Posts

Showing posts from July 1, 2014

MTOTO WA MIAKA 9 ATAKA KUWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA KUTUMIA NJIA NGUMU

Image
Mzazi wa mtoto Idda Baitwa,Bw Respcius Baitwa akifanya maandalizi na mwanae ya kuanza safari  ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro Mtoto Idda Baitwa akiwa na baba yake mzazi Bw Respcius Baitwa pamoja na ndugu zake wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza safari  ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro. Mtoto Idda Baitwa akijiandikisha katika lango la Umbwe la kupanda mlima Kilimanjaro kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima huo.nyuma yake ni Bw Respicius Baitwa akshuhudia. Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mtoto Idda Baitwa ikaanza. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini. MTOTO wa miaka tisa(9) Idda Baitwa ameanza safari  ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa na umri mdogo zaidi huku akitumia njia ya Umbwe ambayo inaaminika kuwa ngumu zaidi kwa watalii wakati wa kupanda mlima huo. Msichana huyo mwanafunzi wa darasa la nne, katika shule ya msingi Mnazi iliyoko Manispaa ya Mos

Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe za miaka 10 ya chuo cha JKT mapinga

Image
  Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa anakata utepe kuashiria uzinduzi rasimi wa uwanja  uliopewa jina la Jenerali Davisi Mwamunyange  ambao utatumika kwa shughuli mabalimbali ikiwemo gwaride kulia ni Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga na kushoto ni Mkuu wa chuo cha JKT Mapinga Meja Aristides Rutta sherehe hizo ziliambatana na kutimiza miaka kumi ya kuanzishwa kwa chuo cha JKT Mapinga  kilichopo jijini Dar es salaam  Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Devisi Mwamunyange akikagua gwaride h lililo andaliwa wakati wa sherehe za kutimiza miaka kumi ya kuanzishwa chuo cha jkt Mapinga kilichopo jijini Dar es salaam   Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali  Devisi Mwamunyange akiwa anangalia bwawa lakufugia samaki ambalo limejengwa na chuo cha jkt mapinga jenerali Mwamunyange alikuwa mgeni rasimi katika kuadhimisha miaka kumi ya kuanzishwa kwa chuo cha jkt mapinga  Jengo la utawala la  chuo cha JKT Mapinga  kilichopo jijini Dar es

ANGALIA PICHA SAFARI YA MWISHO YA MWANAFUNZI DANIEL LEMA ALIYECHOMWA MOTO KWA KUTUMIWA KUWA MWIZI

Image
Mwili wa Daniel Lema ukiagwa na baadhi ya wanachuo pamoja na raia waliojitokeza kuhudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu mapema asubuhi ya leo katika hospitali ya rufaa mkoani iringa. Mwanafunzi (LEMA) aliyejeruhiwa kwa moto   Baadhi ya raia walijitokeza kumuaga Lema katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa. LEMA Aliyekua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO), mwanzoni mwa wiki hii ameshambuliwa kwa kuunguzwa na moto akidhaniwa ni mwizi. Mnamo tarehe 24.06.2014 mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5 Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na binti ambaye alianza kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi. Na kwakua eneo

ANGALIA PICHA APIGWA NYUNDO YA KICHWA NA MKEWE

Image
Faustina Selali,akiwa katika maumivu makali baada ya kushambuliwa na mumewe. Inasikitisha sana jamani. Faustina Selali, 38, mkazi wa Mgeta, Mvomero mkoani hapa, yupo kwenye mateso makali akijiuguza kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina la Lugasiani John Miasiku, kisa kikiwa ni mumewe huyo kutaka kuoa mke wa pili. Mwanamke huyo amelazwa katika wodi nambi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ambapo amesimulia kisa chote mbele ya kamera ya Uwazi. KISA CHENYEWE Akizungumza kwa tabu, Faustina alisema tukio hilo lililobadilisha historia ya maisha yake na kumwachia machungu moyoni mwake, lilitokea Juni 25, mwaka huu majira ya saa nne usiku ndani ya nyumba yao. “Mimi na mume wangu tumeishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 20 na kufanikiwa kupata watoto watano. Kwa kipindi kirefu nilihisi ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, wakati naendelea kumchunguza, mume wangu akaniambia anataka kuoa mke wa pili,”