Posts

Showing posts from September 14, 2016

Wakurugenzi Manispaa, Miji Na Halmashuri Waapishwa Dodoma

Image
Baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya wakila kiapo wakati  kukabidhiwa majukumu yao katika ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma Septemba 13. Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Umma Ofisi ya Kanda ya kati Dodoma, Cathlex Makwaia (kulia) akiwaapisha wakurugenzi 13 wa manispaa, miji na na halmasahuri mjini Dodoma. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bernard Makali.  Wakurugenzi wakiendelea kula kiapo. …Wakitia saini viapo vyao. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, akiwapa mawaidha na ushauri wa kiutendaji wakurugenzi baada ya kuapa. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, akiwapa mawaidha wakurugenzi. Waziri Kairuki akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu, Hudson Kamoga. Waziri wa Nchi, Ofisi ya

Simbachawene Awapa Somo Wakurugenzi Wapya

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Boniface Taguluvala Simbachawene amewapa somo wakurugenzi wapya walioteuliwa hivi karibu na kuapishwa jana mjini Dodoma. Waziri huyo amewataka wakurugenzi hao kuacha kufanya na mitandao ya kijamii kwa kuwa imekuwa ikitoa taarifa ambazo siyo sahihi. Kauli hiyo aliitoa jana mjini humo alipokuwa akizungumza na wakurugenzi hao baada ya kuapishwa. Alisema:  “Msifanye kazi na mitandao ya  jamii kwa sababu  mingi ni ya uzushi na imekuwa ikidanganya watu, siyo kila unachokiona unakiweka katika mtandao. Waziri huyo alitoa mfano wa taarifa iliyotolewa katika mitandao ya  jamii hivi karibuni kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi  imeanza kuwaruhusu waombaji wa ajira za ualimu kuanza kutumia mfumo wa maombi ya ajira za ualimu(On line Teachers Employment Application System-OTEAS) kuwa siyo za kweli. “Imetuletea shida kubwa, inawaumiz,a unakuta mtu ametoka kijijini ametumia zaidi ya Sh 100,000  k

Wanafunzi Wadaiwa Kuwacharaza Viboko Walimu Wao

Image
Wanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele Mkoa wa Katavi, wanadaiwa kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wao wawili miongoni mwao akiwemo Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Makonda Ng’oka “Membele’‘ (34) ambaye ameng’olewa meno matano kwa kipigo hicho. Walimu hao wawili wamedai kuwa hawako tayari kuendelea kufundisha katika shule hiyo huku wakisisitiza kuwa ni fedheha kwao kucharazwa viboko na wanafunzi wao wenyewe ambapo Mwalimu Gabriel Kambona aliachwa na ngeu kichwani. Mei mwaka huu, Ng’oka “Membele” alifikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake akidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Novemba 2015 na Aprili mwaka huu. Ilisemekana kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kulifuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano sasa wako Kidato cha Sita katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake. Wanafunzi ha

RUBY AKANUSHA KUWA NA TATTO YA FREEMASON

Image
Ruby alikanusha kuwa katika imani hiyo na kusema kila kuwa mtu ana jicho na hana maana ya kuwa kwenye imani hiyo ya Freemason bali yeye ni Mkristo na anamuamini Mungu. “Hakuna binadamu bila macho, na mimi ni mkristo namuamini Mungu so sijawahi kuingia kwenye Freemason so hizo ni imani za watu na hiyo tattoo sijachora kwa ajili ya Freemason.” Amesema Ruby. Pia kuhusu uongozi Ruby ameweka wazi kuwa kwa sasa anajisimamia yeye mwenyewe, “Nimeamua kubadili uongozi na sasa najisimamia mwenyewe kwa ajili ya mashabiki wangu”.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 14.06.2016

Image
Posted by JAFE MALIBENEKE at Wednesday, September 14, 2016 Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU ASHIRIKI SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS WA ZAMBIA EDGAR LUNGU

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akipungia mkono maelfu ya wananchi waliokuwa wakimshingilia wakati akiingia kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016  Rais Robert Mugabe akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt Kenneth Kaunda Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama baada ya kuwasili