Posts

Showing posts from September 5, 2016

UHURU KENYATTA AKANUSHA KUWEPO MVUTANO WA KIUCHUMI KATI YA TANZANIA NA KENYA

Image
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumamosi alikanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba kuna mvutano baina ya Kenya na Tanzania. Akizungumza mjini Mombasa wakati wa ufunguzi gati la makontena katika bandari ya Mombasa, Kenyatta alipuuzia maneno kwamba kuna mvutano wowote na badala yake akasema kuwa nchi hizo zinasaidiana. Alisema anaona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna “mgogoro baina yetu, lakini nataka kusema wazi wazi kwamba Kenya na Tanzania hazina mgogoro wowote baina yao,” alisema.Kenyatta alisema uchumi wa nchi hizo mbili umefungana kwa miaka mingi na ni kwa ajili ya faida ya watu wa nchi hizo mbili. Alitaja kufunguliwa kwa njia inayojulikana kama “northern frontier” ambayo itaunganisha bandari ya Mombasa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania, hadi Bujumbura, Burundi – njia ambayo itafupisha urefu wa kutoka Bujumbura hadi Mombasa kwa kilomita 300 nzima. “Afrika Mashariki haiko katika mashindano ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kenyatta. “Afrika M

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 05.09.2016

Image

Polisi Wafyatua Risasi & Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa Lipumba

Image
  Jeshi la Polisi limelazimika kufyatua risasi angani na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba waliokuwa wakimzuia mwenyekiti wa muda wa CUF, Julius Mtatiro, kuingia ofisini eneo la Buguruni. Wafuasi hao wameeleza kuwa wameamua kumzuia kwani Msajili wa Vyama vya Siasa ametaka shughuli zozote ndani ya CUF zisiendelee hadi hapo mgogoro wa uongozi utakapotatuliwa. Itakumbukwa hivi karibuni CUF kilimteua Julius Sunday Mtatiro kuwa mwenyekiti wa muda baada ya mwenyekiti aliyekuwepo, Prof. Lipumba kijiuzulu Agosti 2015. Julius Mtatiro leo amefanya mkutano na waandishi wa habari  katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam ili kuzungumzia kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa visiwani Zanzibar.

WAZIRI MAHIGA AONGOZA TIMU YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC UCHAGUZI WA JAMHURI YA SHELISHELI

Image
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustino Mahiga akifungua Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016, Mahe Seychelles. Mhe Waziri anamuawakilisha Mhe. Rais John pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC. Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na  Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016 huko Mahe, Seychelles. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb.), jana tarehe 2 Septemba, amezindua Misheni ya Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC kwenye uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli kwa niaba ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika -SADC Organ.  Misheni hiyo ya wa