Posts

Showing posts from June 19, 2013

KISWAHILI KITUMIKA HADI VYUO VIKUU MBUGE AJENGA HOJA

Image
MBUNGE wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM), amehoji lini serikali itapitisha Kiswahili kitumike kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu. Aidha, alisema mwaka 2004, Umoja wa Afrika ulipitisha Kiswahili kiwe ni lugha ambayo itatumika katika mikutano na shughuli mbalimbali. “Je, serikali imejiandaa vipi kupeleka wakalimani wa kutosha kutoka Tanzania ili waweze kujipatia ajira?” alihoji. Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala alisema jitihada zinafanywa na taasisi hizo za kukuza Kiswahili mojawapo kuandika vitabu vingi vya kufundishia na kuongeza wataalamu. “Nasema wazo hilo tumelipokea na sisi ndani ya serikali tunaendelea kulifanyia kazi na hata wakati tunawasilisha bajeti yetu zilitoka hoja hizo za kuwa Kiswahili kifundishwe madarasani,” alisema. Aidha, Makala alikiri kupitishwa kwa azimio hilo na kuongeza kuwa: “Kama Tanzania tumeona kuwa hii ni fursa muhimu na tayari moja ya kazi zinazofanywa na Taasisi za k

ARUSHA KWACHAFUKA TENA.....MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA WANANCHI

Image
  Hali kutoka mkoani si nzuri...mabomu ya machozi yanapigwa  kuwatawanya  wananchi  waliojitokeza  kuiaga  miili ya  wananchi  waliofariki katika mlipuko wa bomu... Hivi sasa polisi wanapiga mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliofurika katika uwanja wa Soweto Mjini Arusha ulipotokea mlipuko wa bomu Jumamosi kuomboleza ambapo polisi inasema mkusanyiko huo si halali Taarifa toka mkoani humo zinadai kuwa gari la mh. Lissu liteketezwa vibaya kwa bomu.

SABABU ZA JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU YA MABOMU JIJINI ARUSHA

Image
Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo . Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi. Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo. Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza .. Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta  mvutano kati ya vi

NAPE , GODBLESS LEMA NA MBOWE WATAKIWA KUPELEKA ASHAHIDI WAO POLISI, VINGINEVYO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE

Image
Jeshi la Polisi limetishia kuwakamata Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na limesema litamhoji Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya wanasiasa hao kudai kufahamu watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja aliwataka wanasiasa hao kuwasilisha ushahidi wa kile wanachofahamu kuhusu kulipuliwa kwa bomu hilo. Juzi, Mbowe akiwa na Lema, alisema wana ushahidi wa picha za video zikiwahusisha polisi na kulipuliwa kwa bomu hilo katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani kwa Chadema, Jumamosi iliyopita. Mkwara wa Chagonja Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na Lema kupeleka ushahidi ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo. “Tunamtaka Mbowe na Lema kutoa ushahidi wa askari wetu kuhusika na tukio la bomu pale Soweto. Wasipofanya hivyo tutatumia sheria kuwalazimisha kufa