Posts

Showing posts from July 23, 2013

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar lakamata silaha 7 na majambazi 8 na pia lakanusha Mh. Mnyika kukoswa na bomu.

Image
  Baadhi ya askari polisi wakionyesha kwa waandishi wa habari silaha zilizokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa matukio ya ujambazi. DCP Mlege akitoa taarifa ya mafanikio ya Jeshi hilo kwa waandishi wa habari ambapo akizungumzia suala la Mh. Mnyika amesema askari No. E. 5340 D/CPL Julius aliyekuwa ndani ya gari la polisi PT. 1902 alikuwa anasogeza boksi lenye mabomu ya kutoa machozi ya kurusha kwa mkono, kwa bahati mbaya bomu hilo lililipuka ndani ya gari hilo na halikuleta madhara yeyote kwa askari polisi wala raia waliokuwa eneo la uwanja wa Sahara uliopo Mabibo ambako chama cha CHADEMA kilikuwa kifanye mkutano wa hadhara tarehe 21 Jula 2013 kinyume na utaratibu. Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata sila 5 ikiwemo SMG moja, Shortgun mbili, Riffle Mark 3 tatu, Pisto moja, Risasi 56, Maganda ya Risasi 17 na Majambazi 8. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kwa niaba

RAIS KIKWETE LEO AKUATANA NA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU

Image
RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MPITO WA WA MADAGASCAR IKULU   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa serikali ya mpito ya Madagascar Mhe Andy Rajoelina Ikulu jijini Dar es salaam leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza  Rais wa serikali ya mpito ya Madagascar Mhe Andy Rajoelina baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo . RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA LEO IKULU Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwonesha mandhari mbalimbali Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAKAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi na Bw. Manoj Kohli wa Airtel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Pamoja wa chama hicho alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Beatrice Singano, mmoja wa wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na  wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.PICHA NA IKULU

KASI YA MAAMBUKIZI YA VVU/UKIMWI YAPUNGUA HALMASHAURI YA MOSHI

Image
Kasi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi imepungua katika Halmashauri ya Moshi baada ya kuanzisha kampeni za kuhamasisha jamii kupima afya zao kwa hiari kwa kutumia vikundi mbalimbali vya sanaa za maonyesho . Mratibu wa UKIMWI wa Halmashauri ya Moshi Benedicto Rwamuruku amesema ,kampeni hiyo wamaeanzisha baada ya kuona mafanikio ya elimu iliyotolewa awali  kwa njia ya sinema imewafikia jamii na maambukizi yamepungua. Aidha ameongeza kuwa maambukizi hayo yamepugua kutoka wastani wa asilimia 1,6 hadi kufikia asilimia 1.3 miaka mitaano iliyopita na lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi  hayaogzeki kwani Tanzania bila ukimwi inawezekana.

YUSUF MLELA AFUNGUKA KUMRITHI SAJUKI KWA WASTARA

Image
Jul 23 2013 BAADA ya wiki iliyopita kumleta kwenu staa wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela ili mumuulize maswali, leo tunawaletea majibu na ufafanuzi wa maswali mliyomuuliza. SHUKA NAYO… HUYU ANAMKUBALI Mimi ninakukubali kinoma kwa sababu huna majivuno wala skendo kwa hiyo kaka endelea hivyohivyo. Calvin Mabula, 0719371176 MLELA: Asante. ONGEZA UBUNIFU Nakupa hongera kwa uigizaji wako lakini pia ongeza ubunifu, skendo usizipe nafasi hazitakujenga bali zitakubomoa. Kelvin Mwaibula, 0713644447 MLELA: Asante kwa ushauri wako nitaufanyia kazi. YEYE NA WASTARA Mlela umeanzia mbali enzi zile ukiwa bado chalii, nakuombea heri uendelee kuwa nyota, fafanua kuhusu uhusiano wako na Wastara (Juma) maana tayari watu wanasema unataka kumrithi (Juma Kilowoko (Sajuki). Rocky, Moshi, 0715289337 MLELA: Wastara ni mtu wangu wa karibu sana tangu Sajuki akiwepo, tunafanya kazi

