Posts

Showing posts from May 14, 2016

YANGA YAKABIDHIWA UBINGWA WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA

Image
Waziri na Kilimo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam baada ya mchezo dhidi ya Ndanda FC uliomalizika kwa sare ya 2-2 Wachezaji wa Yanga wakifurahia na Kombe lao jioni ya leo Uwanja wa Taifa

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KITUO CHA KISASA CHA HUDUMA ZA MAGARI MKOANI ARUSHA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Saddik alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Katikati Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Daud Felix Ntibenda. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi na Makamanda wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Vikundi vya Ngoma za aina mbalimbali alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza zi

Mkenya Adandia Helikopta na Kuning’inia, Apaa nayo Angani

Image
Mwanaume mmoja katika Mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya ameshangaza ulimwengu baada ya kudandia helikopta ambayo ilipaa angani na kuondoka naye jana. Helikopta hiyo ilikuwa imesafirisha mwili wa mfanyabiashara mashuhuri nchini humo, Jacob Juma aliyeuawa kwa kupigwa risasi na kufariki dunia jijini Nairobi wiki iliyopita, vyombo vya habari nchini Kenya vinasema. Mfanyabiashara Jacob Juma, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Erad  amekuwa akizua mjadala mitandaoni Kenya kutokana na ujumbe wake anaoandika hasa kwenye Twitter, aliuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi wiki iliyopita. Video zinazosambaa mitandaoni zinaonesha helikopta hiyo ikipaa juu angani kutoka uwanja wa Posta, mwanamume huyo akiwa amejishikilia kwenye vyuma vya helikopta hiyo. Taarifa zinasema baadaye ndege ilitua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Bungoma na mwanamume huyo kupelekwa hospitali. Wengi wameeleza kushangazwa kwao na tukio hilo la aina yake huku wengine baadhi ya Wak

Nadia Buhari ateswa na aibu

Image
Nadia Buhari Mrembo anayeuza nyago kwenye filamu za Ghallywood, Nadia Buhari amefunguka kuwa tabia yake ya aibu inamtesa sana kiasi kwamba watu wengi wamekuwa wakimchukulia tofauti kuwa anaringa na kujisikia jambo ambalo halina ukweli wowote. Nadia alisema; “Kiukweli aibu inanitesa. Ila watu wanatakiwa kuelewa kuwa nimezaliwa nikiwa na aibu na watu wasinichukulie tofauti, kila mtu anaasili yake.”
Image
Dili limekamilika: Jose Mourinho kusaini mkataba Manchester United ndani ya masaa machache Jose Mourinho anakaribia kutangazwa kuwa meneja mpya wa Manchester United kwa mujibu wa habari Mkongwe huyo wa miaka 53 amehusishwa sana na tetesi za kutua Old Trafford tangu alipotimuliwa Chelsea Desemba mwaka jana. Bosi wa sasa Louis van Gaal amewekwa kitimoto baada ya kushindwa kufanya vizuri katika kampeni za msimu huu, jambo ambalo limeifanya Manchester United ishindwe kutamba katika mbio za kuwania taji Ligi ya Uingereza. United kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, pointi mbili nyuma ya Manchester City inayoshika nafasi ya nne, na ni wazi kwamba wameshindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa. Hata hivyo watacheza dhidi ya Crystal Palace katika fainali ya Kombe la FA katika uwanja wa Wembley baadaye mwezi huu. Lakini inaonekana hata kama wakitwaa kombe la FA, bado mafanikio hayo hayatatosha kuokoa kibarua cha Mdachi huyo. Iliripotiwa kuwa Mourinho a

BLOGGERS WATINGA BUNGENI KWA MWALIKO WA WAZIRI NAPE

Image
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (aliyevaa tai) akiwa katika picha  ya pamoja na wamiliki wa Blogs  (Bloggers) aliowaalika wakati wa kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Annastazia  Wambura. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG  Baadhi ya Bloggers wakiwa bungeni wakati wa Bajeti ya wizara hiyo  Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' akisoma taarifa ya maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo.  Baadhi ya Bloggers wakisikiliza mwenendo wa bunge. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Wamiliki wa Bloggers Tanzania (TBN).  Nape akiwa na Bloggers pamoja na wasanii bungeni Dodoma  Nape akiwa na Bloggers  Nape akisalimiana na Blogger Salum Mwinyimkuu Mmiliki wa Blog ya Fullshangwe, John Bukuku (kushoto) na Mmiliki

Mrembo Anayedaiwa Kutembea na Diamond Kumbe Denti

Image
Mrembo anayedaiwa ‘kutembea’ na Diamond, Irene Hilaly  ‘Lynn’. Stori: Mayasa Mariwata, RISASI JUMAMOSI BINTI anayedaiwa kubanjuka kimalovee na staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’ anayejulikana kwa jina la Irene Hilaly  ‘Lynn’ kumbe ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msimbazi Centre aliyeacha masomo akiwa kidato cha tatu mwaka jana. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Irene anayeonekana katika video ya Wimbo Kwetu wa Raymond, anadaiwa kuwa na umri chini ya miaka 18, hajahudhuria shuleni tangu Machi mwaka jana na endapo angekuwa akienda, hivi sasa angekuwa kidato cha nne. “Kila kukicha walimu wanawatuma wanafunzi wenzake wamtafute Irene sababu hawajui pa kumpata, ili tu arudi shule aendelee na masomo kwa kuwa tangu alipofanya mtihani wa kidato cha pili akawa anakuja kwa kusuasua mwisho akakata mguu kabisa ‘form three’ mwanzoni,” kilisema chanzo hicho.   Staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’. Baada ya kuunyaka ubuyu huo pap