Posts

Showing posts from May 8, 2016

LEICESTER CITY YAKABIDHIWA KOMBE LAO LA LIGI KUU ENGLAND

Image
 Leicester City wamesherekea ubingwa wao wa Premier League ambao ni wa kwanza katika historia ya klabu hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 132 iliyopita. Furaha hiyo imechagizwa na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa King Power. Leicester wamekabidhiwa rasmi ubingwa wao baada ya kujihakikishia kutwaa taji hilo tangu siku ya Jumatatu wakati Tottenham iliposhindwa kuifunga Chelsea. Klabu hiyo imeandika historia ambayo imeuteka ulimwengu ambapo nahodha Wes Morgan pamoja na kocha Claudia Ranieri kwa pamoja walinyanyua taji la Premier League baada ya kumaliza safari ya kupambana kutoshuka daraja hadi kutwaa ubingwa katika kipindi cha miezi 12. Ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton ulikuwa unaendelea kudhihirisha uwezo, kujitoa na ubora uliowapa ubingwa, lakini siku ya Jumamosi ya May 7 ni zaidi ya mchezo wa soka kutokana na kufunikwa na hisia za kila aina.

DUNIA INA MAMBO MAZITO BI HARUSI AMPA SUMU MUMEWE

Image
Msichana mdogo alieolewaBi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake. Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu. Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa. Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho. Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri. Msichana huyo wa miaka 7

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA BI LUCY KIBAKI

Image
 Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.  Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.  Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.