Posts

Showing posts from July 5, 2022

Manara Amuangukia Rais Karia Akili Kukosea Kama Binadamu, Aomba Yaishe

Image
Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Sunday Manara MSEMAJI wa Yanga Haji Manara amemuomba msamaha Rais wa TFF Wallace Karia kutokana na tukio lililotokea Jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.   Mara baada ya mchezo huo kuna video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha Afisa huyo wa Yanga akijibizana au kutupiana maneno na Rais wa TFF Wallace Karia huku wengi wakitafsiri kuwa Manara alikuwa akimtukana Rais huyo.   Akiongea na waandishi wa habari Manara amenukuliwa akisema: “Rais nimekuja kwa kukujibu vile au kujibizana mimi na wewe nimekosea “I’m Sorry” mi ni mdogo wako mimi ni kama mwanao, No matter labda wewe ndiye uliyeanza lakini kukujibu tu hata kama ulinianza nimekosea, I’m Sorry My President of Football.” Alisema Manara Manara amemuomba msamaha Rais wa TFF Wallace Karia Aidha Manara ametumia nafasi hiyo kuwaomba radhi mashabiki na wapenzi wa soka nchini ambao wanaona kwa kujibu vile alikosea akisema yeye ingawa amekaa kw