Posts

Showing posts from September 25, 2016

Diamond Na Zari Waendeleza Bata Zanzibar

Image
Diamond. Diamond na mpenzi wake Zari. Kutoka kushoto Moses Iyobo, Aunt Ezekiel, Diamond na Zari. Mwanamuziki Diamond akiwa katika mapozi tofauti  na mchumba wake Zari na baadhi ya marafiki zao. Mwanamuziki Nassib Abdul amedhihirisha ule usemi wa wahenga wa zamani kwamba pesa maua na ukiwa nazo unaweza kufanya jambo lolote lile. Baada ya kumfanyia sherehe ya kuzaliwa mchumba wake Zari, aliyezaa naye mtoto mmoja na ambaye ni mjamzito kwa sasa wawili hao bado wapo visiwani Zanzibar wakiendelea kula bata hata baada ya kumaliza kwa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Zari zilizofanyika visiwani humo . Na Leonard Msigwa/GPL.

Msimamo wa CUF kuhusu uamuzi wa Jaji Mutungi kuamua kuwa Prof. Lipumba bado ni Mwenyekiti

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kimepokea kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kile kinachoitwa “Msimamo na Ushauri wa Vyama vya Siasa kuhusu Mgogoro wa Uongozi wa Kitaifa wa Chama cha Civic United Front (CUF)” ambao uliwasilishwa Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, jana usiku.   Baada ya kupokea Ushauri huo, The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kinapenda kueleza yafuatayo:   1. Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act, No. 5 of 1992) haimpi mamlaka wala uwezo wowote Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa ushauri, msimamo au mwongozo kwa vyama vya siasa kuhusiana na maamuzi ya vikao vya Chama.   2. Msimamo huo wa kisheria wa nchi hii umetiliwa nguvu na kuthibitishwa na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UAMUZI wa tarehe 9/5/2005 wa Jaji T.B. Mihayo katika kesi ya Emmanuel Nyenyemela na Magnus Msambila v/s Registrar of Political Parties & Others (Civil Case No. 6 of

Hoja 11 Zilizomrudisha Lipumba CUF

Image
Profesa Lipumba akiwa na Maalim Seif kabla ya hajajiuzulu kama mwenyekiti wa CUF. DAR ES SAALAM: Hoja 11 zilizotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, zimetosha kumrejesha katika wadhifa wake, Mwenyekiti ‘aliyejiuzulu’ wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba. Mbali ya Lipumba viongozi wengine ambao msimamo wa Msajili unawarejesha madarakani moja kwa moja baada ya kusimamishwa na Baraza Kuu la Uongozi la CUF, katika kikao chake cha Agosti 30, mwaka huu kilichofanyika jijini Dar es Salaam ni Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua na Naibu Mkurugenzi wa Habari Taifa, Abdul Kambaya. Wengine ni Mbunge wa Mtwara, Maftaha Nachuma, wajumbe wa Baraza Kuu Taifa, Masudi Omari Mhina, Thomas Malima, Ashura Mustafa na Kapasha Kapasha. Pia Musa Haji Kombo, Habibu Mnyaa na Haroub Shamis ambao wataendelea kuhesabika kama wanachama halali wa chama hicho. Katika barua yake kwa viongozi wa CUF, Msajili ali

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI KUADHIMISHA SIKU YA BWANA YA 19 BAADA YA PENTEKOSTE KANISA LA MTAKATIFU ALBANO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.   Waumini wakipokea baraka katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam wakati wa Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Mpiga kinanda Bw. Charles Mang'enya akielekeza wimbo kwa waumini katika kanisa la Anglikana l