Ruge akanusha Gerald Hando na PJ kuacha kazi!

12809737_1074835289226555_2108898734342699721_n
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
MKURUGENZI wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba,  leo kupitia kipindi cha Power Breakfast‬ amekanusha uvumi wa watangazaji wa kituo hicho, Gerald Hando, Abel Onesmo na PJ,  kuacha kazi.
“Kwa nafasi yangu kama mkurugenzi,  taarifa nilizonazo ni kwamba tuna mikataba na wafanyakazi hao ambayo inaisha leo tarehe 31.  Sehemu kubwa ya wafanyakazi  wetu mikataba yao inaisha mwezi huu, hivyo  katika hali ya kawaida huwa tunatoa nafasi ya kumwambia anayetaka kuendelea na mkataba aandike barua au aseme,” alisisitiza Mutahaba

Comments

Popular posts from this blog