Posts

Showing posts from August 21, 2013

KWELI NAWEZA SEMA SAFARI SIO KIFO ILA.......................

Image
  Tazama maisha ya Mtanzania yanavyozidi kuwa hatiani kila kukicha, hapa nia abira wakionekana kugombania usafiri na wengineo wakiwa wako juu ya keria ili mradi tu wafike waendako. JE NAULI INALIPWA KWA WOTE? Uko nchi ya jirani Kenya nako hali ya usafiri imekuwa ngumu kila kukicha, hawa nia abiria waliokutwa na kamera zetu wakiwa wamejazana kwenye matatuu nao hitaji lao ikiwa nikufika waendako bila kujali uasalama wa maisha yao

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AFANYA MABADILIKO MAKATIBU WAKUU

Image
NA MAGRETH   KINABO NA ELEUTERI MANGI – MAELEZO RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu katika wizara mbalimbali, ambapo  wapo waliohamishwa, wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.  Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. “Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali  katika ngazi hizo za juu,”alisema Balozi Sefue.  Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa makatibu wa wakuu ni kama ifuatavyo; Dk. Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Joyce Mapunjo Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki(awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara

ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA PHILIP MANGULA

Image
Mwakilishi wa Mheshimiwa Rais katika mazishi ya Nemela Mangula Mh. Anne Makinda akiwa ameongozana na Mh. Wassira na viongozi wengine wakipitia wosifu wa marehemu pamoja na ratiba za mazishi. Wana familia na waombolezaji wakiwa katika hali ya huzuni. Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Nemela Mangula,mkoani Njombe.  Jeneza la Neema Philip Mangula  Watumishi wa CCM Makao Makuu wakibadilishana mawazo na Viongozi wa Dini wakati wa mazishi ya Neema Mangula. Mahala ulipopumzishwa mwili wa Neema Mangula.

MUUMINI NA WAZIRI SONYO WACHAPANA MAKONDE NA KUTAKA KUPIGANA VISU LIVE WAKIWA MAZOEZINI KWENYE BENDI

Image
WANAMUZIKI wawili wenye majina ya kutisha, Waziri Sonyo na Rais wa zamani wa bendi ya Victoria Sound, wamepigana katika mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam.    Waziri Sonyo kushoto. Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika ya aina yake inayoendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya Victoria Sound. Akizungumza muda mchache baada ya kadhia hiyo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi. Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo. “Leo ndio nimedhihirisha huyu ( hapa kuna tusi ila limefichwa kwa sababu za kiungwana) ni kweli yy amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza

ANGALIA PICHA ZA MAPOKEZI YA FEZZA KESSY NCHINI BOSTWANA

Image
Akiwa Katika Gari la wazi mara baada ya kupokelewa uwanja wa Ndege wa Bostwana..

AJALI YA LORI NA GARI NDOGO MOROGORO

Image
Gari Aina ya Prado tz ikiwa imepata ajali kwa kugongwa la lori la mizigo jana usiku Maeneo ya Nane Mkoani Morogoro.Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba Chanzo Cha Ajali hiyo ni Uzembe wa Dereva wa Gari ndogo aina ya Prado iliingia barabara kuu bila kuangalia pande zote kama kuna gari nyingine na ndipo alipoingia na kukutana la Lori La Mizigo likiwa kwenye Mwendo kasi na ndipo lilipoligonga gari hilo.Kwenye Gari Dogo alikuwa dereva Mwenyewe Hakuna Mtu Aliyepoteza maisha. Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa eneo la tukio wakiliangalia gari hilo lililopata ajali Eneo la Nane nane Mkoa wa Morogoro jana usiku.Picha na   MATUKIO NAMICHAPO BLOG Picha ya gari hilo mara baada ya kuondolewa eneo la tukio na hivi ndiyo lilivyoharibika baada ya Ajali Hiyo Askari Polisi wakiwa Eneo la tukio muda Mfupi Mara baada ya ajali hiyo kutokea Askari wa usalama barabarani akiwa eneo la tu

