Posts

Showing posts from April 18, 2017

Upendo Nkone autaka Ubunge

Image
Mwanamuziki wa injili, Upendo Nkone amesema yuko tayari kutumikia nafasi ya ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo  Rais Magufuli atamteua. Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Upendo alisema, anaamini ametumwa na Mungu kufikisha ujumbe wake kupitia uimbaji, lakini pia yuko tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge, na kuweka wazi kuwa si kwa ubunge wa kugombea jimboni. "Sina mpango wa kuwa mwanasiasa, kwahiyo hata ubunge wa kugombea siwezi, lakini kama Rais wangu Magufuli akilala akiota kwamba anipe ubunge viti maalum, kwakweli napokea.... Mh. Magufuli nimeambiwa nigombee ubunge, basi unikumbuke baba" Amesema Upendo Amesema aliwahi kushauriwa kugombea ubunge katika jimbo fulani lakini hakuwa tayari kwa kuwa hapendi kugombea. Akieleza sababu kuu ya kutopenda ubunge wa kugombea, amesema masharti ya kugombea ni lazima uwe kwenye vyama vya siasa jambo ambalo halipendi. Jambo lingine amesema mchakato wa kupata ub

JACQUELINE NTUYABALIWE ANYAKUA TUZO ZA A-PRIME DESIGN

Image
Mrembo wa Tanzania mwenye tamaa ya kuwa na himaya ya samani za kimataifa kupitia kampuni yake, kama alivyowahi kuelezwa na jarida la Forbes hivi karibuni, Jacqueline Ntuyabaliwe ametwaa tuzo mbili za ubunifu kupitia kampuni ya Molocaho by Amorette. Ushindi wake huo unamuingiza katika kundi la watu wenye ubunifu mkubwa wa bidhaa za majumbani na katika maofisi, muda mfupi tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. Molocaho by Amorette kampuni ya kubuni na kutengeneza samani ilizinduliwa Septemba 2016. Miezi michache tu tangu kuundwa kwake inaonesha kukimbia na kufanikisha tuzo tatu za kimataifa. Katika tuzo zenye ushindani mkali na heshima kubwa kwenye ubunifu za kimataifa zijulikanzo kama A-Prime Design (A'Design) zilizofanyika mjini Roma mwishoni mwa wiki Jacqueline amepata tuzo katika kategori mbalimbali na kuwa wa pili kategori nyingine.  Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi Bidhaa zilizompatia tuzo ni samani na pia za mwanga. Ngorongoro Settee ilimpatia medali ya shaba

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA NANE CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 APRIL 18, 2017 MJINI DODOMA

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO). Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais TAMISEMI Mhe. Luaga Mpina akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Mbunge wa Nanyamba (CCM) Mhe. Abdallah Dadi Chikota akiuliza sw

Breaking Nwez: Simba Yabaki Na Pointi Tatu Ilizopewa Na Kamati Ya Saa 72

Image
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemaliza kikao chake na Simba inaendelea kubaki na pointi ilizopewa na Kagera Sugar. Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine, amesema kamati hiyo itakaa tena na kuna shahidi wengine wataitwa kuhojiwa. Kikao hicho kimefanyika kuanzia leo asubuhi  katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na waamuzi, wafanyakazi wa bodi ya ligi, viongozi wa simba, Kagera Sugar, waamuzi wa mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon na beki Mohammed Fakhi wamehojiwa. Baada ya kuhojiwa, kilichofuatia lilikuwa ni suala la kamati kukaa kwa takribani saa moja kuonyesha walikuwa wakimalizia kuhusiana na kile walichowahoji wahusika. Kabla, kamati ya Saa 72, ilikuwa imeipa Simba pointi tatu na mabao matatu licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar. Kamati ya Saa 72, ilibaini Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akiwa na kadi tatu za njan

Wema Sepetu arudi kwa kasi bongo movie

Image
Tanzanian SweetieHeart Wema Sepetu amewataka watanzania ukaa mkao wa kula kwa kazi yake mpya Hii ni kufuata mfukulizo wa post zake kuhusu ujio wake mpya wa kazi zake katika kuigiza, amewaasa wabongo kuwapa ushirikiano wa dhati kabisa kwani amedhamiria kuirudisha Bongo Movies katika kiwango cha enzi zile za Kanumba Tanzanian SweetieHeart Wema Sepetu amewataka watanzania ukaa mkao wa kula kwa kazi yake mpya Hii ni kufuata mfukulizo wa post zake kuhusu ujio wake mpya wa kazi zake katika kuigiza, amewaasa wabongo kuwapa ushirikiano wa dhati kabisa kwani amedhamiria kuirudisha Bongo Movies katika kiwango cha enzi zile za Kanumba

Njia ya kupanga uzazi kwa kutumia Kalenda/ Kuzuia Mimba Kwa Njia ya Kalenda

Image
Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii i

Kikosi hatari cha US NAVY 'SEAL' chatua rasmi Korea Kasikazini

Image
NI wazi kuwa jaribio lilifanywa na Korea Kaskazini la Makombora yake ya Nukria  limeshtua  Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo la Florida nchini Marekani. Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya kimarekani. Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni Sea, Air and Land. Ni Mara chache s

VIONGOZI WA DINI WAJUMUIKA KUFANYA DUA MAALUM KUZIOMBEA MKURANGA NA KIBITI

Image
Rufiji. Viongozi wa dini ya Kiislamu Mkoa wa Pwani, wamefanya dua maalumu ya kuuombea mkoa huo ili kuirejesha hali ya usalama. Dua hiyo imefanywa wakati wilaya tatu za mkoa huo, Kibiti, Mkuranga na Rufiji zikikabiliwa na matukio ya mauaji ya mara kwa mara ya wenyeviti wa vijiji na maaskari polisi Alhamisi iliyopita watu wasiofahamika waliwashambulia na kuwaua polisi wanane waliokuwa doria katika Kijiji cha Jaribu, wilayani Kibiti. Askari mmoja alinusurika na kujeruhiwa mkononi. Mauaji mengine yanayotokea katika maeneo hayo ni kama lile la kuuawa kwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya. Hadi sasa viongozi wa vijiji zaidi ya 10, katika wilaya hizo wameuawa kwa kupigwa risasi au kukatwa mapanga tangu mwaka jana. Wakizungumza katika dua hiyo iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa, Ikwiriri juzi, Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Wilaya ya Mkuranga Sheikh Mohammed Katundu alisema wao kama viongozi wa dini wamelazimika kufanya ibada hi