Posts

Showing posts from August 11, 2016

Kitwanga, JPM Wakutana Uso kwa Uso

Image
Rais John Magufuli jana alikutana ana kwa ana na rafiki yake, Charles Kitwanga ikiwa ni siku 80 baada ya kumvua cheo cha Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kosa la kuingia bungeni kujibu maswali akiwa amelewa. Wawili hao walikutana kwenye Jimbo la Misungwi ambako Rais alisimama akitokea Wilaya ya Sengerema ambako alihutubia wananchi. Rais alitengua uteuzi wa Kitwanga Mei 20, wakati sakata la utekelezwaji mbovu wa mkataba wa Sh37 bilioni baina ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises likivuma kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano. Lakini jana, hali ilionekana ya kikazi zaidi wakati Rais alipofika kwenye jimbo hilo. Kitwanga, ambaye ni mbunge wa Misungwi mkoani Mwanza, alitumia nafasi hiyo kukutana na Rais kwa mara ya kwanza hadharani, kuwasilisha kero za wananchi wake, hasa ya maji. Katika tukio hilo lililovutia hisia za waliokuwepo, Rais aliuthibitishia umma kuwa yeye na Kitwanga ni marafiki wa muda mrefu, alipokuwa akijibu ombi la mbunge huyo la kutaka Ser

Njemba Avamia Makao Makuu ya Trump, Apanda Ghorofa 21 kwa Saa 3

Image
Polisi wakijitahidi kumtoa njemba huyo aliyepanda juu ya ghorofa. Njemba huyo katika haakati za kukwea jengo hilo la ghoofa 58. Akikazana kukwea. Hali ilivyokuwa Mashuhuda wakitahauki. Polisi wakijitahidi kumdhibiti Akitolewa na polisi NEW YORK: Njemba mmoja nchini Marekani aliyejiita kuwa ni mtafiti binafsi na shabiki wa Donald Trump, jana Agosti 10, 2016 alitumia masaa matatu kupanda jengo la mfanyabiashara huyo maaufu duniani ambaye pia ni mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Republican lililopo jijini New York. Taarifa zimeeleza kuwa njemba huyo mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Virginia alitumia vifaa maalum kupanda ghorofa hilo lililojengwa kwa vioo ambalo pia ni Makao Makuu ya Kampeni za Bwana Trump na ndiyo Makao yake Makuu Kibiashaa kabla ya polisi kumtoa akiwa amefikia ghorofa ya 21 huku akiwa amechomwa vibaya na vioo vya jengo hilo. Trump anaishi kwenye ghorofa ya ya juu kabisa ya jengo hilo lakini kwa sasa an