Posts

Showing posts from November 28, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA VIJANA WA UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM)

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya Mapambano dhidi ya Ukimwi na Katibu wa Hamasa na Chipukizi Taifa, Paul Makonda, wakati alipokutana na Vijana hao wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wenye lengo la kusambaza ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa UVCCM, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na OMR makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Vijana wa CCM, baada ya mazungumzo yao alipokutana nao jana kwa ajili ya kumkabidhi ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza

SHIJA ALIZWA NA THEA

Image
Na Gladness Mallya SIKU chache baada ya ndoa ya mwigizaji, Ndubagwe Mithayo ‘Thea’ kuvunjika, mwigizaji Deogratius Shija ‘Shija’ ameibuka na kueleza maumivu anayoyapata juu ya tukio hilo. Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ siku ya ndoa yao. Akizungumza na Amani hivi karibuni, Shija alisema taarifa za kuvunjika kwa ndoa ya Thea na Mike Sangu zilimuuma na kuwataka vijana wengi kuwa makini kabla ya kuoa na haswa kumshirikisha Mungu kila siku kwenye maombi ili ndoa zao zidumu. “Ndoa siyo maigizo. Ndoa ni mkataba mkubwa sana ambao wanaingia wanadamu hivyo inapovunjika huwa haileti picha nzuri kwa Mungu, binafsi inaniuma sana,” alisema Shija.

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA MTOTO WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM, PHILP MANGULA, PETER MANGULA, OYSTERBAY DAR JANA

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam,jana jioni kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Peter Mangula, aliyefariki juzi asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili. Peter anatarajia kuzikwa kesho Ijumaa jijini Dar es Salaam.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, marehemu Peter Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phili Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole.   Maka

BABA KANUMBA AKIMBIWA NA WANAWAKE

Image
Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa. Na Gladness Mallya BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda. Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini ajabu wote waliingia mitini. “Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba.

MTEMVU AFUNGUA NJIA KWA WATANZANIA NAFASI ZA AJIRA UGHAIBUNI

Image
 Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo Job Centre Agency (LTD)Abbas Mtemvu, Akifafanua jambo  Mbele ya waandishi na Wanao Safirishwa na Kampuni hiyo Mwishoni Mwa Wiki Dar es Salaam.    Baadhi ya wahudhuriaji wa tukio hilo  Mmoja wa Wasafiri hao Shamimu Mwarufai  Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD)  Mmoja wa Wasafiri hao Fatuma Chambo  Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD)   Dominica Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) kwa niaba ya Tabu Khalfani  Lita  Dominik Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) kwa niaba ya Tabu Khalfani mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.  Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agnc

ONA MAUNO KATIKA WIMBO WA SNURA "NIMEVURUGWA"

NORA AWANANGA RAY NA JOHARI

Image
Musa Mateja na Gladness Mallya BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao. Nuru Nassoro ‘Nora’. Akizungumza na mapaparazi wetu hivi karibuni, Nora alisema Ray na Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni. Johari. “Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini Mungu analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu, wakanipoteza kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua sitapona, lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama pete na kidole. “Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi

Wema Sepetu ajuta kutumia mikorogo, aanza kuitamani ngozi yake ya awali

Image
Wema Sepetu ambaye ni Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu anajuta kutumia mkorogo na hatimaye kupoteza urembo wake wa asili aliokuwa nao mwanzo kabla ya kuanza kujichubua.    Chanzo kimoja makini ambacho kipo karibu na Wema na ambacho pia ni star wa filamu kimetutonya kuwa Wema anajuta kujichubua na hajiamini tena katika urembo tofauti na miaka ya nyuma kwani kila mtu sasa hivi anajua Wema ni fake na amejaa urembo wa kichina kwa aslimia kubwa.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA MAOMBOLEZO KUFAUTIA MSIBA WA MZOBORA

Image
Marehemu  Dunia Mzobora enzi za uhai wake. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kufuatia kifo cha Mwandishi wa Habari na Msanifu wa Habari Msaidizi Mkuu wa Gazeti la Uhuru, Bwana Dunia Mzobora, kilichotokea tarehe 27 Novemba, 2013 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya shinikizo la damu. Marehemu aliajiriwa katika Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mwaka 1989 kama Mwandishi wa Habari Mwanafunzi, kisha akaendelea kupanda ngazi hadi kufikia cheo cha Msanifu wa Habari na hatimaye kuwa Msanifu Mkuu Msaidizi, cheo alichokuwa akikishikilia hadi mauti yalipomkuta. “Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha mmoja wa Waandishi wa Habari Shupavu na Mchapakazi, Dunia Mzobora aliyekuwa akilitumikia Gazeti la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la UHURU, kilichosa

SIRI 5 ZA WOLPER ZAVUJA .... HIZI HAPA ALIVYOZIANIKA

Image
MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili. Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar. Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni,… Na Sifael Paul MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili. Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar. Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwen

MAN UNITED YAFANYA MAUAJI, YAWAPIGA WAJERUMANI 5-0 NYUMBANI KWAO

Image
wachezaji wa Manu wakishangilia moja ya magoli yao Wyne Rooney na Giggs wakifurahia ushindi Kagawa akikata mbuga kuelekea kutafuta goli MANCHESTER United imefanya mauaji makubwa ugenini, baada ya kuitandika Bayer Leverkursen mabao 5-0 nchini Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya. Mabao ya United usiku huu yamefungwa na Valencia dakika ya 22, Spahic aliyejifunga dakika ya 30, Evans dakika ya 65, Smalling dakika ya 77 na Nani dakika 88. Wayne Rooney ndiye alikuwa nyota wa mchezo kutoka na kupika mabao manne katika ushindi huo ambao haukutarajiwa. Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra/Buttner dk70, Jones, Giggs, Valencia/Young dk80, Kagawa, Nani na Rooney/Anderson dk80. Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Spahic, Omer Toprak, Can, Bender/Kohr dk81, Reinartz/Hegeler dk70, Rolfes, Castro, Son Heung-min/Derdiyok dk70 na Kiessli n big up
Image
MEZA YETU YA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 28.11.2013 MAGAZETI YA UDAKU LEO . MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI