Posts

Showing posts from September 23, 2016

Shoga: tui la nazi lazima lionjwe!

Image
SHOGA yangu u hali gani? Ni siku nyingine tena tulivu imefika na tumekutana kwenye kona yetu hii inayowaelimisha wengi hususan wanawake wenzangu japo wanaume nao siwaachi nyuma. Natumai na wewe ni mzima wa afya na kama mgonjwa nakuombea kwa Mwenyezi Mungu atakutia nguvu. Baada ya hayo tugeukie basi kwenye hiki kilichonifanya niwaandikie, si mnakumbuka mara ya mwisho nilitoa somo la chakula cha usiku hakifunikiwi! Wengi mlinipigia simu na kunitumia meseji jinsi mnavyowafanyia waume zenu. Inanipa raha sana kuona mada imewaingia kisawasawa na kuyafanyia kazi shoga, mwanamke sharti ujue kukipika chakula bwana! Kiwe kitamu pia usimfunikie mume wako eti kwa kuhofia nzi au kupoa, kifunue ili akila ajihisi ameridhika, upo? Shoga baada ya hayo, nimepata maswali mengine mengi kutoka kwa nyie wasomaji wangu wengi mnaniuliza hivi tui la nazi lina utamu gani? Wengine mnauliza kwani lazima lionjwe? Jamani hata hili kweli la kuuliza au la kujiongeza mwenyewe? Umeshaandaa m

Ufanyeje unapompenda aliyependwa?

Image
KWANZA nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kuandika haya tena wiki hii tukiwa wazima. Lakini pia tumshukuru kwa kutuletea kitu kinachoitwa mapenzi. Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda. Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa. Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyo-pendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma. Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume unaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake yaani ameshapendwa. Moyo w

Wastara, Bond Mapenzi Upyaa!

Image
STAA wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma na meneja wake, Bond Suleiman mapenzi yao yamerejea upya baada ya miezi kadhaa nyuma Wastara kumtosa na kwenda kuolewa na Mbunge wa Jimbo la Donge-Zanzibar, Sadifa Juma. Kurejea kwa penzi la wawili hao kulibainika baada ya hivi karibuni waandishi wa habari hii kufika nyumbani kwa Wastara maeneo ya Magereza Relini jijini Dar na kumkuta Bond akiwa amejaa tele huku wakioneshana mahaba ya njiwa.  Wastara afunguka  Licha ya kwamba mwanzo zilipovuja taarifa kuwa wamerudiana walikuwa wakitumia nguvu kubwa kukanusha, safari hii walipobambwa hawakuwa na ujanja zaidi ya kuamua kuanika kila kitu kweupe. Staa wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma na meneja wake, Bond Suleiman wakiwa pamoja. “Kweli tumeamua kurudi kwenye penzi letu na sikutaka kufunguka mapema kwa sababu siyo kila uhusiano unaufungukia kwani si kila mtu anayependa, nimepitia matatizo mengi na sababu kubwa ni wanadamu hivyo sikuona haja ya kutangaza tena huu uhusiano.

Irene Uwoya: Mapedeshee Siku Hizi Hawatoi Pesa

Image
Staa wa Bongo movie, Irene Uwoya ‘Mama Krish’. MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii uipendayo ya 10 Question? Kama kawa, kama dawa wiki hii tunaye mwanamama ambaye bado ni mrembo, Irene Uwoya ‘Mama Krish’. Naye yuko hapa kujibu maswali mbalimbali ambayo amembana nayo na yeye akaonesha ushirikiano katika kuyajibu. Je, una shauku ya kujua ni maswali gani aliyobananishwa nayo na akajibu vipi? ‘Intaviu’ hii hapa chini inakuhusu… Ijumaa: Hivi ni ipi siri ya wewe kuonekana mrembo siku zote? Uwoya: Cha kwanza mimi najipenda sana, kingine napenda kutumia vitu kwenye ngozi yangu ambavyo havina madhara na nakula matunda sana.  Ijumaa: Ni kweli wewe na Ndikumana bado ni mke na mume au ndo’ vile? Uwoya: Ndoa ya Kikristo haivunjiki bwana, mimi bado hakuna jinsi. Ijumaa: Hamna mpango wa kuishi pamoja na kumlea Krish wenu? Akiwa katika pozi. Uwoya: Ipo siku Mungu atajaalia itakuwa hivyo. Ijumaa: Uliwahi kusema unataka kupata mtoto wa pili kupitia kwa huyohuy

Rais Magufuli Ateua Viongozi Shirika la Ndege La Tanzania (ATCL)

Image

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA JAMHURI YA KOREA HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young mara baada ya kupokea picha hiyo ya mfano wa Daraja jipya la Salenda. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini hadi eneo la Coco

KWETU FASHION ILIVYOWAKILISHA MAVAZI YA KIMASAI KATIKA SHUKHULI YA East Africa cultural festival 2016 U.S.A.

Image
 Vivazi vya Missy Temeke wa Kwetu Fashions vikiwa tayari kwenye onesho la mavazi la Utamaduni wa Afrika Mashariki lililofanyika Onley, Maryland siku ya Jumamosi Septemba 17, 2016.  Missy T (kati) akiwa katika picha ya pamoja na models wake wakiwa na vivazi vya kimasai.