Posts

Showing posts from July 13, 2016

STEVE NYERERE AIZUNGUMZIA ISSUE YA KUKOSA U DC ,AELEZA MENGI

Image
Baada ya madai kuwa msanii wa filamu, Steve Nyerere alikuwa na matumaini ya kuteuliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika uteuzi wa wakuu wa wilaya (ma-DC) wapya, staa huyo wa filamu amefunguka na kuzungumzia issue hiyo. Steve Nyerere Steve Nyerere amesema yeye ni mmoja kati ya watu ambao walikuwa wanasubiria uteuzi wa ma- DC na hajajisikia vibaya kukosa kwa kuwa ana imani bado Magufuli anamwangalia. “Mtu kama upo smart kwanini usisubirie nafasi kama hizo, mimi ni mtu safi na kazi naiweza,” alisema Steve. Aliongeza, “Uteuzi nimeusikia, tuombe mungu kama akinifikiria kwa awamu nyingine sio mbaya, tena ningependa Kinondoni, ni sehemu ambayo naona naweza kuifanyia kazi vizuri kwa sababu hata kwenye nafasi za ubunge nilishika nafasi yatatu, kwa hiyo kama ningepata Kinondoni ingekuwa poa zaidi” Mwigizaji huyo ni mmoka kati ya wasanii ambao walikuwa katika team ya kampeni ya Magufuli katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Njombe kidedea Kampeni ya Usafi, yatwaa Toyota Land Cruiser

Image
         Waziri wa afya, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisoma hotuba katika hafla hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  akiwakabidhi cheti baadhi ya wawakilishi kutoka halmashauri zao. …Akiendelea kukabidhi vyeti vya ushindi. …Akikabidhi kombe kwa mmoja wa wakilishi wa halmashauri hizo. Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi kombe wawakilishi wa halmashauri zao. Baadhi ya wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali wakipita mbele kupewa mkono wa hongera. Waziri Mwalimu (kushoto) akiwa na baadhi ya wawakilishi wa Halmashauri ya Mkoa wa Njombe. Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa halmashauri zilizoibuka kidedea kwa usafi. Mwalimu (mwenye kilemba kichwani) akishuhudia gari la ushindi lililotolewa Njombe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Njombe, Valentino Aidani,  akiwa ndani ya gari walilojishindia. Gari la ushindi wa Halimashauri ya Njombe. HALMASHAURI ya Mkoa wa Njombe leo imeimbuka kidedea na kutwaa gari aina ya  ‘Toyota La

Nafasi 500 za Udereva Kutoka UDA

Image
Uongozi wa UDA Management Agency Limited unatangaza kazi za Madereva 500 wenye leseni daraja “C” na uzoefu wa kuendesha mabasi ya abiria kwa miaka kuanzia 2 na kuendelea. Maombi yawasilishwe kwa Charles Nzilankoma -Operations Manager 0763 600 376 au kwa Cyprian Malekela 0754 266 029 kwa Usaili wa awali.

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA MAJIJI, MANISPAA,MIJI NA WILAYA WALA KIAPO CHA AHADI YA UADILIFU KWA VIONGOZI WA UMMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kuwatumikia wananchi ikiwemo kuondoa kero zinazowakili wananchi katika maeneo yao kama utitiri wa kodi hasa kwenye bidhaa wanazozalisha.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya (Hawapo pichani) walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kwenye matumizi ya Kanuni, Sheria na Taratibu katika kutimiza majukumu y

Mfanyabiashara Anayedaiwa Kujipatia Milioni 7 Kwa Dakika Afikishwa Mahakamani Na Kusomewa Mashitaka 199

Image
Hatimaye mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa amekuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika, amepandishwa kizimbani na wenzake wanne na kusomewa mashtaka 199, wote kwa pamoja. Mfanyabiashara huyo, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif Kabla, walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.  Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni. Katika ya mashtaka hayo, Yusufali maarufu kwa majina ya Mohamedali, Choma au Jamalii anakabiliwa na mashtaka 198 yeye peke yake huku wenzake wakikabiliwa shtaka moja la utakatishaji fedha. Kutokana na wingi wa mashtaka hayo, waendesha mashtaka wawili; Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro na Wakili wa Taasisi y

Cameron Kuachia Ngazi Leo Uingereza

Image
David Cameron . Theresa May leo anakuwa waziri mkuu wa pili mwanamke katika historia ya nchi ya Uingereza baada ya Margaret Thatcher aliyetumikia nafasi hiyo kati ya 1979-1990. Waziri mkuu huyo mtarajiwa  huenda akaongeza nafasi nyingi zaidi za wanawake kwenye baraza la mawaziri. Mwanamama Amber Rudd huenda akateuliwa katika moja ya nafasi nyeti ya waziri wa mambo ya ndani au waziri wa fedha. Justine Greening. Justine Greening na Priti Patel waliokuwa vinara wa kutaka nchi ya Uingereza kujitoa kwenye Jumuiya ya Ulaya wanapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa na waziri mkuu mpya anayeamini umefika wakati wa wanawake kupewa majukumu zaidi katika nafasi nyeti ndani ya serikali. Priti Patel. Waziri mkuu mtarajiwa anaweza kuvunja rekodi ya kuwateua wanawake wanane kwenye baraza lake la mawaziri. Leo asubuhi waziri mkuu aliyejiuzulu atawasilisha barua kwa Malkia Queen Elizabeth II itayohitimisha utawala wake na kutoa nafasi ya kuundwa kwa serikali mpya ya May.

Polisi wavamia nyumbani kwa Diamond usiku!

Image
Diamond Platnumz IMELDA MTEMA NA GABRIEL NG’OSHA DAR ES SALAAM: Polisi wenye silaha hivi karibuni wali ka nyumbani kwa msanii nyota, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayeishi Mivumoni Madale na kusitisha shughuli za burudani zilizokuwa zikiendelea ndani, Risasi Mchanganyiko limedokezwa. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, shughuli iliyositishwa  na polisi ilikuwa ni ile ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama mzazi wa mkali huyo wa muziki, Sanura Kassim ‘Sandra’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Ilidaiwa kwamba msanii huyo amekuwa akifanya sherehe mara kwa mara katika nyumba yake hiyo, hali inayosababisha kero kwa baadhi ya majirani zake, ambao nao, wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwa viongozi wa serikali ya mtaa huo. Nyumbani kwa Diamond Platnumz Gazeti hili baada ya kuupata ubuyu huo, lilifunga safari hadi nyumbani kwa msanii huyo na ku kia ofisini kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha ambaye baada ya kuulizwa ku