Posts

Showing posts from September 13, 2016

WABUNGE WATOA POSHO KUSAIDIA MAAFA KAGERA

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi) George Simbachawene amesema madaktari bingwa zaidi ya 15 kutoka Mwanza wamepelekwa Kagera kwa ajili ya kuongeza huduma kwenye hospitali. Kadhalika, wabunge wameunga mkono juhudi za serikali na wameridhia kukatwa posho ya siku moja ili kuchangia kusaidia maafa yao. Hatua hiyo inafuatia muongozo wa mbunge wa Mlalo CCM, Rashid Shangazi aliyeomba kiti kutoa muongozo ili wabunge watoe fedha hizo kama sehemu ya kuomboleza pamoja na waathirika. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa pande zote bila kuangalia itikadi zao. Hata hivyo, Mbunge wa Tarime vijijini Chadema John Heche alisema chama chake kilishatoa Sh 100,000 kila mbunge lakini kufuatia hoja hiyo na wao wapo tayari kuchangia posho zao.

SELECTION ZA VYUO VIKUU KWA WANAFUNZI WALIOOMBA KUJIUNGA NA VYUO MBALIMBALI MWAKA HUU ZIMETOKA

Image
Selection za TCU kwa walioomba kujiunga na vyuo mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2016/2017  z imetoka. Bofya hapa  kuangalia     Selection Status  NB:  Tumia index number yako na password

MAAJABU: HUYU NDIYE BINADAMU MWENYE VIDOLE 12 MIGUUNI NA MIKONONI!

Image
Vijay akionesha vidole vyake 12 vya mikono.  Mchapaji wa India Vijay Singh anaweza kuchapa zaidi ya maneno 100 kwa dakika kwa kutumia vidole vyake 12.  Lakini Vijay, ambaye pia ana vidole 12 vya miguuni kutokana na dosari yake hiyo ya kimaumbile, anasema hawezi kupata kazi katika nchi yake aliyozaliwa sababu waajiri wanataka tu wanawake wenye mvuto. Sasa anapanga kuhamia Uingereza kwa lengo la kutafuta ajira baada ya kuwa amekataliwa maombi yake ya kazi zaidi ya 50. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 48, anayetokea Agra kaskazini mwa India, alisema: "Wanataka wanawake wenye mvuto, si wanaume wenye vidole 12." Miguuni pia, Vijay ana vidole 12.  Watu wenye dosari za kimaumbile wanaonekana wenye bahati nchini India na Vijay yuko kwenye hali nadra kutokana na vidole vyake vya ziada kufanya kazi kama kawaida.  Watu wengi wenye hali hiyo wana vipande vichache vya tishu laini ambazo zinaweza kuondolewa na mara chache huwa na mfupa

Jamhuri Yajibu Kesi Ya Dada’ke Msuya

Image
UPANDE wa Jamhuri leo umetoa majibu ya hoja ya kutaka kufutiwa mashtaka ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyela. Awali, wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliwasilisha maombi ya wateja wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kile alichodai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa ina mapungufu kwa kuwa haioneshi kama washitakiwa hao walikuwa wana nia ovu. Akijibu hoja hiyo ya Kibatala mahakamani hapo, wakili wa serikali, Diana Lukundo alisema hoja zote walizoziwasilisha na upande wa washtakiwa haziko kisheria na kuna aina mbalimbali za kuwasilisha mashtaka. Baada ya upande huo wa Jamhuri kujibu hoja hizo za upande wa washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkuu, Magreth Bankika, mahakama hiyo inatarajia kutoa maamuzi ya hoja hiyo Septemba 27, mwaka huu. Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mnamo Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam, Miriam Mrita na Revocatus Muye

TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA LAPELEKEA SHULE ZA SEKONDARI ZA IHUNGO NA NYAKATO KAFUNGWA KWA MUDA

Image
Shule ya Sekondari Ihungo iliyoko mjini Bukoba huko Kagera yafungwa hadi Septemba 26 baada ya miundombinu kuharibiwa na tetemeko la ardhi, diwani wa kata ya Nshambya Jimmy Karugendo athibitisha leo asubuhi. Mwenyekiti wa taifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe aliishauri serikali kuifunga shule ya sekondari ya Ihungo ambayo imepata madhara makubwa kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera na kuunda kamati ya kitaifa ya maafa itakayoshughulikia madhara yaliyotokana tetemeko hilo liliyoyakumba maeneo mbalimbali yaliyoko katika mkoa huo. Alitoa kauli hiyo baada ya kujionea madhara yaliyotokana na tetemeko hilo katika shule hiyo hali inayowalazimu wanafunzi kulala kwenye uwanja na madhara ya nyumba za makazi ambazo zimeharibika vibaya na nyingine kuanguka kabisa, amesema madhara ya tetemeko hilo serikali inapaswa kuyachukulia kama moja ya majanga la kitaifa.