Posts

Showing posts from July 14, 2017

Diwani Chadema Mbaroni kwa Tuhuma za Rushwa

Image
Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa  Sh.5,000,000/=. kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa  TAKUKURU wilaya ya  Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa  na watuhumiwa kuwapa  rushwa ya Sh.10,000,000/= Inadawaiwa Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji  inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo. Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa kinyume na kifungu namba 15 ch

Majaliwa Amkalia kooni Mkurugenzi Lindi

Image
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Lindi, Samuel Warioba Gunzar leo alijikuta katika wakati mgumu mbele ya waziri mkuu wa Jamuhuri ya Tanzania, Kassim Majaliwa baada ya kukutana na maswali mzito mfululizo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa nchi.  Hayo yamejiri katika mji mdogo wa Mtama kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa umefurika mamia ya wananchi. Hali ilikuwa mbaya kwa Gunzar kutokana na taarifa iliyotolewa na mbuge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye aliyekueleza waziri mkuu kwamba katika mji huo mdogo in unaokadiriwa kuwa na wakazi takribani 4000 hauna kituo cha afya.  Maelezo ya Nape yalisababisha waziri mkuu amuite mkurugenzi huyo aeleze nikwanini eneo hilo lisiwe na kituo cha afya wakati linaidadi kubwa ya watu. Huku akihoji kwanini imekuwa hivyo wakati kuna madiwani na watendaji katika halmashauri hiyo.  Alisema sera ya afya ipo wazi nasifa za kuwa na zahanati, vituo vya afya na hospitali zinafahamika. "Mkurugenzi  njoo utueleze kwanini hap

Usher Raymond atembelea mbuga ya Serengeti

Image
Usher Raymond Msanii wa Marekani Usher Raymond yuko ziarani nchini Tanzania akitembelea eneo la uhifadhi wa wanyama pori la Serengti National Park. Bwana Raymond alichapisha baadhi ya picha akiwa na familia yake katika akaunti yake ya Twitter. Alielezea hali ilivyo katika eneo hilo kama ya kufurahisha . Ripoti za Usher Raymond kuzuru Tanzania zilisambaa kwa haraka nchini humo. Watu wengine maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Becham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho, mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin ni miongoni mwa wale waliozuri katika sehemu mbali mbali za kitalii nchini humo mwaka huu. Vivutio vya kitalii nchini Tanzania kama vile mbunga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Serengeti na mlima Kilimanjaro ni vivutio vinavyoongoza kwa utalii ambapo watu wengi maarufu wametembela.

ACACIA Yakubali Kulipa Mirabaha Iliyomo Kwenye Sheria Mpya Madini

Image
Balozi wa Canada nchini na Mwenyekti wa Barrick Gold Corporation (mmiliki mkubwa wa Acacia) Prof. Thornton wakiongea na waandishi wa habari Ikulu Dar. (Picha na Maktaba). Kampuni inayomiliki Makampuni ya Uchimbaji wa Madini ya ACACIA imesema italipa mirabaha iliowekwa katika sheria mpya za madini. Sheria mpya ya madini inawataka wawekezaji katka sekta hiyo kulipa asilimia 6 ya mirabaha ikiwa ni ongezeko la asilimia 2 zilizokuwepo awali, ambapo asilimia 1 ni kwaajili ya usafirishaji kwenda nje.

Umewaona mapacha wa Beyonce?

Image
Beyonce na mapacha wake. MWANAMUZIKI maarufu duniani, Beyonce Knowles kwa mara ya kwanza ameawaanika hadharani watoto wake mapacha ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya kujifungua. Alichokiandika Beyonce Januari akiwa na mimba. Muimbaji huyo kupitia mtandao wa Instagram, ameonyesha kuwa watoto hao wana mwezi mmoja tangu wamezaliwa. “Sir Carter and Rumi 1 month today. 🙏🏽❤️👨🏽👩🏽👧🏽👶🏾👶🏾,” ameandika Queen Bey kwenye mtandao huo. Mapacha hao waliozaliwa ni mmoja wa kike na mwingine wa kiume na tayari walishapewa majina ya Sir na Rumi.

Taiwan: Wabunge Wavurugana Bungeni, Wachapana Live

Image
Wabunge wakizichapa kavukavu. WABUNGE wa Taiwan leo walichapana makonde, wakarushiana viti na mabaluni ya maji baada ya kutofautiana kuhusu mradi mmoja wa miundombinu. Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio yaliyoanza jana ambapo katika kubishana, wabunge hao walikwidana mashati na kuchapana wakati wa kupitia bajeti ya mradi huo. Mpango huo ni moja ya miradi mikubwa iliyopendekezwa na Rais Tsai Ing-wen ambayo inajumuisha ujenzi wa reli za kutoa huduma ndogondogo, hatua za kuthibiti mafuriko na mazingira yanayosababishwa na viwanda. Hata hivyo, chama cha upinzani cha Kuomintang kinapinga mradi huo kikisema unapendelea miji na wilaya ambazo zinaunga mkono chama cha Democratic Progressive (DPP) ambako kina uhakika wa kuungwa mkono katika uchaguzi wa mikoa mwaka kesho. Isitoshe, wapinzani wanapinga kiasi kikubwa mno cha Dola bilioni 13.8 ambazo zitatumika katika mradi huo. Waziri Mkuu Lin Chuan alishindwa kutoa ripoti ya bajeti hiyo Alhamisi baada kutupiwa b

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MADAKTARI AFRIKA YA NCHINI MAREKANI WAFANYA MATIBABU YA MOYO KWA WAGONJWA KWA KUWEKA KIFAA MAALUM

Image
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) . Kushoto ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Moyo Mathew Sackett. Tangu kuanza kwa kambi hiyo mwanzoni wa juma hili jumla ya wagonjwa 20 wameshapatiwa matibabu kati ya hao nane wamewekewa Pacemaker na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.  Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini Marekani Mathew Sackett akizungumza na waandishi wa habari na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa ulioufanya katika matibabu ya Moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Ta

Hakuna aliyekamilika, Cha Muhimu ni Kuvumiliana

Image
UHALI gani msomaji wangu! Ni matumaini yangu kuwa uko poa kabisa. Ni ijumaa nyingine nzuri ninayokualika kwenye uwanja huu, kwa wewe ambaye mambo yako hayaendi sawa, nakuombea kwa Mungu akufanyie wepesi. Mada yetu ya leo ni kama inavyojieleza, wapo baadhi ya watu ambao wao kamwe hawakosei, kila tatizo linapotokea basi wanawasukumia mizigo wenzi wao, wanaamini wao ni wakamilifu ila wenzi wao ndiyo wana matatizo. Ipo wazi kwamba uhusiano wa kimapenzi ni jambo ambalo linatakiwa kuwa la furaha, wewe na mwenzi wako muishi kwa upendo na amani, hata kama kunatokea misuguano, basi inakuwa ni ile ya kawaida ambayo mnaimaliza mapema, kwa amani na maisha yanaendelea. Kwa bahati mbaya, uhusiano wa kimapenzi wa watu wengi siku hizi, umejawa na migogoro, maudhi na karaha za mara kwa mara, hasa kwa wale wapenzi wanaoishi kwenye uhusiano wa kudumu, uwe ni uchumba au ndoa. Jambo ambalo watu wengi huwa hawalijui, ni kwamba amani, upendo na maelewano huwa haviji tu, ni lazima vij