANGALIA PICHA YA KITU KILICHOTISHIA USALAMA WA KANISA KIJITONYAMA HIKI HAPA

Image
Kinachoninginia kwa hiyo transfoma inasadikiwa ni bomu.. Hofu kubwa imewapata waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Kijitonyama, baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kurushwa kanisa hapo. Polisi wafika kanisa hapo na kuondoka na kitu hicho.

NICK MBISHI ATANGAZA RASIMI KUWA YEYE NI MUATHIRIKA WA UKIMWI

Image
Tumekuwa  tukishuhudiwa  vituko  mbalimbali  vya  wasanii wetu  ambao  wamekuwa  wakihangaika  usiku  na  mchana  kuusaka  umaarufu.... Wapo  ambao  wamekuwa  wakivua  nguo  zao  jukwaani, wapo  ambao  wamekuwa  wakipiga  picha  za  uchi  na  kuzitupia  mitandaoni.Yote  hiyo  ni  kutafuta  Jina  au  umaarufu ambao  mimi  binafsi  nauita  ni  umaarufu  wa  kishamba..... Leo  Nick  Mbishi  ametoa  kituko  ambacho  kimenifanya  niamini  kuwa  wasanii  wetu  wana njia  mpya  kwa  sasa  za  kutaka kujulikana ( kuwa  maarufu). Katika  account  yake  ya  Twitter, N ick  Mbishi  alitoa  post  moja  ikielezea  kuwa  yeye  ni  muathirika  wa  ukimwi. Post  hiyo  ilikuwa  na  taswira  mbili  za mafumbo . Fumbo  la  kwanza  linamaanisha  kuwa  Yeye  NI  mwathirika  wa  UKIMWI  huku  fumbo  la  pili  likimaanisha  kinyume  chacke. Baada  ya  post  hiyo, mijadala  kadhaa  ya  watu iliibuka  kwenye  mitanado  ya  jamii.Wapo waliompa  pole  na  wapo  waliompongeza  kwa 

DILLISH TOKA NAMIBIA AIBUKA MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA 2013

Image
  Fainali za Big Brother zimefikia  tamati  usiku  huu  zikiwa  na  washiriki  watano  ambao  ni  Beverly, Melvin, Cleo, Elikem  na  Dillish. Mshiriki  wa  kwanza  kutolewa  alikuwa  ni  Beverly  akifuatiwa  na  Melvin  huku  Elikem  akiwa  ni  mshiriki  wa  tatu  kutolewa.. Mchujo  huo  uliwafanya  Cleo  na  Dillish  waingie  katika  masaa  ya  fainali za  mwisho  ambapo  Cleo  alielemewa  na  kutolewa  huku  akimwacha  Dillish  akichekelea  $300,000  za  ushindi  wa  shindano  hilo.... Agalia  jinsi  kura  zilivyopigwa:   Angola : Dillish Botswana : Cleo Ghana : Elikem Kenya : Dillish Ethiopia : Beverly Malawi : Cleo Namibia : Dillish Nigeria : Melvin South Africa : Cleo Sierra Leone : Elikem Tanzania : Dillish Uganda : Dillish Zambia : Cleo Zimbabwe : Elikem Rest of Africa : Melvin Total :  Dillish = 5, Cleo = 4, Elikem = 3, Melvin = 2, Beverly = 1.   Hongera sana Dillish

HATIMAYE "FOOLISH AGE" YA LULU MICHAEL YARUHUSIWA BAADA YA KUZUIWA

Image
  Bodi  ya   ukaguzi  wa  filamu  Tanzania  imeridhia  na  kuiruhusu  filamu  ya  Foolish Age  ya  Lulu  Michael  iingie  sokoni  baada  ya  kuizuia  hapo  ijumaa.... Filam  hiyo  ilizuiliwa   kutokana  na  mavazi  ya  nusu  uchi  yaliyokuwa  yamevaliwa  na  washiriki  wake  na  kumtaka  Lulu  Michael  aifanyie  marekebisho  kwa  kuviondoa  vipande  hivyo  ambavyo  vilikuwa  kinyume  na  maadili  ya  kitanzani.... Filamu hiyo  ambayo yupo Lulu, Diana Kimaro, Jengua na Hashim Kambi itazinduliwa tarehe 30 mwezi huu katika ukumbi wa Mlimani City Kupitia  account  yake  ya  instagram, Lulu  amepost  ujumbe  huu.