Posts

Showing posts from July 12, 2013

HIKI NDO KIASI CHA PESA ANACHO INGIZA RAISI OBAMA KWA MWAKA

BAADA ya kuchaguliwa katika awamu ya pili ya utawala wa Marekani, Rais Barack Obama, ameendelea kupata mshahara wa dola 400,000 kwa mwaka. Wakati alipopata utawala, Rais huyo mwenye nguvu duniani ameendelea kuwa Kamanda wa Jeshi la Marekani, Rais mwenye nguvu duniani na ameendeleza utawala wa Air Force One. Obama alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza, kipato chake kilikuwa dola 1.3 milioni. Miaka minne baada ya kukaa Ikulu kipato chake kimeongezeka kwa asilimia 800 sasa anapata dola 11.8 milioni. Kipato kimeongezeka vipi? Awali Obama alikuwa na kipato kidogo, alikuwa akilipwa dola 60,000 kwa mwaka alipokuwa Seneta wa Illinois na baadaye akawa analipwa dola 175,000 kwa mwaka. Jambo la kufurahisha ni kuwa kabla Obama hajawa Rais, hakuwa na mshahara mkubwa, hata mke wake, Michelle,  alimzidi kwa kipato. Michelle alikuwa akiingiza kiasi cha dola 320,000 kwa mwaka, wakati huo alikuwa Makamu wa Rais wa Kitengo cha Ushir

MAANDAMANO MAKUBWA TOKA MISRI YAFANYIKA LEO

Image
Wafuasi na wapinzani wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi Wanafanya maandamano makubwa mjini Cairo mchana huu, huku waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimisha Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadan. Wafuasi wa Bwana Morsi wanatarajia kuwa mamilioni ya raia wa nchi hiyo, wataendelea kuunga mkono wito wao wa kutaka Bwana Morsi kurejeshwa madarakani. Wapinzani wa rais huyo wa zamani ambao waliandamana hadi rais huyo akaondolewa madarakani na jeshi watakusanyika katika medani ya Tahrir. Watu kadhaa wameuawa kwenye ghasia zilizotokea tangu Morsi alipoondolewa. Mwandishi wa BBC mjini Cairo, Jim Muir anasema vuguvugu la Muslim Brotherhood huenda liliwatenga raia wengi wakati wa utawala wa Morsi, lakini bado raia wengi wa nchi hiyo hawataki jeshi kuingilia masuala ya siasa. Marekani kutuma ndege za kivita Misri Siku ya Alhamisi serikali ya Marekani, ilitoa wito kwa utawala mpya wa Misri, kusitisha harakati zake za kuw

MAISHA BORA KWA MTANZANIA JE YANAKIDHI.......

Image
Hawa ni vijana kutoka MKOANI - MANYARA maeneo ya HARKA waliokutwa wakijadilini ni kwa jinsi gani wapataweza kupata unga angalau hata robo kilo ili wakapike kupunguza ukali wa njaa mara baada yakupata mboga mafungu mawili ya mboga za majani,na hatimaye msamaria mmoja kuhamua kuwanunulia mua ili wapunguze njaa zao. Ukiwa kama Mtanzania Mwenzetu je ungewasaidiaje hawa vijana. TUPE MAONI YAKO

HUYU ndo MWANAJESHI ALIYEKAMATWA NA JINO LA TEMBO ANGALIA PICHA

Image
Mwanajeshi anayesadikiwa kukutwa na jino la Tembo akiwa chini ya ulinzi pamoja na kidhibiti chake, huyu alitegemewa kuilinda Nchi lakini . (Picha na maktaba) Alitaka kuingia Malawi, apandishwa kizimbani OFISA Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Suleiman Chesana, anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni nne, amepandishwa tena kizimbani baada ya kukutwa na meno mengine ya tembo kilo 781 yenye thamani ya Sh bilioni 9.3. Mshtakiwa huyo, alipandishwa tena kizimbani jana kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, mbele mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kusomewa mashtaka na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka. Kweka alidai kosa la kwanza ni la kujishughulisha na nyara za Serikali bila kibali, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi. Ilidaiwa Mei 23, mwaka huu, katika mpaka wa Malawi na Tanzania, mtuhumiwa alikamatwa akisafirisha isivyo halali nyara zenye t

KILA SIKU KUNA JIPYA MZEE ASEMA ANATAKA KUMFUFUA NYERERE

Image
MAAJABU YA MBEYA HEBU SOMA HII KWA MAKINI KABISA.   Huyu mzee alifika katika studio za Kyela FM, anasema yeye anahitaji Msaada anataka kwenda kumfufua Mwl. Julius Kambarage Nyerere baba wa Taifa aliyefariki Miaka 15 iliyopita,Na huo ufunguo ameushika mkononi ndiyo wa kumfufulia! Madai yake mzee huyu anasema anaenda kumfufuana Mwalim ndiye atakuja kusimamia uchaguzi wa mwaka 2015.Na pia anaibashiria CCM kuwa mshindi atatoka katika chama cha CCM.

TANZANIA YAMJIBU RAIS KAGAME....YADAI IPO TAYARI KWA LOLOTE NA AKITHUBUTU ITAMCHAPA KAMA MTOTO

Image
SERIKALI ya T anzania imeipa onyo kali nchi ya Rwanda ikiitaka isijaribu kuota ndoto za kuishambulia kijeshi, vinginevyo itajibu mapigo kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa imeichakaza. Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania. Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame. Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30, nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana. Kwa mujibu wa hotuba hiyo, ambayo kwa wiki sasa imesa