Posts

Showing posts from November 10, 2015

UNYAMA Dar! Mke wa Mtu Atembezwa MTUPU, Apigwa Mawe na Kuchomwa Moto!

Image
Kundi la vijana hao wakimtembeza Shakila mitaani huku akiwa mtupu. Na Makongoro Oging’ DUNIA katili! Mrembo mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shakila Kocho (21), mkazi wa Tabata- Kimanga jijini Dar amelazwa Wadi namba 24, Jengo la Mwaisela, Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia majeraha yaliyotokana na kupigwa mawe na kuchomwa moto wa petroli kwa kisa cha tuhuma za kuwa kwenye mtandao wa wizi wa bodaboda. Wakimshambulia kwa mawe. WALIOTEKELEZA UKATILI Msichana huyo alifanyiwa kitendo hicho hivi karibuni maeneo ya Buguruni Sukita, Dar na watu wanaodaiwa kuwa ni madereva wa bodaboda ambao ndiyo waliomtuhumu. Taarifa zilizopatikana kwa mashuhuda zinadai kwamba, Shakila kabla ya kuchomwa moto alitembezwa mtupu mtaani huku watu wakimsonga na baadaye akapigwa mawe na fimbo halafu akamiminiwa petroli na kulipuliwa kwa kiberiti. Shakila akiwa ameanguka. MSOMALI ASAIDIA Kwa mujibu wa mashuhuda hao, wakati Shakila akiwa chini kutetea roho yake huku akiungua moto, mwanaum

SITTA:NINA SIFA ZOTE KUONGOZA BUNGE LIJALO

Image
Dar es Salaam. Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Samuel Sitta amesema kutokana na hali ya joto la kisiasa ilivyo, ambayo ilidhihirika zaidi wakati wa uchaguzi, wabunge walioshinda wengi ni vijana na ni wazi spika anayehitajika ni mwenye uzoefu. Sitta ameyasema hayo leo wakati akihojiwa na Radio Uhuru FM, ambako amethibisisha kwamba naye anakusudia kugombea nafasi hiyo ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa anaamini anazo sifa zote zinazohitajika.

TAARIFA KUTOKA JIMBO LA LUDEWA MAPYA KUHUSU MRIDHI WA DEO FILIKUNJOMBE

Image
Makada 10 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu wanatarajiwa kupigiwa kura na wanachama wa CCM ili kumpata mgombea atakayepambana na wagombea wa vyama vya upinzani. By Joyce Joliga, Mwananchi Ludewa. Wanachama wa CCM katika Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, leo wanapiga kura za maoni ili kumpata mgombea ubunge kupitia chama hicho atakayeziba pengo lililoachwa na Deo Filikunjombe aliyefariki dunia Oktoba 15, mwaka huu. Makada 10 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu wanatarajiwa kupigiwa kura na wanachama wa CCM ili kumpata mgombea atakayepambana na wagombea wa vyama vya upinzani. Makada hao ni Philip Filikunjombe (mdogo wa Deo Filikunjombe), Edgar Lugome, Johnson Mgimba, Emmanuel Mgaya, James Mgaya, Jackob Mpangala, Simon Ngatunga, Evaristo Mtitu, Deo Ngalawa na Zephania Chaula. Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Ludewa mjini, Tafuteni Mwasonya alisema kuwa tayari Mungu ame

WAZIRI MKUU MPYA WA SERIKALI YA WAMU YA TANO NI HUYU

Image
Fumbo kuhusiana na mtu mwenye sifa za kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli limeanza kufumbuliwa. Hali hiyo inatokana na kile alichokidhihirisha Magufuli siku moja baada ya kuapishwa kwake na pia baada ya hapo wakati alipochukua maamuzi kadhaa ya vitendo, ikiwamo kutoa maelekezo muhimu yaliyodhihirisha aina ya Waziri Mkuu atakayemteua. Kwa mujibu wa muundo wa serikali, Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, ambaye mbali ya kuwa kinara wa mawaziri wengine, ndiye anayetakiwa pia kutoa maamuzi mazito linapojitokeza jambo linalomlazimu kufanya hivyo. Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya siasa na uongozi nchini wamesema hatua alizochukua Magufuli kuanzia siku ya kwanza ya kuapishwa kwake zinatoa picha ya wazi aina ya watu atakaotaka kuwa nao katika serikali yake. Baada ya kuapishwa Novemba 5, 2015, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Dk. Magufuli alianza kazi siku hiyo hiyo kwa kuto

Maagizo 11 ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa Wizara ya Afya, Ikiwemo ya Maduka ya Dawa Binafsi Yaliyoko Maeneo ya Hospitali za Serekali Kuondolewa

Image

MAGAZETI YALEO JUMANNE.

Image