ANGALIA PICHA YA BINADAMU MWENYE KILO 610 APELEKWA RIYADH, SAUDI ARABIA KWA UPASUAJI

Image
Khalid Mohsen akishushwa toka ghorofa ya pili kwa folklift nyumbani kwake mjini wa Jazan nchini Saud Arabia kwa ajili ya kupelekwa Kwenye Hspitali ya Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia kwa upasuaji Khalid Mohsen akiwa kwenye Folklift kupelekwa uwanja wa ndege tayari kusafirishwa Riyadh, mji mkuu wa nchi hiyo kwa ajili ya upasuaji.   Khalid Mohsen akiingizwa kwenye ndege kutumia Folklift.  Khalid Mohsen akitolewa kwenye tolitoli mara baada ya kuwasili Hospitali ya Riyadh  

HII NDO KAULI YA DIAMOND BAADA YA KUHUSISHWA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

Image
Msanii Wa Muziki wa Bongofleva mwenye jina kubwa Town na mwenye Mkwanja mkubwa hapa nchini Nasseeb Abdulmaliki “Diamond” amejitokeza na kukanusha kuwa hahusiki na biashara ya madawa ya kulevya.   Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa za Diamond kujihusisha na biashara hiyo hasa kutokana na ukaribu wake na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini.  Taarifa zaidi zinasema ni wafanyabiashara hao waliohusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kifo chake ziligubikwa na matumizi ya madawa ya kulevya. Akikanusha taarifa hizo Diamond amesema  :   “ Ni kweli mimi nina pesa za kutosha kuniwezesha kuishi maisha ninayotaka lakini sijawahi kujihusisha na biashara hiyo . ... "Kufanya kazi kwa bidii kunalipa na kazi yangu inaonekana na ndiyo inayoniwezesha kuwa na fedha ambazo leo watu wameanza kuzitilia shaka. Sielewi nia ya watu hawa ni nini?”

ALHAJ MWINYI NA MZEE MKAPA WAWASILI ZIMBABWE KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS MUGABE

Image
Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Benjamin William Mkapa pamoja na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiwasili katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Harare, Zimbabwe, walikoalikwa kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe. Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Agosti 21, 2013.   (PICHA NA IKULU)

GODLESS LEMA AUGUA GHAFLA, KESI YAKE YAAHIRISHWA

Image
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha jana imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, kutokana na mbunge huyo kuwa mgonjwa. Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Hawa Mguruta, anayesikiliza shauri hilo kuwa Lema anaumwa na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya AICC tangu Agosti 14 hadi 19, mwaka huu aliporuhusiwa kutoka hospitali, hivyo ametakiwa apumzike kwa muda wa siku 10 kuanzia Agosti 19, mwaka huu.   Wakili Kimomogoro aliomba shauri hilo liahirishwe hadi siku nyingine, ombi lililokubaliwa na hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 1 na 2 mwaka huu, ambapo mashahidi tisa wanatarajiwa kutoa ushahidi wao. Wakili wa Serikali, Elizabeth Swai, anayesaidiana na Mary Lucas, alikubaliana na ombi hilo na kuongeza kuwa mashahidi wanne miongoni mwa tisa walikuwapo mahakamani hapo kutoa ushahidi wao jana ambao ni Mkuu

ANGALIA PICHA ZA MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE ULIVYOPATA AJALI MKOANI DODOMA:

Image
MBIO za Mwenge wa Uhuru uliokuwa ukikimbizwa katika Wilaya ya Dodoma mjini zimeingia Dosari baada ya kupata ajali kilometa 3 kabla ya kukabidhiwa wiliya ya Mpwapwa. Ajali hiyo iliyotokea jana majira ya 2;24 asubuhi katika mtelemko wa mlima fufu wilayani Chamwino na kusababisha watu 5 kujeruhiwa na kukimbizwa katika hospital ya mkoa wa dodoma. Watu hao ambao majina yao Bado hayajatambulika walipata majeraha katika maeneo mbali mbali ya miili yao ikiwemo kichwani, kifuani, mguuni na mikononi. Kaimu Kamanda wa polisi Suzan Kaganda aliyefika na kujione hali ilivyokuwa katika eneo hilo alisema chanzo cha ajali hiyo ni Matuta yaliwekwa kwenye Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami toka fufu hadi Dodoma bila kuwa na alama yoyote.  majeruhi akisaidiwa kupekwa kwenye gari tayari kukimbizwa hospital  gari iliyokuwa imembeba kiongozi wa mbio za mwenge ikiwa imeumia vibaya  majeruhi wakipatiwa hud

