Posts

Showing posts from October 10, 2016

EXCLUSIVE: Babu Seya, Papii Watuma Ujumbe Mzito Kwa JPM!

Image
Papii Kocha (katikati) akiimba na baba yake Nguza Viking (kulia). DAR ES SALAAM!  Kwa Wabongo walio wengi, majina ya Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ siyo mageni. Wao ni wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha ndani ya Gereza la Ukonga, Dar baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kulawiti na kunajisi watoto 10. …Wakipelekwa mahakamani kabla ya hukumu yao. Tangu kufungwa kwao, mwaka 2004, miaka 12 iliyopita, mengi yamesemwa, mengi yameandikwa, lakini wenyewe hawajawahi kufungua vinywa kusema lolote, hivyo kwa mara ya kwanza, Septemba 3, mwaka huu, Risasi Mchanganyiko, limekutana nao ndani ya gereza hilo na kufanya nao mahojiano yaliyochukua dakika 55. ILIKUWAJE? Septemba 2, mwaka huu, Risasi Mchanganyiko lilipata taarifa kwamba, wafungwa hao waliandika barua kwa Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ wakiomba msamaha kutoka kwake ili waachiwe huru. Ili kuweka sawa mzani wa habari, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen Mwa

MASAUNI ALITAKA JESHI LA MAGEREZA KUTEKA SOKO NDANI YA NCHI

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akijionea kiatu aina ya Safari buti kinachozalishwa na Kiwanda cha Karanga kilichopo Mkoani Kilimanjaro wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kiwandani katika Mkoa huo. Masauni amesisitiza kiwanda hicho kuzalisha bidhaa bora zaidi ili kuteka soko kubwa zaidi pamoja na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho Mrakibu Msaidizi, Michel Minja na kushoto ni Ali Jambaraga Fundi Mkuu.  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akiangalia kiatu kilichokuwa tayari kuvaliwa kilichotengenezwa katika kiwanda cha Karanga kilichopo Gereza Kuu la Karaga mkoani Kilimanjaro. Naibu Waziri huyo amesisitiza Jeshi hilo kuzidi kutengeneza bidhaa bora zaidi za viatu ili kuhakikisha wanapata soko kubwa ndani nan je ya nchi., kulia ni Kamishan Msaidizi Mwandamizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa aliye aambatana nae

RAIS MAGUFULI AMTEUA MHANDISI JAMES MITAYAKINGI KILABA KUWA MKURUGENZI MKUU TCRA

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mhandisi James Mitayakingi Kilaba at