WALIOWAUA WANAJESHI WA TANZANIA WATAJWA.....NI KUNDI LA "JANJAWEED" LINALOUNGWA MKONO NA SERIKALI YA SUDAN

Image
WAKATI miili ya wanajeshi saba ikiwa imeagwa jana katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, imeelezwa kuwa kundi la Janjaweed linaloungwa mkono na serikali ya Sudan ndilo lililowavamia na kuwaua askari hao nchini humo  na kuwajeruhi wengine 17 . Wanajeshi hao wa Tanzania ambao walikuwa ni sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), walifanyiwa unyama huo Julai 13, mwaka huu katika eneo la kusini mwa Darfur, nchini Sudan. Kiongozi wa moja ya makundi ya wapiganaji la Sudan Liberation Movement (SLM), Minni Mannawi ameibuka na kuwatuhumu wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo na ametaka ufanyike uchunguzi wa kimataifa. Katika mahojiano yake na Gazeti la Sudan Tribune alipokuwa anahudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu namna ya kupata amani ya kudumu nchini Sudan uliofanyika jijini Geneva Uswisi wiki iliyopita, alikanusha kuwa kundi lake linahusika na shambulio hilo.   “Tuna uhakika shambu

VIJANA WAUANA JIJINI MBEYA WAKIGOMBANIA PENZI LA MSICHANA

Image
Mnamo tarehe 21/07/2012 majira ya saa 23:30hrs huko kijiji cha Nkwangu wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya, Seni s/o Sandu, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na Tolo s/o Seko, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu. Chanzo ni ugomvi wa kumgombania msichana aitwaye Holo d/o Kulwa, miaka 16, Msukuma mkulima na mkazi wa Nkwangu. Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa. Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza. Signed by, [Diwani Athumani – ACP] kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya.  Source: Watemi

WANAOPINGA KODI YA LINE ZA SIMU NI WANAFIKI WASIOPENDA MAENDELEO.

Image
  Wakati Serikali ikiahidi kutazama upya tozo ya Sh 1,000 kwa laini za simu ili kupunguza mzigo kwa wananchi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema tozo hiyo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini. Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma, baada ya kuutembelea mkoa mpya wa Njombe. “Ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petroli, ambayo imetupa fedha nyingi kwenye Mfuko wa Barabara, za kuunganisha miji na mikoa na nyingi zimejengwa na zinaendelea kujengwa. “Nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vid ogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema,” alisema Pinda. Bunge la bajeti lililomalizika mwezi uliopita, lilipitisha tozo ya

POLISI WAFANIKIWA KUMKAMATA MVUTA BANGI ANALIYEMUUA MDOGO WAKE KWA KUMKATA MAPANGA HUKO SINGIDA

Image
 Jeshi la polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kumkamata Elibariki Alphoce (21) mkazi wa kijiji cha Kizega wilaya ya Iramba, anayetuhumiwa kumuua mdogo wake Mariam (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Kizega. Elibariki anatuhumiwa kumuua mdogo wake Mariam Julai 16 mwaka huu katika kijiji cha Kizega kwa kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuteganisha kichwa na kiwiliwili. Ilielezwa kuwa Elibariki ni mtumiaji sugu wa madawa ya kulevya aina ya bangi. Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Julai 18 mwaka huu akiwa amejificha kando kando ya mto Ruruma wa kijiji cha Ruruma tarafa ya Kiomboi. 

DIAMOND PLATNUM AZUNGUMZIA KIFOCHAKE SOMA HAPA

Image
Msanii anayefanya vizuri sana kwa sasa Afrika mashariki Nasib Abdul aka Diamond Platnumz amezungumza maneno mazito aliyokiri huwa yanamtoa machozi, ni mambo yanayohusiana na ‘kifo chake’!. Dakika chache zilizopita hit maker huyo wa ‘Kesho’ ame post picha Instagram yenye sura yake na maswali yanayouliza nini kitatokea baada ya kifo chake. Tazama picha hiyo inazungumza yenyewe Picha hiyo ilisindikizwa na caption hii “One of my songs,always gets me crying whenever I listen to it, how I wish u would hear it, but then again I have no clue as to when I will release it… #WCB” Platnumz amekaa kimya bila kutoa wimbo mpya kwa muda sasa, je unahisi kuna uwezekano ‘KAMA NIKIFA KESHO’ ukawa ndio ndio wimbo mpya anaotegemea kuachia hivi karibuni? Tusubiri tuone!

HUU NDO MWONEKANO MPYA WA JOKATE MWEGELO

Image
TUPE MAONI YAKO KWA KUJIUNGA NASI KATIKA UKURA WA FACEBOOK

LWAKATARE KWENDA INDIA KUTIBIWA

Image
Mahakama yaridhia Lwakatare kwenda India kwa matibabu Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema, Willifred Lwakatare akizungumza kuhusu hali ya ugonjwa wake akiwa katika Tasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix  Na James Magai,Aziza Masoud  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imempa kibali Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, akatibiwe nje ya nchi. Lwakatare ambaye anasumbuliwa na maumivu ya shingo, kwa sasa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa uangalizi maalumu na kufanya mazoezi, alipata kibali hicho kwa kuwa anakabiliwa na kesi ya kula njama za kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky. Wakili wake, Nyaronyo Kicheere alililiambia gazeti hili nje ya mahakama kuwa Lwakatare anatarajiwa kupelekwa India, lakini akasema tarehe ya kusafi