Basi la Turu lachomwa moto na wanakijiji....Abiria 60 wamenusurika

Image
  Abiria wapatao 60 waliokuwa wanasafiri na basi la Turu linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Singida na Haidom mkoani Manyara, wamelazimishwa kuteremka toka ndani ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 ) wa vijiji vitatu, na kisha kulichoma moto basi hilo. Taarifa toka eneo la tukio zinasema wananchi hao ni wa vijiji vya Singa, Idabagadu na Nkungi mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria wote wameshuka, walilichoma moto basi hilo ambalo limetekea sehemu kubwa. Sababu ya wananchi hao kuchukua uamuzi huo ni kutokana na basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita

MERKEL APENDEKEZA MARUFUKU YA SILAHA MISRI

Image
Ujerumani imependekeza kupiga marufuku upelekaji wa silaha nchini Misri kama hatua itakayoratibiwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya kupinga hatua ya serikali ya Misri ya kuvunja maandamano kwa kutumia nguvu na kusababisha umwagaji damu. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ametowa wazo hilo katika mahojiano na televisheni la taifa hapo jana. Kansela Merkel amesema hatua zote zinaweza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kupeleka silaha nchini Misri zikiwemo zile ambazo tayari zimeidhinishwa kwa serikali ya Misri. Amesema suala hilo litajadiliwa kati ya Ujerumani na washirika wenzake wa Umoja wa Ulaya katika mkutano utakaofanyika siku chache zijazo. Umoja wa Ulaya utakuwa na kikao chake cha kwanza cha mazungumzo ya dharura kutokana na umwagaji damu nchini Misri uliozusha wasiwasi mkubwa huku ukionya kwamba utaangalia upya uhusiano wake na nchi hiyo iliokumbwa na ghasia.

ANGALIA PICHA ZA MJUSI MKUBWA WA TANZANIA ALIEKO UJERUMANI ANAYETAKA KURUDISHWA

Image
  The governments of Tanzania and Germany will soon strike an agreement for the return to Lindi region of the remains of huge lizard species known as a dinosaur, which were taken to the European country during the colonial era, Parliament heard yesterday. The dinosaur remains were discovered in 1912 at Tandeguru village, Mipingo ward in Lindi region, and were taken for preservation in Humbolt museum. Dinosaur Skeleton

HII NDIO HISTORIA FUPI YA MAISHA YA ANTI EZEKIEL ALIKO ANZIA MPAKA SASA.ISOME HAPA

Image
JINA la Aunt Ezekiel siyo geni  kwa wadau mbalimbali wa burudani hapa nchini, ni staa ambaye hivi sasa ana jina kubwa kupitia sanaa yake ya uigizaji wa filamu aliyoianza miaka sita iliyopita. Japokuwa kwa sasa ni staa, amepitia mambo mengi magumu katika safari yake ya maisha mpaka kufikia hapo alipo hivi sasa. Aunt alizaliwa mwaka 1988 mkoani Dar es Salaam, baba yake akijulikana kama Ezekiel Grayson’ Jujuman’ ambaye alikuwa ni mchezaji hodari sana wa timu ya Simba. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Bunge mwaka 1993 hadi 1998. Alienda kumalizia darasa la saba katika Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Kisarawe, mkoani Pwani. Vipi maisha yalikuwaje baada ya kumaliza shule? “Kwa kweli maisha yalikuwa ni magumu mno kwa maana nilipomaliza shule tu, alijitokeza mwanaume na kutaka kunioa kitu ambacho mimi sikukipenda kabisa lakini baba yangu alitaka hivyo kwa vile uwezo wa kunisomesha hakuwa nao tena na maisha yalikuwa ni magumu sana. “Ba