Posts

Showing posts from November 25, 2013

SAFISHA MACHO MTU WANGU WA NGUVU

Image
baada ya uchovu wa foleni sina budi kupunga upepo kwa muda

LADY JAY DEE AMVAA JANUARY MAKAMBA LIVE

Image
Lady Jaydee Lady Jaydee kweli ni Anaconda na sio mtu wa kuchezea kwani ukiingia kichwa kichwa kwenye kumi na nane zake anakumeza na kukupaka live kama huna hoja ya msingi. Hayo yamempata Mbunge wa Bumbuli January Makamba. Angalia alichoandika Makamba hapo chini na jibu la Lady Jaydee ambaye ni mwanamuziki mwenye jina kubwa Afrika mashariki.

MSANII SNURA AFIWA NA KAKA YAKE WA TUMBO MOJA APATWA NA AJALI YA RADI MLANDIZI

Image
 msanii SNURA kafiwa na kaka yake wakuzaliwa nae anaejulikana kwa jina la Yusufu kaka yake wa kwanza kuzaliwa kwa marehemu baba yake mzee Mushi. Msiba huo umetokea Mlandizi baada ya kupigwa na radi kali jana asubuhi wakati marehemu akiwa shambani kwake Mlandizi. SNURA akiongea na blog hii  amesema wanazika leo huko huko Mlandizi mida ya saa kumi jioni.   Mungu alaze roho ya maehemu YUSUFU MUSHI mahala pema peponi. AMIN

MTOTO MIAKA 6 ALAWITIWA, AHARIBIWA!

Image
Stori: Joseph Ngilisho, Arusha   Dunia haina huruma! Mtoto wa kiume ambaye ni denti wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka sita anayesoma katika shule moja ya msingi iliyopo Olasiti jijini hapa, anadaiwa kulawitiwa hadi kuharibiwa vibaya sehemu za siri. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea hivi karibuni, inadaiwa kuwa kitendo hicho kilifanywa na kinyozi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50. Akizungumza akiwa na shangazi yake  katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru alikolazwa akipatiwa matibabu, mtoto huyo alimtaja mtuhumiwa kwa jina moja la Abuu, mkazi wa eneo hilo ambaye alimrubuni mwathirika huyo kwa ofa ya kumnyoa nywele. Alidai Abuu amekuwa akimfanyia mchezo huo mchafu majira ya mchana au usiku katika nyumba ambayo haijamalizika kujengwa (pagale) na wakati mwingine humzungusha nyuma ya saluni yake. Ilidaiwa kuwa hali ilikuwa mbaya baada ya mtoto huyo kushindwa kutembea na kutokwa na haja kubwa bila mpangilio

Malkia wa nyuki aandika barua kujitoa Simba

Image
Malkia wa Nyuki akiwa ofsini kwake. Na Mwandishi Wetu MALKIA wa Nyuki ameandika barua ya kujiondoa kwenye Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba kutokana na kuchukizwa na migogoro. Malkia ambaye jina lake halisi ni Rahma Al Kharusi, amethibitisha hilo na kusema aliamua kufanya hivyo kutokana na kukerwa na migogoro ndani ya kamati hiyo. Akizungumza jana kutoka Oman, Malkia wa Nyuki alisema aliamua kujiondoa kwa mambo mawili makubwa ambayo ni migogoro na kukosa nafasi. “Baada ya kumueleza Rage kwamba nimefikia uamuzi huo, ameniomba nibaki kwa kuwa ninahitajika Simba. Kanishauri kwamba niingie katika upande wa baraza la wadhamini. Kwangu naona si mbaya, maana sitakuwa na vikao vya mara kwa mara, lakini bado nasisitiza migogoro si sahihi,” alisema.   “Kwani kama si kuteuliwa katika nafasi hii ya kusimamia mali za Simba, basi nilikuwa nimeshajiondoa kabisa Simba hadi hapo hali itulie maana

MH. LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KATA YA SARANGA,KIMARA JIJINI DAR

Image
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiburudika kwa kucheza muziki sambamba na wakina Mama wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam,Mwishoni mwa wiki wakati alipokwenda kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo.Zaidi ya Sh. Mil. 100 ziliweza kupatikana kwenye harambee hiyo.  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipena mikono na Wakazi mbali mbali wa Kata ya Saranga,Kimara wakati akiendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki.  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisisitija jambo kwa wananchi wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya p

KINANA AANZA ZIARA RASMI MKOANI MBEYA

Image
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ipinda wilayani Kyela kwenye mkutano wa hadhara ambao ndio mkutano wake wa kwanza kama Katibu Mkuu wa CCM lakini pia ndio siku aliyowasili akitokea Ruvuma .  Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakazi wa Ipinda wilaya ya Mbeya na kuwasihi wakina mama wawe mstari wa mbele kuhakikisha mabinti zao wanapata elimu.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ipinda na kuwaeleza mambo muhimu ya kutafakari kabla hawjakurukupia siasa na baadhi ya vyama vingi vipo kwenye mfumo na utawala binafsi.  Mbunge wa Kyela Dk. Harisson Mwakyembe akihutubia wakazi Ipinda wa kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa Nyumbani kwa Balozi wa Nyumba 10 Ndug