NAY WA MITEGO ATANGAZA KUMPIGIA KAMPENI LOWASA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2015

Image
Haya  ni  mashairi  aliyoyaandika Nay wa  mitego  kwenda  kwa  mtoto  wa  Rais  a.k.a Riz One  akimtaka  amwambie  baba  yake  kuwa  mtwara  hawataki  korosho, wanataka   gesi  na  pia Lowassa  asiache  kugombea  urais  maana  yupo  tayari  kumpigia  kampeni-2015 ---------------- MASHAIRI YAKE: Naongea na Riz one hey Riz One, we si mtoto wa raisi Riz one. Mwambie dingi yako Masela hawamuelewi wamakonde wa Mtwara hawataki tena Korosho, wanaitaka ges si mtawaua na mkong'oto?! Nani rafiki wa Lowasa anifikishie salam 2015 nataka agombee uraisi nitamfanyia kampeni wananchi wampe nafasi,  # Salam zao#  my new track coming soon.!! Credit:djchoka

FFU WAPINDUKA NA GARI NA MMOJA WAO KUFARIKI PAPO HAPO WAKATI WAKIELEKEA KWENYE ENEO LA TUKIO KUZUIA MAANDAMANO HUKO KILIMANJARO..!

Image
ASKARI mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoani Kilimanjaro, Fidelis Mwaliyatabu, amefariki dunia papo hapo na wengine tisa akiwamo Mkuu wa Kikosi hicho kujeruhiwa vibaya baada ya gari lao kupinduka katika kijiji cha Kilingi, wilaya ya Siha, wakati wakienda kuzima vurugu za wananchi. Ajali hiyo ilitokea wakati kikosi hicho kikielekea katika kijiji cha Karansi kwa ajili ya kukabiliana na wananchi waliokuwa wakiandamana kupinga wenzao waliokamatwa usiku wa manane baada ya kuvamia mashamba mali ya Shirika la Roho Mtakatifu-Kilasara. Taarifa kutoka kijijini humo zilieleza kwamba wanakijiji waliamua kuandamana baada ya wenzao watano kukamatwa na Jeshi la Polisi nyakati za usiku kwa mahojiano kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kushawishi wanakijiji wenzao kuvamia maeneo ya Shule ya Kilasara na kusababisha hasara kubwa kwa shule hiyo. Kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa hao, wanakijiji waliamua kuaandamana hadi katika kituo cha polisi ili kuwatoa wenzao ha

MALKIA WA UINGEREZA APATA KITUu ,MKE WA MJUKUU WA MFALME APATA MTOTO WA KIUME

Image
kate and William are thrilled to welcome a baby boy into  the royal  family! His Royal Highness Prince of Cambridge was born on July 22 at 4:24 p.m. GMT weighing eight pounds, six ounces, and  Prince William  was present for the birth! While the world has been keeping a major watch on Kate waiting for her to give birth, everyone has also been eagerly awaiting the announcement of the gender, as Kate and William never revealed it — because they didn’t know either! Now that we know that the baby is a boy, we are so excited to know the future heir to the throne will succeed the line of men  that are  set to take the throne after Queen Elizabeth. The baby is now third in line of succession after his grandfather, Prince Charles and his father, Prince William. Kate Middleton Has Baby Boy: Kensington Palace’s Announcement Kensington Palace released any official statement confirming the good news: Her Royal Highness The Duchess of Cambri

HATIMAYE AMINA SAIDI AAMUA KWENDA KUMZIKA MSOFE TANGA.

Image
Amina Juma.     MT 97024 PTE Fortunatus Wilbard Msofe- 36 KJ. KIBAHA.  MCHUMBA   wa marehemu, Fortunatus Msofe, ambaye ni mmoja wa wapiganaji wa JWTZ, waliofia Darfur, ameondoka kwenda Tanga kumzika mwenza wake huyo. Mwanamke huyo Amina Juma, amekataliwa na ndugui wa marehemu ambao wameifunga kwa kufuli nyumba inayodaiwa kuwa amejenga marehemu. Akizungumza na gazeti hili jana, Amina alisema ingawa awali alikata tamaa ya kumzika mwenzake, lakini jana aliamua kwenda Tanga kuhudhuria mazishi na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya kujishauri sana. Baba wa marehemu, Wilbad Msofe aliiambia gazeti hili kutoka Kange, Tanga kuwa alishangazwa na hatua ya Amina kutowafahamisha kuhusu msiba huo. Alisema hiyo ndiyo sababu za yeye kuamua kutaka mwanawe apelekwe Kange kwa mazishi.