Posts

Showing posts from June 5, 2014

NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

Image
 Nyoka aina ya chatu aliyetolewa nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Joseph Magesse akivutwa na wananchi kuelekea kwenye kanisa katoliki la karsamatiki eneo la Sakina jijini Arusha ambapo aliuawa kwa kucharangwa na shoka na wananchi wenye hasina na imani hizo za kishirikina  ​​Kijana akiwa amembeba nyoka baada ya kucharangwa kwa mapanga akitoka naye nje ya uzio wa kanisa hilo ​​ umati wa watu waliofika kushudia tukio hilo  Nyumba yamfanyabishara ambapo alikutwa nyoka huyo na chini ni sehemu ya magari ya mfanyabiashra huyo Kitambaa chenye maandishi ya kiarabu alichokutwa nacho nyoka huyokikiwa mbele ya geti la nyumba ya mfanyabiashara huyo

208 wafariki kutokana na Ebola Guinea

Image
Maafisa wa afya wakiwazika waathiriwa wa homa ya Ebola Maafisa wa afya duniani wanaarifu kuwa watu wasiopungua 208 wameaga dunia kutokana na virusi vya Ebola nchini Guinea baada ya ugonjwa huo kusambaa kwa siku za hivi karibuni. Angaa watu 21 waliaga dunia na visa vingine 37 vinavyohusiana na Ebola kuripotiwa kati ya tarehe 29 mwezi Mei na tarehe 1 mwezi Juni na kufikisha idadi ya visa hivyo kufikia 328 katika taifa hilo lililoko magharibi mwa Afrika. Hadi sasa, hakuna dawa za kuzuia wala kutibu Ebola- moja kati ya virusi hatari sana duniani.Kati ya visa hivi, 193 vilithibitishwa kupitia vipimo vya maabara. Zaidi ya nusu ya vifo vya hivi karibuni vilitokea kusini mwa eneo la Guekedou, mahali ambapo ugonjwa huo ulianzia. Visa vitatu vimedhibitishwa na vingine 10 vinavyodhaniwa kuwa wa ugonjwa huo vimeripotiwa katika nchi Jirani ya Sierra Leone. Mgonjwa wa Ebola akipokea matibabu Inaaminika kuwa watu kumi wameaga dunia katika taifa hilo, huku wen

G7 watishia kuiwekea Urusi vikwazo zaidi

Image
Mkutano wa G7 Viongozi wa mataifa tajiri ya magharibi wanaokutana mjini Brussels wamesema kuwa wako tayari kuweka vikwazo zaidi kwa Urusi iwapo itaendelea kuvuruga amani mashariki mwa Ukrain. Taarifa ya pamoja ya mataifa ya G7 imesema kuwa Mambo yanayofanywa na Urusi nchini Ukrain hayawezi kukubalika kamwe na lazima yakomeshwe. Huu ndio mkutano wa kwanza wa viongozi hao tangu waifukuze Urusi kama mwanachama. Urusi ilibumburushwa kutoka G7 kwa kosa lake kubwa zaidi, kuinyakua Crimea kutoka Ukraine. Viongozi wa mataifa hayo ya G7 wanakutana sasa kwa mara ya kwanza tangu wakati huo. Lakini huku wakikutana mapigano yamechacha kati ya serikali ya Ukrain na majeshi yanayounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine. Urusi imeendelea kukana kuhusika na mapigano hayo. Ukraine vita vimechacha Miongoni mwa mikutano iliyopangwa Alhamisi hii, waziri mkuu wa Uingereza Davin Cameron atakutana na rais Obama mjini Brussels, ambapo kwa upana zaidi wata

ZSTC yastawisha upya zao la karafuu, Zanzibar.

Image
 Zanzibar ni visiwa vinavyosifika kwa uzalishaji wa karafuu bora duniani. Katika miaka 30 ya nyuma pia ilisifika kwa uzalishaji karafuu nyingi, wastani wa tani 8,605 zilikuwa zikizalishwa kwa mwaka. Jamii ya wakati huo walikuwa wakizijali, wakizithamini na wakizipenda sana karafuu ukilinganisha na kizazi cha sasa. Walihakikisha karafuu zao wakiuza vituoni tena zinakuwa safi, zimekauka vizuri na zinapata daraja la kwanza. Katika miaka hiyo zao la karafuu lilikuwa ndiyo tegemeo kubwa la pato la kiuchumi katika visiwa vya Zanzibar.  Pato la Serikali lilitegemea sana zao hilo na kuiwezesha kuenedesha mipango yake ya kiuchumi na kijamii bila ya kuyumba. Hali hiyo ilitokana na ukubwa wa soko la dunia na ubora wa kipekee wa karafuu za Zanzibar katika soko hilo. Lakini kwenye miaka ya 1990, hali ya soko haikuwa nzuri sambamba na kushuga kwa bei na kuongezeka kwa nchi zinazozalisha karafuu duniani na hivyo kuleta ushindani wa kibiashara. Kushuka kwa bei

JE,SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA NI ZIPI?

