Posts

Showing posts from April 8, 2017

Nape amtaka Rais Magufuli aunde tume

Image
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Mtwara kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye amtaka Rais Magufuli aunde tume huru ambayo itaweza kuchunguza matukio ya uhalifu ya uvamizi wa studio unaoendelea nchini. Mbunge Nape Nnauye akilia kwa furaha baada ya wananchi wa jimbo lake wakimtaka kupita juu ya migongo ya wamama ambao walijipanga ili kiongozi wao huyo apite juu yao, kwa heshima. Hatua hiyo inatokana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea Tanzania na kuacha maswali mengi vichwani mwa wananchi kushindwa kufahamu kuwa watu hao na vikundi hivyo vya kihuni vinavyofanya vitendo hivyo vinapata wapi mamlaka hayo kuwa na nguvu kushinda Dola. “Ombi langu kwa Rais namuomba aunde tume huru ichunguze matendo haya yasijirudie tena kwa sababu yasipochukuliwa hatua yataharibu sura ya Tanzania pia yataweza kuibuka makundi ya wahuni kuanza kuteka watu nao kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa. Tumsaidie Rais Magufuli kwa kumwambia ukweli naimani atasikia na atafanyia kazi

14 Things Men Only Do When They’re Crazy About You

Image
When you start falling for someone, it’s exciting, but also terrifying. You’re not sure if he feels the same way back, and you’re looking for signs while also attempting to sus out red flags. Here are some signs that you can let that guard down and finally relax with the knowledge that he wants you for keeps. 1. He doesn’t noticed the cellulite and stretch marks – he finds you beautiful not in spite of your flaws, but with them in mind. Now that’s a real man. 2. He tells you what you don’t what to hear, but what you need to hear. This guy isn’t feeding you lines, and it means he really cares and has your best interest at hear.    3. He’ll do spa nights with you. Yes, he will go to spas and get that mani/pedi and green tea mask with you, without shame that guy friends will see. Now that’s true love – has just wants to do what makes you happy.   4. Similarly, he’ll even go shopping with you . Those are usually husband or serious boyfrie

Breaking News: Roma apatikana, yupo kituo cha Polisi Oysterbay

Image
  Msanii Roma Mkatoliki anadaiwa kupatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar . Habari ya akina Roma kupatikana imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada. Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanadaiwa kuwepo kituoni hapo kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo. Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii. Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake. Taarifa zaidi zinafuata..

Sababu za Faru Fausta kutumia Sh760 milioni kwa mwaka zatajwa

Image
Arusha. Hakuna bosi yeyote serikalini anayelipwa zaidi ya Sh17 milioni baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza sera zake za kubana matumizi, lakini yupo kiumbe hai mmoja tu ambaye matumizi yake yalifika Sh64 milioni kwa mwezi; na kuna sababu za kuhalalisha gharama hizo. Kiumbe huyo ni mnyama mwitu aina ya faru aliyepewa jina la Fausta, ambaye sasa anatumia Sh20.4 milioni. Fausta ndiye faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia. Fausta anaishi Hifadhi ya Ngorongoro ambako analindwa kwa saa 24 kumuepusha kushambuliwa na wanyama wengine kama fisi na mbwa mwitu kutokana na uzee, lakini gharama za ulinzi zitapungua baada ya kupata makazi salama ndani ya mwitu jengo lake litakapomalizika. Hiyo ni sehemu tu ya gharama zinazomfanya Fausta kutumia fedha nyingi zaidi ya mfanyakazi mwandamizi wa serikalini. Kazi ipo kwe

SUPERSTAA DIAMOND PLATNUMZ ATOA SABABU YA KUACHIA NYIMBO YAKE MPYA "ACHA NIKAE KIMYA

Image
Diamond Platnumz ameachia wimbo wake mpya kwa kushtukiza uitwao ‘Acha Nikae Kimya.’ Wimbo unazungumzia masuala mengi yanayotokea sasa ikiwemo hofu iliyotanda baada ya Roma na wenzie kutekwa. Wimbo huo hata hivyo umepokelewa kwa hisia tofauti. Hizi ni sababu zake kwanini ameamua kuuachia: Ili Nchi ipate maendeleo inahitaji Upendo na Ushirikiano wa Wananchi na Serikali..Na Nikiwa kama Msanii, jukumu langu ni kuhakikisha natumia Hekma na busara kukemea jambo nilionalo haliko sawa ili lirekebishwe, lakini pia panapokuwa hakuna maelewano jukumu langu pia ni kupatanisha ili kwa pamoja tujenge nchi yetu kusudi wazazi wetu, watoto pamoja na familia zetu waishi kwa Upendo Amani na kufurahia nchi yetu…Na ndiomaana kwenye nyimbo nakwambia “MI NA WEWE WA TAIFA MOJA…KAMBARAGE BABA MMOJA….SASA TOFAUTI ZA NINI TUSHIKAMANE TUKAIJENGE TANZANIA”… Unatakiwa utambue kuwa kila kiongozi ni Binadamu na kama wote tujuavyo, Binadamu hatujakamilika… hivyo katika nch

Bashe: ‘Uchunguzi makontena ya mchanga uoneshwe kwenye TV’

Image
MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe(CCM), ameiomba Kamati iliyoundwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kuchunguza makontena ya mchanga katika Bandari ya Dar es Salaam, kurekori kilichomo katika makontena hayo ili yaoneshwe kwenye televisheni kwa lengo la kuwaondoa hofu Watanzania. Ombi hilo limekuja siku chache baada ya Rais Magufuli kuunda Kamati kwa ajili ya kuchunguza makontena ya mchanga katika Bandari ya Dar esSalaam. Alitoa ombi hilo bungeni mjini hapa wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi yaWaziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018. Alisema wengi wanaamini kwamba yale makontena yaliyokamatwa bandarini yana dhahabu. “Spika kule kwangu Nzega wanaamini yale makontena yaliyopo bandarini yana dhahabu,tunaomba mrekodi hili tukio la uchunguzi halafu mtuoneshe kwenye TV tuone kilichomo ndani ya zile kontena,” alisema. Alisema yeye ni miongoni mwa watu amba

Mdee: Niliwahi Dodoma kuepuka kukomolewa

Image
Dar es Salaam. Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amesema aliamua kuwahi Dodoma kuepuka kukomolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyeagiza afike mbele ya Kamati ya Maadili jana asubuhi na kuagiza polisi wamsake popote alipo, ikiwezekana apelekwe akiwa amefungwa pingu. Mdee, ambaye alikuwa Dar es Salaam wakati amri hiyo ikitolewa juzi saa 5:00 asubuhi, aliwasili Dodoma jana, lakini suala lake litajadiliwa leo. “Spika ana mamlaka ya kisheria ya kuomba vyombo vingine vya dola kumsaidia kumkamata mtu,” alisema Mdee alipoongea na Mwananchi jana. “Kwa sababu hiyo, ana uwezo wa kutumia mamlaka hayo kumkomoa mtu. Ndiyo maana nikaja mwenyewe Dodoma. Niliacha majukumu mazito niliyokuwa nayo ili lengo lake la kunikomesha lisifanikiwe,” alisema. Spika Ndugai, aliyezungumza kwa ukali, alisema anajua kuwa Mdee alikuwa nje ya Dodoma, lakini akataka awe amefika mbele ya kamati hiyo jana muda sawa na ule aliokuwa akitoa maagizo hayo juzi. Mdee anatuhumiwa kutoa lugha