Posts

Showing posts from April 1, 2016

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA GEREZA LA BANGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATUMISHI WA WIZARA MKOANI KIGOMA

Image
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akiongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo(kushoto) na Mkuu wa Gereza la Bangwe,SSP Raphael Mwanyingile(kulia), alipofika kutembelea gereza hilo katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma tarehe 31/3/2016. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisaini kitabu cha wageni katika Gereza la Bangwe mkoani Kigoma, ambapo baadae alisikiliza risala iliyohusu  mambo mbalimbali,  iliyoandaliwa na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo na kuahidi kushughulika changamoto zao. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo, akisoma taarifa ya hali ya magereza mkoani Kigoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Mmoja wa Askari Magereza mkoa wa Kigoma, akizungumza wakati wa kipindi cha maswali kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch

Tuhuma za Rushwa: Mbunge Ndassa Naye Afikishwa Kortini

Image
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa. MBUNGE wa Sumve, Richard Ndassa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar, leo akituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi  milioni 30  akiwa kwenye Kamati za Bunge. Ndasaa  anakuwa  mbunge  wa  nne  wa  CCM kupandishwa  mahakamani  kwa  tuhuma  za  rushwa  baada  jana wabunge Mh.Kangi Lugola wa jimbo la Mwibala, Mh.Sadiq Murad wa jimbo la Mvomero na Mh.Victor Mwambalaswa wa jimbo la Lupa kupandishwa  mahakamani kwa tuhuma za kuomba rushwa ya milioni 30 toka kwa mkurugenzi wa Wilaya ya Gairo  ili taarifa yake ipitishwe bila kujadiliwa.

SERIKALI KUPITIA UPYA MIKATABA YA TRL

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza mmoja wa abiria anayetumia usafiri wa reli ya kati mkoani Kigoma. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Saveli Maketta. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mkoani Kigoma. Muonekano wa mabehewa ya treni yakiwa mwisho wa reli ya kati, mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kapteni wa Meli ya MV Liemba ya namna inavyoendeshwa, mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akipata ufafanuzi wa namna ya injini za Meli ya MV Liemba zinavyofanya kazi wakati alipotembelea Meli hiyo mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye kizibao cha njano), akimsikiliza Kapt

Wifi wa Zari adaiwa kutimuliwa kwa Diamond

Image
Wifi nambari moja wa Zarinah Hassan ‘Zari’, Esma Platnumz. Stori:  Musa Mateja,  Ijumaa Hivi karibuni yalitua madai kwenye meza ya gazeti hili yakieleza kuwa, eti yule wifi nambari moja wa Zarinah Hassan ‘Zari’ anayefahamika kwa jina la Esma Platnumz (pichani) ametimuliwa pale nyumbani kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Madale jijini Dar na sasa anaishi Tandale. Chanzo chetu ambacho kiliomba jina lake lisiandikwe gazetini kilidai kuwa, baada ya Zari kutua Bongo kabla ya kwenda Ulaya, Esma alitakiwa kufungasha kila kilicho chake na kwenda kuishi kwenye ile nyumba ya familia iliyokuwa ikikarabatiwa pale Tandale. Diamond akiwa na waubani wake, Zari. “Nyie mbona mnapitwa na ubuyu? Esma katimuliwa pale kwa Diamond, sasa hivi anaishi kule Tandale kisa ni zile figisufigisu zilizokuwa zikitokea kati yake na Zari. “Diamond ameona ili mzazi mwenzake awe na amani, anayeweza kuondolewa kwenye ule mjengo aondolewe ili amani itawale na kusiwepo manenomaneno,” kilidai chanzo