Posts

Showing posts from February 21, 2018

MGUU WA MTOTO WANASA KWENYE NGAZI ZA UMEME AIRPORT

Image
Mtoto Julian ambaye mguu wake ulinaswa kwenye ngazi za umeme kwenye uwanja wa ndege wa Vancouver, Canada. Mama yake, Andrea Diaczok, ametoa wito kwa wazazi kuwa macho na watoto wao katika sehemu hizo. MTOTO Julian mwenye umri wa miaka miwili alijikuta akivunjwa mifupa ya mguu wake uliponasa kwenye ngazi za umeme katika kiwanja cha ndege cha Vancouver, Canada. Kiatu cha Julian kikiwa katika mashine za ngazi za umeme kilipokuwa kimenasa. Julian alikuwa na wazazi wake, Andrea Diaczok, mama yake,  na baba yake, Jeff Lee walikuwa wakirejea mjini Calgary wiki iliyopita kutokea Vancouver.  Mguu wa mtoto huyo ulikwama pembeni kati ya ngazi na vyuma vinavyozungusha mikanda inayopandisha abiria. Julian akiwa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu, kinyume na woga wa wazazi wake ambao walifikiri huenda mguu wake ungekatwa. “Mguu wake ulipotea kabisa kwenye mkanda unaozunguka,” Diaczok, alisema na kuongeza kwamba kuona hivyo alipiga kelele kwa nguvu. Wazazi wa Ju

Mtanzania Akamatwa na Dhahabu ya Bilioni 2, Nairobi

Image
MWANAMME mmoja anayedaiwa kuwa ni raia wa Tanzania amekamatwa na maofisa wa forodha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya, akisafirisha dhahabu ya thamani ya dola milioni moja (sawa na zaidi Tsh. Bilioni 2) taarifa zinasema. Mtu huyo mwenye umri wa miaka 46 anadaiwa kuingia Nairobi akitokea mkoani Mwanza, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) na alikuwa safarini kuelekea Dubai. Gazeti la Nation limesema mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halijajulikana hadi  sasa, aliwasili uwanja wa JKIA, Ijumaa, Februari 16 na  ndege ya Precisio Airlines akitaka kuunganisha na ndege ya Kenya Airways kuelekea Dubai kabla ya kukamatwa na kuhojiwa na Maofisa wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai nchini humo na wachunguzi kutoka Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA). Sheria za Usimamizi wa Forodha za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za mwaka 2004, Kifungu 85(3) na Kiambatisho cha Pili Sehemu B (4) huharamisha usafirishaji wa madini ambayo hayaja