NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA GEREZA LA BANGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATUMISHI WA WIZARA MKOANI KIGOMA

22Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akiongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo(kushoto) na Mkuu wa Gereza la Bangwe,SSP Raphael Mwanyingile(kulia), alipofika kutembelea gereza hilo katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma tarehe 31/3/2016.
23Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisaini kitabu cha wageni katika Gereza la Bangwe mkoani Kigoma, ambapo baadae alisikiliza risala iliyohusu  mambo mbalimbali,  iliyoandaliwa na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo na kuahidi kushughulika changamoto zao.

24Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo, akisoma taarifa ya hali ya magereza mkoani Kigoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
25Mmoja wa Askari Magereza mkoa wa Kigoma, akizungumza wakati wa kipindi cha maswali kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani).Naibu Waziri alifanya mkutano na watumishi wa Idara zote zilizopo chini ya Wizara, mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF),mkoani Kigoma.
26Watumishi wa Idara zilizopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF), mjini Kigoma.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Comments

Popular posts from this blog