Posts

Showing posts from May 24, 2014

WANAHABARI KUMI, WAFANIKIWA KUINGIA FAINALI YA TUZO ZA HABARI ZA UTALII

Image
Frank Leonard alipopata fursa ya kuzungumza na wanahabari wa Arusha wakati wa ziara ya wanahabri wa Iringa jijini humo Jumla ya Waandishi wa Habari 10 wamefanikiwa kufikia hatua ya fainali ya Tuzo za Uandishi wa Habari za Shirika la Hifadhi za Taifa za mwaka 2013. Wanahabari waliofanikiwa kufika hatua ya fainali ni pamoja na Frank Leonard (Habari Leo), Jackson Kalindimya (Nipashe), Humphrey Mgonja (Radio SAUT FM), Raymond Nyamwihula (Star TV) na Vedasto Msungu (ITV). Wengine ni pamoja na Kakuru Msimu (Star TV), Gerald Kitabu (The Guardian), Salome Kitomari (Nipashe), David Rwenyagira (Radio 5) na Cassius Mdami (Channel Ten). Hafla ya utoaji Tuzo za Habari za TANAPA itafanyika siku ya Jumanne tarehe 27 Mei, 2014 jijini Mwanza ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu. Hafla hii itaenda pamoja na Mkutano wa kila mwaka baina ya TANAPA na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini inay

JK.ASHUHUDIA RAIS ZUMA AKILA KIAPO KUIONGOZA AFRIKA KUSINI KWA MARA NYINGINE.

Image
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Nelson Mandela Amphitheater katika jengo la Union Buildings mjini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini leo Mei 24, 2014   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Nelson Mandela Amphitheater katika jengo la Union Buildings mjini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini leo Mei 24, 2014 Rais Jacob Zuma akila kiapo katika Nelson Mandela Amphitheater katika jengo la Union Buildings mjini Pretoria wakati wa sherehe za kuapishwa kwake  leo Mei 24, 2014

HARUSI YA MBUNGE MAARUFU WA VITI MAALUM CCM VICKIE KAMATA YAAHIRISHWA LEO MARA BAADA YAKUUGUA GHAFLA NA KULAZWA

Image
Mbunge Vicky Kamata akiwa amelazwa Hospitali ya Tabata General, Dar es Salaam jana Dodoma/Dar es Salaam. Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.   Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni. Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.   Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo’ zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.  Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wa