Rais Zuma apewa siku 105 kurejesha fedha za umma alizotumia kukarabati makazi yake

Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika ya Kusini imemuamuru Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ndani ya siku105 awe amerejesha serikalini dola milioni 16 fedha za walipakodi ambazo alizitumia kukarabati makazi yake binafsi.

Mahakama hiyo imesema Rais Zuma mwenye umri wa miaka 73 alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kumtaka alipe fedha hizo zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi.

Jopo la Majaji 11 wa Mahakama hiyo ya Kikatiba ya nchini Afrika ya Kusini limesema Rais Zuma alikiuka Katiba ya nchi hiyo kwa kutumia fedha hizo katika ukarabati wa nyumba yake hiyo ambayo ipo eneo la nkandla -kwazulu-natal na kuhitimisha miaka 6 ya sakata hilo.

Chama cha siasa cha Democratic Alliance cha nchini humo  kimeanzisha kampeni ya kumuondoa Rais zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka Katiba.

Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimisha Rais Zuma kuzingatia matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kesi ambayo leo hii imetolewa hukumu

Comments

Popular posts from this blog