Posts

Showing posts from March 28, 2017

Watuhumiwa wa ugaidi waigomea mahakama

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imesikiliza malalamiko ya watuhumiwa 61 wanao kabiliwa na kosa la ugaidi, ambapo ni shauri lililofunguliwa mwaka 2014. Wakizungumza leo mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa leo ndiyo itakuwa mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa jamuhuri utakapo kamilisha upelelezi wao. Wamesema wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa makosa ya kusingiziwa. Aidha wamesema wamekuwa wakipewa ahadi  hewa na mkuu wa upelelezi  kuwa angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake  wa kikatiba linaleta ukakasi kwa wananchi. Hakimu Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa na subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11 mwaka huu na amewataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati akifanya utaratibu

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF PALAMAGAMBA KABUDI AWASILI OFISINI MJINI DODOMA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko alipowasili Wizarani mjini Dodoma WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.PalamagambaKabudiakisikilizamaelezombalimbalialipokutananawatendajiwaWizaranaMahakamakatikaukumbiwamikutanoWizaranimjini Dodoma. ……………….. WaziriwaKatibanaSheriaProf.PalamagambaKabudiamewasilikatikaOfisizaMakaomakuuyaWizarazilizokondaniya Chuo Kikuu cha Dodoma nakulakiwanawatumishiwaWiza

SAKATA LA RC PAUL MAKONDA KUVAMIA CLOUDS LAVUKA MIPAKA YA TANZANIA

Image
Asasi za kiraia 33 barani Afrika zimelaani kitendo cha kuvamiwa kwa studio za televisheni ya Clouds na kulazimisha maudhui yasiyostahili yarushwe hewani. Tamko la asasi hizo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, (THBUB), Jukwaa la Wahariri (TEF) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kulaani kitendo hicho kinachodaiwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Asasi hizo zinazohusika na utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa habari zilikutana hivi karibuni mjini Kampala nchini Uganda katika mkutano uliokuwa ukizungumzia uhuru wa kujieleza na kupata habari. Tanzania kwenye mkutano huo iliwakilishwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) , miongoni mwa mijadala iliyotawala ni kukemea vitisho na vitendo vya kunyanyasa waandishi. Pia, wajumbe katika mkutano huo waligusia mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais John Magufuli kwa kumtoa Nape Nnauye kwenye

NAPE AMKABIDHI RASMI OFISI WAZIRI MWAKYEMBE

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiwakaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma. Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitoa neno kwa Waziri mpya na Waziri aliyepita wakati wa makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma. Mhe. Nape Moses Nnauye aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akitoa shukurani zake kwa watendaji wa Wizara kwa muda wote aliotumikia Wizara katika makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe akimshukuru aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kwa kuitu