Posts

Showing posts from July 6, 2016

Oscar Pistorious asomewa hukumu kwa kosa la kumuua mpenzi wake

Image
Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius aliyekuwa nakabiliwa na shtaka la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp leo amesomewa hukumu ya kesi hiyo nchini Afrika Kusini. Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka 6 gerezani kwa kukutwa nahatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi. Pistorius alitenda kosa hilo Februari 13, 2013 ikiwa ni usiku wa kuamkia siku ya Valentine Day na inaelezwa alimpiga mpenzi wake risasi kwa madai alidhani ni mwizi aliyekuwa amejificha bafuni.

Aishi na risasi miaka nane

Image
Hassani Athumani akiugulia. Na Gregory Nyankaira, UWAZI MARA: Ama kweli kabla hujafa hujaumbwa! Kijana Hassani Athumani (30) mkazi wa Kiabakari, Kata ya Kukirango, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara anaishi na risasi mwilini kwa miaka nane sasa huku akiwa anasikia maumuvi makali na mwili wake ukiwa umejaa vidonda kutokana na kulala muda wote. Kijana huyo amepata masaibu hayo baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi Machi 6, 2008. Hassani Athumani akiwa na mama yake mzazi na mwanaye. Akisimulia juu ya tukio hilo Ijumaa ya wiki iliyopita nyumbani kwao akiwa amelala huku akitokwa na machozi kutokana na kudhoofika mwili wake kuanzia sehemu ya mgongo aliyopigwa risasi hadi miguuni, Hassani alikuwa na haya ya kusema: “Hiyo Machi sita mwaka 2008 tulikuwa tunacheza disko na wenzangu katika ukumbi mmoja uliopo Kiabakari, ghafla saa 4.30 usiku, majambazi yakiwa yamevalia makoti meusi na kufunika nyuso zao, yalivamia katika ukumbi huo n

NORWAY YATOA MSAADA KUSAIDIA WAHITIMU WAHANDISI WANAWAKE KUJIENDELEZA

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Profesa. Ninatubu Lema na Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad wakitia saini makubaliano ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 2 kwa ajili ya kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili. Programu inayoanza 2016 – 2021. Wanaoshuhudia utiwaji wa saini ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (nyuma kushoto). Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akizungumza wakati wa hafla fupi ya Kutiliana saini baina ya Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB) na Serikali ya Norway kuhusu msaada wa kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini ili waweze kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad na Mwenyekiti wa Bodi

MABADILIKO RATIBA YA MAZISHI YA MHE. BEATRICE SHELUKINDO - SASA KUFANYIKA KESHO NA SIO LEO HUKO OLOIRIEN JIJINI ARUSHA

Image
  Familia ya William H. Shelukindo inapenda kuwataarifu kuwa mazishi huko Arusha ya Mpendwa wao Beatrice Matumbo Shelukindo Mbunge wa zamani wa Kilindi sasa yatafanyika kesho siku ya Alhamisi tarehe 7/7/2016 na sio leo Jumatano tarehe 6/7/2016 kama ilivyotangazwa awali. Mazishi yatafanyika kesho saa tisa alasiri pale pale eneo la Oloirien jijini Arusha. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe. AMEN

Kisa kukataliwa kujiunga na ISIS, mapacha wamuua mama yao, wamjeruhi baba!

Image
MAPACHA wawili wamemuua mama yao mzazi na kuwajeruhi baba mzazi na kaka yao kwenye makazi yao yaliyopo Riyadh, Saudi Arabia baada ya kuzuiwa kujiunga na kundi lenye itikadi kali la wapiganaji wa ISIS. Mapacha Khaled na Saleh al-Oraini wenye umri wa miaka 20, wamemwua mama yao Haila aliyekuwa na umri wa miaka 67, walikamatwa na kushikiliwa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo wakati wakijaribu kutoroka kwenye mpaka wa Yemen. “Mbali na kumuua mama yao mzazi, pia walijaribu kumuua baba yao mzazi na kaka yao mkubwa ambao wamelazwa hospitalini kwa matibabu. Vilevile  wanahusishwa na mauaji yaliyofanyika June 24 mwaka huu ambapo nchini humo watu kadhaa walijeruhiwa na kuuwawa”. Alisema Msemaji wa Jeshi la Saudi Arabia, Mansour al-Turki.  

Waziri Mkuu aongoza Swala ya Eid El Fitr jijini Dar

Image
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akitoa mawaidha  mbele ya waumini wa kiislamu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu Majaliwa akiendelea kutoa mawaidha yake kwa waumini hao ambao hawapo pichani.            Mufti Mkuu wa Tanzania, Shekh Abubakar Zubery akitoa mawaidha yake mbele ya waumini wa kiislamu. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa akiongea na waumini wa dini hiyo na kuwatakia sikukuu njema waislamu wote nchini. Kutoka kushoto mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, Rais Mstaafu, Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa. Waumini wakiomba dua. Alhadi Mussa akihutubia waumini wa dini ya kiislamu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Taswira ya  baadhi ya waumini waliojitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja inavyoonekana. Sehemu ya waumini akinamama walijitokeza katika swala hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja. WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa mapema leo Jumatano, ameongoza

MREMBO ANASWA LIVE AKIFANYA BIASHARA YA NGONO NJE YA OFISI YA SERIKALI.

Image
Mrembo aliyekuwa akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za serikali akikurupuka mara baada ya kunaswa mtegoni. Njaa mbaya! Kama ulikuwa unadhani ile Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers imenywea, basi umenoa! Safari hii imenasa tukio la mrembo akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za serikali, Ijumaa Wikienda lina kitu laivu. Tukio hilo lisilo la kimaadili lilijiri usiku wa manane wikiendi iliyopita kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama, Dar. Baada ya kupokea kero kwa wakazi wazalendo wa eneo hilo kuwa ofisi yao inanajisiwa, OFM ilifanya uchunguzi wake wa kina na ilipojiridhisha ndipo ikaweka mtego. Kabla ya tukio ilisemekana kuwa pamoja na ngono kufanyika waziwazi na machangudoa waliopo maeneo mbalimbali ya Sinza na Kijitonyama, Dar, siku hizi wadada hao wafikia hatua mbaya zaidi kwa kufanyia maeneo yenye hadhi na sifa maalum kama viwanja vya shule za msingi, nje ya ofisi za watu, karibu na misikiti na makanisani. Timu ya OFM k