Posts

Showing posts from April 17, 2015

HIZI NDIO TAARIFA ZENYE UHAKIKA KUHUSU ALIYEKUWA MPENZI WAKE LULU MICHAEL

Image
Mitandao ya kijamii kuanzia kwenye Whatsapp mpaka twitter, Facebook na Instagram siku hizi imekua na nguvu kubwa na ndio maana hata taarifa zinaenea kwa kiasi kikubwa sana siku hizi bila kungoja Magazeti, Radio au TV. Najua kama unafatilia habari zinazoendelea mjini utakua umekutana na voicenote au taarifa ya kifo cha huyu ndugu yetu inaweza kuwa imekufikia lakini sio kwa usahihi, au chanzo cha kifo kinaweza kuwa kimepotoshwa.   Sasa familia ya Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga ( Secky ) imekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kupitia voice note na kwenye mitandao kuhusu chanzo cha kifo chake na kwamba alikwenda kwenye birthday,  "ukweli ni kwamba aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba mtoto wake nyumbani kwake, akapelekwa hospitali na baadae akafariki akiwa Hospitali, hakuna kingine zaidi ya hapo". Secky alikua rafiki wa watu wote wakiwemo wasanii wengi wa bongofleva na hata bongomovie pia ndio maana msiba huu umewagusa kutokana

Majibu ya Amanda Kuhusu Madai ya Kutumia ARV

Image
Staa wa Bongo Movies, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni aligeuka mbogo kwa shabiki wake aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi. Ishu ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya Amanda akipima ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo alipokomenti kwamba eti msanii huyo ana ngoma.Akizungumza na Ijumaa, Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu mtandaoni wakidhani kila msanii ni mhuni. “Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote tunatumia ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,” alisema Amanda.

AJALI MBAYA YATOKEA KIWIRA MKOANI MBEYA YAUWA WATU 18 ASUBUHI HI!!

Image
Habari zaidi zitawajia punde tutakapozipata

IRENE UWOYA ANA MIMBA YA PILI?! SOMA ALICHOKIANDIKA NA TAZAMA PICHAZ HAPA...

Image
Staa mrembo wa Bongo, Irene Uwoya amewaacha njia panda mashabiki wake baada ya kubandika picha mtandaoni akionekana yupo bafuni akiwa amejishika tumbo na kuiandikia maneno akiwatata mashabiki wamtajiae majina mazuri ya kike. “Ntajie majina mazuri yakike unayoyapenda.....”- Uwoya aliandika. Kauli hii ilizua maswali mengi kutoka kwa mashabiki wakioji kama mrembo ambae ni mama wa mtoto mmoja kama anaujamzito au la, wengine walienda mbali zaidi wakisema kuwa inawezekana akawa ni mjauzito na anatarajia kujifungua mtoto wa kike. Mbali komenti nyingi kumtaka atoe maelezo zaidi juu ya hili, Uwoya hakujitokeza kusema lolote hivyo hadi sasa mashabiki wake wapo njia panda wakijiuliza, …ana ujauzito au hana? Swaga kama hizi ya mtandaoni huwa mara nyingi zina maaanisha picha picha za tumbo zimekuwa nyingi sana kutoka kwa mrembo huyo. ngoja tuendelee kusubiri kwani hili ni jambo la kheri. Mzee wa Ubuyu

HALI ILIVYOKUWA NYUMBANI KWA GWAJIMA LEO

Image
Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima. Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote. Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano. Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio. Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio. Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.  Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.  Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.  Baadhi ya waumini wa Gwajima wakifuatilia kwa makini hali iliyokuwapo.  Baadhi ya waumini wakiwa mbele ya nyumba ya Gwajima. Gari la polisi likiondoka eneo la tukio. Hapa wakishangilia ushindi baada ya polisi kuondoka eneo la tukio. WAKATI taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili n

TAARIFA KAMILI KUHUSU WALIOFUNIKWA NA KIFUSI MKOANI SHINYANGA!

Image
Eneo la machimbo ya madogo ya dhahabu ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.  Mpaka sasa inadaiwa wachimbaji wadogo wadogo 20 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika machimbo madogo ya dhahabu ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema waliofariki dunia ni watu 19 ambapo usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao. Baadhi ya duara ya simo la kuchimba dhahabu katika kijiji cha Kalole wilayani Kahama mkoani Shinyanga.