Posts

Showing posts from February 22, 2016

Linah alala na Wizkid hotelini

Image
Mwanamuziki wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’. Stori: Musa Mateja, Wikienda Dar es Salaam: Imefichuka! Hatimaye ishu ya wanamuziki wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, kudaiwa kulala kitanda kimoja na msanii wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, imebumburuka. Baada ya kuandamwa na skendo hiyo ya kutoka kimapenzi na Wizkid huku mashabiki wake waliyo wengi wakishindwa kuamini juu ya uhusiano huo, hatimaye sasa mambo yamevuja na kujidhihirisha kuwa kweli staa huyo alilala hotelini tena kitanda kimoja na Mnigeria huyo. Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’. Kikieleza kwa kujiamini, kiliweka wazi kuwa Linah alilala kitanda kimoja na staa huyo kwenye hoteli moja iliyopo Masaki, Dar, baada ya msanii huyo kutua Bongo kwa ajili ya kufanya makamuzi kwenye moja ya shoo zake alizokuwa ameletwa na promota King Solomon. “Linah alilala na Wizkid, alikaa naye hadi siku anaondoka kulelekea Nigeria, na nikwambie ukweli uliyojificha ni kwamba, Linah ku

Wabunge wa Upinzani Waingia na Mabomu ya Machozi Bungeni...Wavaa Gas Mask na Kuyalipua...

Image
Hili ni bunge la Kosovo, nchi iliyojipatia uhuru mwaka 2008 baada ya Yugoslavia kusambaratika. Bunge la Kosovo ni bunge linaloongoza kwa vituko barani Ulaya. Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano mkali bungeni kati ya Serikali na wabunge wa upinzani. Hoja kuu ya upinzani ni Serikali itoe ufafanuzi kwanini nchi yao ya Kosovo imekithiri kwa rushwa, ubadhirifu, ukosefu wa ajira na umasikini. Tarehe 19 Februari mwaka huu bila kutarajiwa wabunge wa upinzani waliamua kuingia bungeni huku wakiwa wamejihami kwa kuvaa vifaa vya kuzuia gesi (gas mask) na kuanza kuwarushia wabunge wa chama tawala mabomu ya machozi.

WATU SABA AKIWAMO MTOTO WAUWAWA KWA RISASI MAREKANI

Image
Watu saba wameuwawa kwa kupigwa risasu akiwemo mtoto wa miaka nane huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika tukio la mauaji lililotokea huko Kalamazoo, Michigan nchini Marekani jana usiku. Mkuu wa Usalama wa Umma wa Kalamazoo Jeff Hadley mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa leo asubuhi. Polisi wamesema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwenye gari linaloshabihiana na lililotumiwa mshambuliaji, ambapo pia bunduki ilipatikana kwenye gari hilo. Mtuhumiwa huyo mzungu mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ni mkazi wa kaunti ya Kalamazoo, imeelezwa alijisalimisha bila ya purukushani.

Wasanii wawili wafa Bongo Muvi

Image
Stori: Imelda Mtema, Wikienda Dar es Salaam: Misiba! Wakati wadau wa Bongo Movies wakiwa kwenye majonzi ya kifo cha Michael Dennis ‘John Woka’, kwenye Bongo nako kuna pigo la kuondokewa na wasanii wawili, Maneno Gongo ‘Mr Gongo’ na Jennifer Vincent ‘Mama Utajiju’. Gongo alifariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na presha kwa muda mrefu. Marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa. Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, ndugu wa marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa, alisema kuwa msanii huyo alisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda refu na alikuwa akijaribu kila dawa bila mafanikio. Mchuwa alisema kuwa jamaa huyo alizidiwa hadi akakakamaa hivyo walimpeleka Muhimbili ambapo ndiko alikokutwa na umahuti. Msanii huyo ambaye alizikwa kwenye Makaburi ya Visiga, Kibaha mkoani Pwani amecheza filamu mbalimbali zikiwemo The Mask akiwa na Aunt Ezekiel, For Sale, Stolen Gold, Sara na nyinginezo. Wakati simanzi hiyo haijapoa, mwigizaji mwingine,

MUHONGO: NCHI INAHITAJI UMEME WA UHAKIKA

Image
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema ili Tanzania iwe nchi ya viwanda inahitaji umeme wa uhakika na nafuu. Mara kadhaa, Rais John Magufuli amekuwa akisisitiza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ili kukuza ajira kwa vijana na kukuza uchumi. Akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni jana, Profesa Muhongo alisema amewapa kazi Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuangalia namna ya kupunguza bei za umeme. Alisema amewaagiza wadau hao wa nishati kumpa ripoti kamili ya namna ya kupunguza gharama za umeme na vyanzo vya kuzalisha ifikapo Machi mwaka huu. “Lengo ni kuhakikisha tunaangalia namna ya kwenda katika uwekezaji wa viwanda huku kukiwa na umeme nafuu,” alisema. Alisema bei ya umeme haiwezi kupungua kama vyanzo vya kuzalisha umeme havitaongezeka. Alisema mkakati uliopo ni kuzalisha umeme wa makaa ya mawe ambao kwa sasa kuna tani zaidi ya bilioni 10 ambazo

A-Z Mchungaji Msigwa alivyotaka kuzichapa na DC

Image
   Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa (mwenye koti katikati) akizozana na mkuu wake wa wilaya ‘DC’, Richard Kasesela (wa kwanza kutoka kulia). Stori: Mwandishi, Wetu Wikienda IRINGA: Neno zuri linaloweza kutumika ni chupuchupu! Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa nusura azichape na mkuu wake wa wilaya ‘DC’, Richard Kasesela kufuatia mchungaji huyo kupandwa na hasira akidai anahujumiwa. Ishu hiyo ilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kitongoji cha Nduli wilayani Iringa ambapo wawili hao na viongozi wengine walikabidhi mabati kwa watu ambao mapaa ya nyumba zao yaliezuliwa na upepo ulioambatana na mvua. Viongozi wengine wakiongea nao baada ya mzozo huo. Ishu ilianza pale Msigwa alipoonesha kukasirishwa kwa DC huyo kutaka kumuengua kwenye picha ya kukabidhi mabati hayo.Mchungaji Msigwa alimjia juu DC akisema amekuwa akimhujumu kwa siri ili aonekane hafanyi kazi jimboni kwake. Hali ikawa hivi: Msigwa: Ananikosea sana h

KUKAGUA MIRADI YA MAJI YA RUVU JUU NA RUVU CHINI.

Image
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akitoka ndani ya moja ya tanki baada ya kukagua ukarabati wa matanki matatu eneo la Kimara yenye uwezo wa ujazo wa lita milioni 34. Aliyesimama juu ya tanki ni Mhandisi wa Mradi huo P. G. Rajan. Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba ya maji eneo la Kiluvya jijini Dar es salaam ili kukamilisha mradi wa ulazaji wa mabomba hayo na kuwahakikishia wakazi wa maeneo ya  Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata maji ya kutosha ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Machi mwaka huu. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo (kushoto) akipata maelezo ya mradi wa ukarabati wa matanki matatu ya maji yenye uwezo wa ujazo wa lita milioni 34 yaliyopo eneo la Kimara jijini Dar es slaam kutoka kwa Mhandisi wa Mradi huo P. G. Rajan (kulia) wakati wa alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mwishoni mwa wiki