Posts

Showing posts from July 21, 2018

Nafasi za Kazi 17 Mamlaka ya Maji Musoma

Image
Musoma Water Supply and Sanitation Authority (MUWASA) is a utility established under section 9 of the Water Supply and Sanitation Act No. 12 of 2009 with the objective of provision of Water Supply and Sanitation services in Musoma Municipality. In this respect, the activities of MUWASA have specifically expanded and the authority now invites application from suitably qualified and skilled individuals who are dynamic and result oriented to fill the following posts:- 1:0 Position: Assistant Technician II 6 Post 1:1 Reporting to: Production Engineer 1:2 Duties and Responsibilities 1) Customer Plumbers i. To repair all water leakages. ii. To assist in connecting new water customers as scheduled. iii. To report on unauthorized water connection. iv. To report of sewerage pipe faults to responsible officers. v. To assist in carrying out water disconnections and re-connections. vi. To reconnect water debtors as assigned timely. 2) Technical Plumbers i. To attend to cust

Mama Afungwa Jela kwa Kuruhusu Wanaume Kumbaka Mwanaye

Image
MWANAMKE Azzie Watson (25) wa Independence, Kansas City, Marekani, ameshitakiwa kwa kuuruhusu wanaume kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka miwili. Mahakama iliambiwa kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa kila mara anasema alimpeleka mtoto wake huyo kwenye nyumba fulani ambako alibakwa mara tano.  Maneno hayo yanadaiwa yalinaswa na rafiki yake wa kiume kwenye kinasa sauti. Watson alikana madai hayo, lakini pia akasema hajui ni kwa nini mtoto wake huyo aliambukizwa ugonjwa wa zinaa. Mtoto huyo wa mtuhumiwa na mdogo wake wa kiume walichukuliwa na kwenda kulelewa na watu maalum wakati kesi ilipoanza kuunguruma. Wakiwa huko, Juni 29, mwaka huu, mama anayemlea alimsikia binti huyo, wakati anamvua nepi, akimlalamikia mwanamme ambaye mlezi huyo hakumjua. “Baba inaumiza.  Baba, usiwe katili.  Baba, inaumiza,” alikuwa akilalamika mtoto huyo. Polisi wamemkata mwanamme mmoja Charles Green (43) kwa mashitaka mawili ya kuhatarisha maisha ya mtoto.  Mtu huyo anadaiwa kuw

JPM ATOA POLE KWA KIKWETE KUFIWA NA BABA MKEWE

Image
Rais John Magufuli akilakiwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete alipofika kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, marehemu Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2018. Mke wa Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli, akilakiwa na Kikwete kwenye msiba huo. Magufuli akimpa pole mke wa Kikwete,  Mama Salma Kikwete.  Magufuli  na Kikwete wakati wa dua.  …Dua ya familia kwa ajili ya marehemu. Rais na mkewe wakiagana na wafiwa. …Akiendelea kuagana na waliofika msibani. Magufuli na mkewe wakisindikizwa.  RAIS  John Magufuli na  mkewe Mama Janeth Magufuli , wamefika nyumbani kwa rais mstaafu, Jakaya Kikwete,   kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, marehemu Rashid Mkwachu, nyumbani Msasani jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2018. Picha na IKULU

Naibu Meya, Madiwani CHADEMA Wajiuzulu Mbeya

Image
IKIWA ni saa chache baada ya uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Mbeya kupendekeza kuwavua uanachama madiwani watatu wa chama hicho mkoani humo kwa utovu wa nidhamu waliouonyesha, madiwani hao wamejiuzulu nyadhifa zao hizo. Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Geofrey Kajigili (Sisimba), Newton Mwatuboje (Manga)na Hamphrey Ngalawa (Iwambi). Madiwani hao wamejiuzulu leo Jumamosi  Julai 21, 2018 baada ya Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu,  kutangaza uamuzi huo  katika mkutano wake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa  vikao halali vya chama vilivyoketi mara kadhaa kujadili hatua stahiki dhidi ya madiwani vimefikia uamuzi huo. Amesema kutokana na utovu wa nidhamu, kukiuka katiba ya Chadema na kukaidi utekelezaji wa maazimio ya uongozi, wamepeleka mapendekezo yao kwa uongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa ili  hatua zichukuliwe. Aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata ya Nsalaga Mjini Mbeya, Mchungaji David Ngogo (

Simba Kufikia Kambi ya Kishua Uturuki

Image
JUMLA ya wachezaji 26 wa kikosi cha Simba, wanatarajiwa kuondoka kesho Alfajiri kuelekea Uturuki kuweka kambi ya takribani wiki mbili kabla ya kurejea hapa nchini Agosti 5, mwaka huu. Wachezaji wa Simba ambao watakuwa kwenye safari hiyo jana Ijumaa walikuwa na zoezi la upimwaji wa afya kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar. Katika nyota hao 26 watakaosafiri, kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto, hatakuwepo kwenye msafara huo ambao utaongozwa na kocha mpya wa kikosi hicho, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji. Msafara mzima wa Simba unaotarajiwa kwenda Uturuki kwenye kambi hiyo, utakuwa na jumla ya watu 35. Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba, kimelidokeza Championi kuwa, mbali na Kazimoto, pia Mosses Kitandu, Jamal Mwambeleko, Ally Shomary na Said Mohammed ‘Nduda’ nao watabaki hapa nchini. “Kama ambavyo imepangwa, kikosi kitaondoka Jumapili alfajiri ambapo baada ya kocha mpya kutangazwa jana (juzi Alhamisi), yeye ndiye atakuwa anawaongoza vijana wake