Image
HABARI za leo wasomaji wangu? Kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mungu kwani ameniwezesha kufika siku hii.Mada leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke  akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba. Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba na kutupa watoto  na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa  zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa. Mimba nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga asipate. Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu ambayo: Mzunguko mfupi wa siku 25 kurudi nyuma, mzunguko wa kawaida wa siku 28 na mzunguko mrefu wa siku30-35. Wanawake wengi mzunguko wao  huwa  ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo nitawaongelea zaidi. Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza kuona damu ya he

Kuonyesha Ni Jinsi Gani Diamond Platnumz Anavyoipeperusha Bendera Ya TZ, Huu Ndiyo Mchango Wa Fast Jet Kwa Diamond Na Crew Yake Nzima

Image
Diamond, Wema na Aunty Ezekiel safarini South Africa kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards Kupitia Instagram yake Diamond ameandika: "Asante sana  @fastjetofficial  kwa kunisafirisha mimi, Familia yangu na team yangu nzima kuelekea kwenye Tuzo za MTV Awards Nchini South Africa.. hakika nyinyi ni Mfano Bora.. Kama Hauna Taarifa bado, Kampuni ya Fast jest sasa imeanzisha huduma mpya ya kutoka Tanzania hadi South Africa... credit:swahilitz

RAIS JAKAYA KIKWETE ALIVYOKUTANA NA WATANZANIA CANADA

Image
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea na viongozi wa Jumiya za Kitanzania zilizopo Toronto, Canada siku ya Ijumaa May 30, 2014. Rais Dkt Jakaya Kikwete alikuwa Canada wiki iliyopita kuhudhuria kikao cha “Improving the Lives of Women and Children: Maternal, Newborn and Child Health “ Viongozi wa ZANCANA walipata fulsa ya kumweleza Mheshimiwa Rais Jumuiya yao inavyojitahidi kusaidia nyumbani Tanzania katika sekta mbalimbali hususan ikijikita kwenye elimu na mahospatalini kwa kupeleka misaada mbalimbali mashuleni na kwenye Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Viongozi wa Jumuiya mbalimbali za Watanzania Toronto, Canada wakimsikiliza Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipokuwa akiongea nao siku ya Ijumaa  May 30, 2014., Makamu wa Rais wa ZANCANA Jamal Jiddawy katika picha yaa pamoja na Rais Dkt. Jakaya Kikwete Executive Manger Bishara na Boardmember Zamil ZANCANA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Dkt Jakaya Kikwete Kwa hisani ya Vijimambo Blog

KIFO CHA TYSON NI ZAIDI YA MSIBA KENYA

Image
Majonzi na simanzi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwongoza filamu za Kibongo, marehemu George Otieno Okumu ‘Tyson’ katika   Viwanja vya Leaders. WAKATI jana jiji la Dar likizizima kwa vilio, majonzi na simanzi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwongoza filamu za Kibongo, marehemu George Otieno Okumu ‘Tyson’ nchini kwao Kenya ni zaidi ya msiba. Tyson aliagwa na mastaa, mashabiki na wadau wa burudani Bongo kwenye Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar kabla ya mwili wake kusafirishwa kwa ndege kwenda Kenya kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Kisumu nchini humo keshokutwa Jumamosi. Mbali na Wabongo, pia kulikuwa na Wakenya ambao walitumia nafasi hiyo kumuaga mwenzao ambapo baadhi yao waliambatana na mwili huo kwenda Kenya. Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu ulipelekwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar tayari kwa safari ya Kenya. Sonia na Monalisa wakiwa na nyuso za huzuni wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Tyson. Kwa mujib

ABIRIA AFIA NDANI YA BASI MKOANI KILIMANJARO

Image
WATU wawili wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro katika matukio tofauti, likiwemo la mmoja aliyekutwa amekufa akiwa katika basi la Kampuni ya Kilenga akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Moita Koka, alisema kuwa mtu huyo ametambuliwa kwa jina la Sayuni Joel (53), mfanyabiashara, mkazi wa Mwembe, wilayani Same, Kilimanjaro. Akizungumzia mazingira ya tukio hilo, Kamanda Koka alisema Joel alipanda basi hilo T 398 BAT na kwamba kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa akisumbuliwa na tumbo na alikuwa akielekea hospitali kupata matibabu. Alisema Joel aligundulika kuwa amepoteza maisha baada ya gari hilo kuingia katika stendi kuu ya mabasi Moshi. Maiti yake imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho ukiendelea. Katika tukio jingine, mkazi wa Kijiji cha Kilema – Kiyou, Kata ya Kilema, wilayani Moshi, Martin Michael (45), amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya chandar